Nyumba ya Dr. Dau yavamiwa; vitu vyaibwa, vingine vyarudishwa kiana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyumba ya Dr. Dau yavamiwa; vitu vyaibwa, vingine vyarudishwa kiana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 17, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Habari ambazo nimezipata (toka kwa ka-nzi) zinadokeza kuwa Mkurugenzi wa NSSF Dr. Ramadhani Dau amevamiwa usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Kinondoni na majambazi na kuporwa vitu mbalimbali vikiwemo fedha na nyaraka mbalimbali. Tunashukuru Mungu kuwa yeye mwenyewe hakudhurika. Uchunguzi wa Polisi unaendelea...

  Habari kutoka Tanzania Daima


  Mkurugenzi NSSF avamiwa


  na Irene Mark


  [​IMG] KIASI kikubwa cha fedha ambacho idadi yake haijajulikana pamoja na nyaraka mbalimbali zimeibwa kutoka kwenye nyumba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau. Akithibitisha kutokea kwa wizi huo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Elias Kalinga, aliliambia Tanzania Daima Jumapili kwamba tukio hilo limetokea majira ya saa tisa usiku wa kuamkia jana.
  Kamanda huyo alisema nyumba iliyovunjwa ni mali ya Dau, iliyoko jirani na viwanja vya Leaders Kinondoni, ambayo hata hivyo hakuna anayeishi humo baada ya mmiliki wake kuhamia sehemu nyingine.
  “Mwenye mali yake amesema hawezi kwa haraka haraka kukumbuka ni kiasi gani cha fedha ingawa anasema kulikua na pesa nyingi pamoja na nyaraka zake mbalimbali. Hakuna mali zaidi zilizoibwa.
  “Hiyo nyumba iko jirani na viwanja vya Leaders pale Kinondoni… awali Dau alikuwa akiishi humo, lakini mpaka wizi unatokea yeye na familia yake walikuwa wanaishi kwenye nyumba nyingine,”
  alisema.
  Akielezea namna wizi huo ulivyofanyika, kamanda Kalinga, alisema ukuta mkubwa unaozunguka nyumba hiyo ulitobolewa kwa kitu kizito ambacho kilitoa sauti na kwamba wahalifu hao waliingia na kuwafunga kamba walinzi.
  Alisema jeshi la polisi linawashikilia walinzi hao ambao ni wafanyakazi wa NSSF kwa tuhuma za kuhusika kwenye tukio hilo na kuwataja kuwa ni Deus Mtatiro (52) mkazi wa Kinondoni na Yusuf Bakari (56), mkazi wa Ubungo.
  “Tunawahusisha hawa walinzi na wizi huo… ni vigumu mwizi kuvunja ukuta na kuingia ndani bila walinzi kushtuka na kutumia silaha zao mpaka wanafungwa kamba hakuna juhudi zozote za kuzuia wizi huo walizofanya.
  “…Ndiyo maana tunawahoji ili kujua kama walihusika ama laa tukimaliza tutawapeleka mahakamani lakini juhudi za kuwapata wengine zinaendelea,” alisema kamanda Kalinga.
   
 2. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kama top kama huyo anavamiwa,je mlalahoi wa Manzese afanyeje?
  Au hawa majambazi ni Mafia waliotumwa kuchukua documents za siri zinazohusika na utendaji wake wa NSSF?
  hii ni bongo yetu
   
 3. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #3
  Apr 17, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Ooh.Inakuwaje anavamiwa?hakuna security hapo kwake?Mkurugenzi wa NSSF kwa nchi yetu ilivyojaa majambazi anahitaji ulinzi wa kutosha.otherwise atuambie ni nyaraka zipi zilizoibiwa isje ikawa......
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Apr 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  walinzi wamejeruhiwa na kuumizwa..
   
 5. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #5
  Apr 17, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Yaani mpaka leo analindwa na walinzi watu?namaanisha security system ya mitambo au walinzi wa uhakika sio hawa walinzi fake wengi tulionao.
   
