Nyumba ya Dr. Dau yavamiwa; vitu vyaibwa, vingine vyarudishwa kiana

Vladmir Semilong,

Ni bahati mbaya nyumba yake kuvamiwa na maisha yake kuwa hatarini. Lakini kuna haya ya msingi ya kujiuliza.

Huyu ni mtu ambaye tuliambiwa alipaswa kuwa Gavana wa Benki Kuu na anaweka fedha nyingi sana nyumbani!

Je hizi fedha nyingi ni kiasi gani? au tafsiri ya fedha nyingi ni nini?

Kwa nini aweke fedha nyingi nyumbani? Ningeelewa japo angekuwa na shilingi Milioni moja na kusema hizi ni kipu chenji za dharura pale nyumbani, lakini akisema kaibiwa milioni kumi nyumbani tumhoji milioni kumi zinafanya nini nyumbani?

Yeye kama mchumi na mtaalamu wa masuala ya fedha aliyebobea, anausaidiaje uchumi wa Tanzania kudhibiti thamani na mzunguko wa shilingi ya Tanzania ikiwa anahifadhi fedha nyingi nyumbani na si Benki?

Hata kama angedai ilikuwa ni kuwalipa vibarua, je vibarua ujira wao ni kiasi gani mpaka awe na "fedha nyingi" nyumbani? Je nyaraka hizi ni zake binafsi na mali zake binafsi au kuna nyaraka za shirika?

Inasikitisha sana unapoona Wasomi wanashindwa kuwa mstari wa mbele kufundisha umma wa Tanzania mambo endelevu. Kila siku tunapiga kelele Ujima wa Tanzania na Watanzania kuficha fedha kwenye godoro na nyaraka uvunguni badala ya kupeleka Benki hata kuweka kwenye sefu la vitu ambavyo ni fedha.

Wenzetu huweka nyaraka na vitu vya muhimu mahali pa salama panapolindwa na nyaraka na vitu hivi vya thamani huwekewa bima, kwa kuwa vyote vina thamani.

Sijui ni lini tutaanza kuyaleta Tanzania yafanyike kwa kweli na si kuendelea kuhubiri "wenzetu ulaya wameendelea" huku wewe ndio wa kwanza kuweka fedha kwenye chungu ukakichimbia kwenye udongo wenye mchwa!
Ni kweli mkuu nashukuru kwa haya uliyouliza maana ni maswali ya msingi sana. Hata hivo, who is Dr who keeps large sum of money at home
? Ni hela tu au na mambo mengine ya muhimu anayatunza ndani ya nyumba yake?
 
ukitaka kujua kama nchi ya Tanzania haina watu waliolemika ndo utajua hapa!...

"It is not the education which works but rather the effect of the education!"...

How can you justify ujambazi? unless you are a criminal minded person. So how many are criminal minded to that extent kujustify ujambazi? Halafu cha kushangaza mtu kaingiliwa na majambazi, watu mnaanza kuquestion pesa kiasi gani? what docs?


EPA,Meremeta etc ni ujambazi ambao watu wameuhalalisha.Tena ni wakubwa tu!
 
Ukitunza kiasi kikubwa cha hela nyumbani,ukiwa ULAYA utatuhumiwa kuwa ni MONEY LAUNDERING.
Lakini Tz ni sawa tu,CEO kufanya hivi,what a shame!
 
Habari Leo

SIKU moja baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau kuvunjiwa nyumba yake na kuibiwa, majambazi hao usiku wa kuamkia Ijumaa wamerudisha kwenye nyumba hiyo sehemu ya mali iliyoibwa ambayo ni bastola aina ya Bereta pamoja na risasi zake 20.

Dk. Dau alipoamka asubuhi amekuta silaha hiyo ambayo anaimiliki kisheria ikiwa na risasi zake 20 kama ilivyoibwa, ikiwa imetelekezwa ndani ya uwanja wa nyumba hiyo iliyovamiwa iliyoko eneo la Ada Estate, Kinondoni.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Dk. Dau ametaja mali zilizoibwa kuwa ni vyeti vya kuzaliwa vya watoto wake wote wanne, mkewe na yeye mwenyewe pamoja na vyeti vya shule hadi chuo vyake na vya mkewe.

“Wamechukua pia hati za kusafiria tano za mke wangu na watoto wangu wanne pamoja na hati za nyumba zangu tatu na hati ya kiwanja cha mke wangu,”
alisema.

Hati za nyumba zilizoibwa ni pamoja na nyumba wanayoishi Ada Estate; nyingine anazomiliki zilizoko Kisota Kigamboni na Kinondoni pamoja na hati ya kiwanja cha mkewe kilichopo Kisota, Kigamboni ambacho hakijajengwa.

“Pia wameiba sefu mbili zilizokuwa na fedha kati ya Sh milioni nne na tano, sina hakika na idadi kamili kwani sijazihesabu lakini ni kati ya hizo nilizokueleza,” alisema.

