Nyumba ya Gavana wa Benki Kuu yaanza kukaguliwa; WAZIRI MKULO umejiaibisha!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyumba ya Gavana wa Benki Kuu yaanza kukaguliwa; WAZIRI MKULO umejiaibisha!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Mar 31, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  waziri wa fedha aliutangazi umma akuna haja ya kuendelea na 'ukaguzi wa nyumba ya gavana maana gavana amejibu kila kitu kwenye tume ya wabunge alioitwa kuulizwa

  EMBU TUELEZE WAZIRI MKULO NA HUU UPUUZI UNAFANYWA WA NINI KAMA UNADIRIKI KUTAMKA KUMSAFISHA MTU KWA MASLAHI YAKO BINAFSI NAONA UNAJIAIBISHA KWELI... USIKURUPUKE KUBWAABWAJA...HAYA KAZI HIYO CHNI

  Nyumba ya Gavana wa Benki Kuu yaanza kukaguliwa

  Na Sadick Mtulya

  TIMU ya wataalamu wa majengo kutoka ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeanza kukagua thamani ya nyumba za gavana wa Benki Kuu (BoT) na naibu wake ambazo zimeelezwa kuwa zilijengwa kwa jumla ya ShSh2.5 bilioni.

  Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa ukaguzi huo wa nyumba za Profesa Benno Ndulu na mmoja wa manaibu gavana wake zilizo Masaki jijini Dar es Salaam ulianza wiki iliyopita.

  Ukaguzi huo unafanyika baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) kuagiza kufanyika kwa uchunguzi huo Januari 21 mwaka huu katika mkutano wake na gavana Ndulu.


  Taarifa ya matumizi hayo makubwa ya fedha kwa ajili ya kujengea nyumba mbili za watumishi hao wa umma ziliripotiwa kwa mara ya kwanza na gazeti hili zikionyesha kuwa nyumba ya gavana ilikarabatiwa kwa takribani Sh1 bilioni.


  Lakini baadaye BoT ilitoa ufafanuzi ikieleza kuwa nyumba hizo hazikukarabatiwa bali zilijengwa upya kwenye viwanja vya BoT na kwamba baada ya taratibu zote za zabuni kufuatwa, nyumba hizo kujengwa kwa gharama ya takribani Sh1.274 bilioni kila mmoja.


  Mwenyekiti wa POAC, Zitto Kabwe aliliambia gazeti hili jana kuwa ukaguzi huo utachukua wiki tatu na baada ya hapo ripoti yake itatangazwa bungeni.


  "Tayari timu ya wataalamu wa majengo kutoka ofisi ya CAG wamekwishaanza ukaguzi wa matumizi ya ujenzi wa nyumba mbili za kuishi magavana wa Benki Kuu," alisema Zitto.


  "Wanafanya hivyo kutokana na agizo la POAC lililotolewa katika kikao chake cha mwezi Janauri mwaka huu. Kamati ilimwagiza CAG afanye ukaguzi wa matumizi ya fedha zilizotumika katika ujenzi wa nyumba hizo. Ukaguzi huo utakuwa ni wa wiki tatu."


  Zitto, ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini, alisema kuwa Jumatano iliyopita alipokea barua rasmi ya CAG, Ludovick Otouh ikimjulisha kuwa ukaguzi huo umeshaanza.

  "Alinitaarifu kuwa timu ya wataalamu wake wa majengo imeanza kufanya ukaguzi katika majengo ya magavana wa BoT," alisema Zitto.

  Alifafanua kuwa lengo la kamati yake kuagiza ukaguzi huo ni kujiridhisha baada ya Profesa Ndulu kuwasilisha ripoti ya BoT kuhusu matumizi hayo ya kutisha kwenye kikao cha kamati hiyo cha Januari 21 mwaka huu.


  Kwa mujibu wa Zitto, ripoti ya ukaguzi huo itawasilishwa kwake baada ya kukamilika ukaguzi huo na kamati kuiwasilisha bungeni katika ripoti yake ya mwaka katika bunge hili la Aprili.


  "Matokeo ya ripoti ya CAG kuhusu matumizi ya ujenzi wa nyumba hizo, yatatangazwa katika ripoti ya mwaka ya kamati yangu bungeni,'' alisema Zitto.


  Awali kabla ya BoT haijajibu tuhuma za matumizi hayo ya fedha, Profesa Ndulu alikiri matumizi hayo lakini akafafanua kuwa kilichofanyika ni kujenga upya nyumba hizo na sio kuzikarabati.


  "Nyumba haijakarabatiwa bali imejengwa from the ground (kutoka chini)... ni tofauti kukarabati na kujenga nyumba mpya huu, ni upotoshaji wa wazi na kujaribu kuchafua mema," alilalamika gavana huyo.
   
Loading...