 6. P

  PELE JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 229
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nilidhani Bongo tambarare, kwa vingunge kama hawa kuanza kuvamiwa (kama kweli kavamiwa) na majambazi majumbani mwao labda sasa ulinzi wa Wananchi na mali zao utapewa kipaumbele cha hali ya juu.
   
 7. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,943
  Trophy Points: 280
  Option 1;

  Kama Dr Ramadhani Dau ana ufisadi ama ni fisadi;
  1)Ni kazi ya wapigania uhuru ambao wameamua kutafuta taarifa kwa njia zao kutokana na ukiritimba wa mafisadi.

  Option 2;

  Kama Dr Dau si fisadi;
  1)Inaweza ikawa ni kazi ya mafisadi kuu destroy ushaihidi wowote utakaowatia hatiani.

  Option 3
  Otherwise ni majambazi.

  However tunaanza kwa kutoa pole kwa victims.
   
 8. M

  Mutu JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wameiba na nyaraka duh.......................................
   
 9. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwamba yeye familia hawakuwepo nyumbani siku hiyo ni bahati au ni "convinience" ya namna nyingine?
   
 10. w

  wakubaha Member

  #10
  Apr 17, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hizo nyaraka sasa ziko mikononi kwa nani? Wanaozihitaji hizo nyaraka wana nia njema au mbaya? Tunaelekea uchaguzi sasa wasije mafisadi tumia mwanya huo kuliibia Taifa.
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Apr 18, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwanza natoa pole kwa mheshimiwa. Wakubwa wakiguswa labda hiyo kengele ya kuamsha walio lala itaongezwa nguvu ili walau na wengine tuambulie masalia ya ulinzi utakaoimarishwa iingawa itakuwa kwa muda tu.

  Lakini ndugu zangu naomba kuwauliza, nyaraka za kampuni zinatunzwa nyumbani kwa boss?
   
 12. A

  August JF-Expert Member

  #12
  Apr 18, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  hao watakuwa washabiki wa "simba" tena watakuwa wametumwa na mafisadi wanao isaidia simba ishinde
   
 13. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #13
  Apr 18, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Nyaraka zake personal....vyeti vyake,hati nyumba zake zote,mashamba,viwanja....silaha,vibali vyake,kadi za magari yake yote......
   
 14. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #14
  Apr 18, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Huyu kijana ni fisadi na amejipatia fedha nyingi sana toka apelekwe hapo NSSF; sio tu kuwa analiibia Taifa through overinvoicing kwenye miradi mbalimbali bali pia ni kinara wa kueneza umujahidina mahala popote pa kazi anapokuwa!! Ulizia pale NssF jinsi anavyoeneza OSAMA philosophy!! Nakungoja GT ukurupuke kwa hili!! I suspect watu waliovunja nyumbani kwake walikuwa na taarifa kuwa alikuwa amepelekewa fedha hapo nyumbani kwake na wakaamua kuchukua chao; siamini kama walifuata documents!!
   
 15. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #15
  Apr 18, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ndo maana ukienda pale makao makuu utakuta wadada na Hijab zao! kama sehemu ya uniform LOL
   
 16. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #16
  Apr 18, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  asante kiongozi kwa tafakari hii makini..uwe na wakati mwema sana weekedn hii
   
 17. t

  tk JF-Expert Member

  #17
  Apr 18, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hebu jamani acheni udini. Mwenzenu huyu kaokoka kifo. Huwezi kujua wangemkuta ndani wangemfanya nini yeye na familia yake. Hivi kivazi tu kinaonyesha imani ya mtu? Hizi hijab za NSSF ni ofisi moja tu. Jee hizo ofisi zilizojaa watu waliovaa misalaba nazo utasemaje? Haya ndio mambo ya chuki za kidini. Mtu akiipenda dini yake akiwa muislamu basi tatizo. Akiwa Mkristo ni sawa au vice versa.