Mkurugenzi huyo alitaja vitu vingine vilivyoibwa kuwa ni televisheni aina ya Hitachi iliyokuwa chumbani kwake.

Hata hivyo hakumbuki ukubwa wa televisheni hiyo na kuongeza, “bado tunaangalia kama kuna vitu vingine walivyochukua ila kwa harakaharaka ni hivyo nilivyokutajia”.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova alithibitisha kuibwa kwa vitu hivyo na kuongeza kuwa kupatikana kwa bastola hiyo na risasi 20 zake ni matokeo ya msako mkali wa Polisi unaofanywa tangu kutokea kwa tukio hilo.

“Polisi tunafanya msako mkali msione vitu vinarudi tu, ni matokeo ya msako wetu na tunawaambia majambazi hao warudishe kila kitu walichochukua kabla hatujawakamata na vielelezo hivyo,” alitoa amri.

Kova alisema licha ya kurudishwa bastola na risasi hizo, msako huo wa Polisi umesababisha vitu vingine vilivyoibwa na majambazi maeneo mengine ya jiji kurudishwa zikiwemo risasi 193 na kati ya hizo 36 za bastola aina ya Bereta, 132 za bunduki aina Riffle na 25 za bunduki aina ya Shot gun na saa moja ya mkononi.

Alisema risasi hizo zilitupwa maeneo mbalimbali ikiwemo zilizotupwa aliposema kuwa ni karibu na nyumba ya Dk. Dau.

Usiku wa kuamkia Ijumaa ajambazi zaidi ya 10 walitoboa ukuta wa uzio wa nyumba ya Dk. Dau na kuingia ndani ambapo walifungua geti na kuingiza gari na kuiba vitu mbalimbali. Sambamba na hilo, waliwafunga walinzi wawili kwa kamba na kufanikisha uhalifu wao.

Hata hivyo wakati ujambazi huo ukifanyika, familia ya Dk. Dau haikuwepo nyumbani hapo bali walikuwepo Kigamboni kwenye nyumba yao nyingine walipokwenda kwa mapumziko ya wikiendi.

Kamanda Kova alisema walinzi hao bado wanashikiliwa kwa mahojiano na watafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya uchunguzi kukamilika.

Walinzi hao ni Deus Mtatilo (52) mkazi wa Kinondoni-Hananasif na Yusuf Bakari (56) mkazi wa Ubungo.

My Take:
Majambazi hawa ni sawa na wale waliomrudishia yule mdada Nyegesi sim card yake baada ya kuwaomba "kaka jambazi"..
 
maigozi nchini kwetu sasa yanavuka mpaka.nothing is serious.juzi bilioni tatu zimechukuliwa polisi waliochukua (sipendi kutumia neno kuiba kutokana na mazingira yenyewe) hawajulikani.leo tena huyu nae kavamiwa watu wameenda kurudisha bastola lol.mwizi gani anarudi kwenye eneo la tukio na mali alioiba? na inamaana baada tukio hilo nyumba bado haikuendelea kulindwa kiasi cha huyu mtu aliyerudisha kutojulikana?
 
Hahaha hahha maskini nchi yangu jamni hebu Mola tusaidie mwaka huu tutasikia na kuona mengi tuuu!!:angry:
 
Jambazi gani anaiba vyeti vya shule na hati za kuasafiria? Mheshimiwa anatuambia jambazi katafuta kitu cha kuchukua akaona hati za kusafiria na vyeti ?

Kuna kitu hakielezwi vizuri hapa.
 
Jambazi gani anaiba vyeti vya shule na hati za kuasafiria? Mheshimiwa anatuambia jambazi katafuta kitu cha kuchukua akaona hati za kusafiria na vyeti ?

Kuna kitu hakielezwi vizuri hapa.

mkuu maigizo ya nchini kwetu ni noma.na kamanda anakwambia usione vitu vinarudi kwani mskao wanaofanya si mchezo ha ha ha.
 
mkuu mwanakijiji dont sweat on this ,its a big joke. wametoboa ukuta,wakafungua geti na kuingiza gari ndani ,kwenye hivyo vyeti na hati ya nyumba ndio wamenimaliza kabisa lol.
 
Nafikiri jamaa waliona kukamatwa na silaha ya wizi tena ya kibosile ingekuwa soo, wakaamua kuirudisha.....
 
“Polisi tunafanya msako mkali msione vitu vinarudi tu, ni matokeo ya msako wetu na tunawaambia majambazi hao warudishe kila kitu walichochukua kabla hatujawakamata na vielelezo hivyo,” alitoa amri.

Hii kali ya mwaka!
 
Ama kweli ni 'animal farm' but kova na dau should know we are smarter than that, only fools can be tamed by such a joke! He who fools smarter people fools himself! Kwa hiyo kova anataka kutuambia jeshi letu la polisi limegeuka private investigation unit? Wakina jaji kapinga wameuawa mpaka leo wameshindwa kumpata muuaji, maalbino wanachinjwa kama kuku polisi haijawahi kuwakamata watuhumiwa leo dau aliyekua kigamboni mapumzikoni kaibiwa vitu ambavyo mpaka sasa havijui lakini vimerudi kwa kazi kubwa waliyofanya polisi 'what a joke' kachoka kazi huyo mr masifa si angemuachia msika aongee walau hahitaji kujikomba wala kufungamana na upande wowote
 
Nafikiri jamaa waliona kukamatwa na silaha ya wizi tena ya kibosile ingekuwa soo, wakaamua kuirudisha.....

Wakaamua kuirudisha? Yaani waliona kukamatwa na silaha ya kibosile ni noma, wakarudi nayo mpaka nyumbani kwake na kuirudisha bila kuogopa kukamatwa walipokuwa wanairudisha?

Hapa huyu Dau either hajaeleza vizuri au kuna kitu anaficha, majambazi hawaibi vyeti na pasi za kusafiria bwana.
 
Ama kweli ni 'animal farm' but kova na dau should know we are smarter than that, only fools can be tamed by such a joke! He who fools smarter people fools himself! Kwa hiyo kova anataka kutuambia jeshi letu la polisi limegeuka private investigation unit? Wakina jaji kapinga wameuawa mpaka leo wameshindwa kumpata muuaji, maalbino wanachinjwa kama kuku polisi haijawahi kuwakamata watuhumiwa leo dau aliyekua kigamboni mapumzikoni kaibiwa vitu ambavyo mpaka sasa havijui lakini vimerudi kwa kazi kubwa waliyofanya polisi 'what a joke' kachoka kazi huyo mr masifa si angemuachia msika aongee walau hahitaji kujikomba wala kufungamana na upande wowote

Huyu Kova ana ji incriminate. Tukichukulia maneno yake yaliyoripotiwa kwa direct quote kuwa ni kweli alisema, anataka kutuambia kuwa wanawajua majambazi na badala ya kuwachukulia hatua za kisheria wanaanza ku negotiate nao warudishe silaha, kisheria hapa si ameharibu ushahidi tayari?

Kamanda wa polisi kajua majambazi wameiba silaha, akawaambia wairudishe silaha haraka sana kabla hayajawakuta makubwa, kamanda wa polisi ashtakiwe kwa kuharibu ushahidi ungeoweza kuwatia hatiani majambazi.

Na kama anawajua mbona hawachukuliwa hatua mpaka leo?

Jamani tunajua bongo level ya analysis ndogo, lakini msiniambie hali ni mbaya kiasi hiki.

Huyu kamanda sanamu, kamanda wa kweli hawaambii majambazi warudishe ushahidi, kamanda wa kweli anaombea majambazi wasirudishe ushahidi ili awanase na kuwatupa mahakamani na ushahidi kamili.Sasa huyu kamanda anayetaka majambazi warudishe ushahidi ana mpango gani wa kutokomeza ujambazi, maanake tunaona kama anawaonea huruma majambazi, hataki kuwakamata na ushahidi.

I wish I was at a press conference na huyu b.w.e.g.e.
 
Sipendi kweli u - sherlok holmes...

Sasa baada ya kuwachukua wale walinzi wawili kuwashikilia polisi ili nyumba

a. Iliachwa bila ulinzi - kitu ambacho kitakuwa ni ujinga wenye kustahili tuzo au

b. Iliachwa na ulinzi - ambao naamini Polisi ndio waliupanga au Dr. Dau mwenyewe aliupanga..

Kama B. ni kweli...
 
Sipendi kweli u - sherlok holmes...

Sasa baada ya kuwachukua wale walinzi wawili kuwashikilia polisi ili nyumba

a. Iliachwa bila ulinzi - kitu ambacho kitakuwa ni ujinga wenye kustahili tuzo au

b. Iliachwa na ulinzi - ambao naamini Polisi ndio waliupanga au Dr. Dau mwenyewe aliupanga..

Kama B. ni kweli...
...ndiyo maana ile bastola ilirudishwa haste haste!
 
ama kweli ni 'animal farm' but kova na dau should know we are smarter than that, only fools can be tamed by such a joke! He who fools smarter people fools himself! Kwa hiyo kova anataka kutuambia jeshi letu la polisi limegeuka private investigation unit? Wakina jaji kapinga wameuawa mpaka leo wameshindwa kumpata muuaji, maalbino wanachinjwa kama kuku polisi haijawahi kuwakamata watuhumiwa leo dau aliyekua kigamboni mapumzikoni kaibiwa vitu ambavyo mpaka sasa havijui lakini vimerudi kwa kazi kubwa waliyofanya polisi 'what a joke' kachoka kazi huyo mr masifa si angemuachia msika aongee walau hahitaji kujikomba wala kufungamana na upande wowote


wauwaji wa kapinga walikamatwa
na walishahukumiwa kifo......

Usizungumze bila research..........
 
Back
Top Bottom