  Nawaomba Polisi wachunguze kwa makini mpaka wawapate hawa watu.


   
 18. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #18
  Apr 18, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Watanzania huwa tuna tabia ya kuoneana huruma wakati wa matatizo,hata kama huyo aliyepata matatizo ni dhohari basi inabidi kwanza tumpe pole halafu ndio tuanze kumchambua kwa mambo yake.Lakini kuanza kushutumu eti ni muislamu naona huko si mahala pazuri kwani nchi hii ni yetu wote sisi wagalatia na hao wajahidina na hata wapagani.Kwenye ukweli tuuweke na tusichanganye mada kwa udini wetu ambao hautotufikisha mbali kama si kuangukia Kongo,Liberia,Nigeria n.k.
  Nawapa pole wote waliopatwa na maswaibu ya mkasa huo na bwana awape moyo wa uvumilivu wakati kipindi hiki kigumu,pia watanzania tuwe watu wa amani tusiichezee kama chizi Mtikila!
   
 19. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #19
  Apr 18, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  [SIZE=+2]Oneni fahari kuwa Waislamu-Dk. Dau[/SIZE][FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1][/SIZE][/FONT] [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1][/SIZE][/FONT]

  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]VIJANA wa Kiislamu wametakiwa kujifakhalisha na Uislamu wao ili kuweza kuwavutia hata walio nje ya Uislamu.[/SIZE][/FONT][FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1][/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Wito huo umetolewa na mgeni rasmi Dk. Ramadhani Dau katika mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Kiislamu wa kidato cha sita iliyoandaliwa na Jumuiya ya wanafunzi wa Kiislamu mkoa wa Dar es Salaam ambayo ilifanyika katika shule ya sekondari ya Tambaza siku ya Jumapili Mei 5, mwaka huu.[/SIZE][/FONT][FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1][/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Akitoa nasaha zake katika mahafali hayo, Dk. Dau alisema moja ya sababu zinazofanya Uislamu kuwa nyuma ni kuwa Waislamu wenyewe wanaona aibu kutekeleza Uislamu mbele ya wasiokuwa Waislamu.[/SIZE][/FONT][FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1][/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]"Imefikia wakati mtu anaona aibu kuwa na jina la Kiislamu au anaona aibu kutekeleza Uislamu wake. Muislamu anatoka ofisini kuelekea Msikitini lakini anaogopa kuvaa kofia yake barabarani. Ataivaa Msikitini na akimaliza anaivua kabla ya kutoka", alisema Dk. Dau kwa masikitiko.[/SIZE][/FONT][FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1][/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Dk. Dau alitoa mfano wa Mayahudi na kusema kuwa ingawa Mayahudi ni wachache hapa duniani lakini wao ndio wanaotawala dunia nzima.[/SIZE][/FONT][FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1][/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]"Idadi ya Mayahudi haizidi milioni tatu duniani hivi sasa, lakini wao ndio waamuzi wa kila kitu, hata Rais wa Marekani hawezi kuchaguliwa bila ya Support yao", alisema na kutaja moja ya sababu za Mayahudi kufanikiwa kiasi hicho ni kuwa na fakhari na imani yao licha ya uchache walionao.[/SIZE][/FONT][FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1][/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Kivutio kikubwa katika mahafali hayo kilikuwa ni onyesho la video la mikanda ya Mwembechai na hotuba ya Sheikh Ponda aliyoitoa Mtambani siku ya Eid el Hajj.[/SIZE][/FONT][FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1][/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Aidha, akitoa nasaha zake katika mahafali hayo, Mhadhiri maarufu Ustadh Shaabani Omar aliwataka Waislamu hususan vijana kuwa tayari kubadili tabia zao kuelekea katika tabia halisi za Kiislamu ili kupata radhi za Allah (s.w.).[/SIZE][/FONT][FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1][/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Katika risala yao, wanafunzi wa kidato cha sita walimueleza mgeni rasmi kuwa miongoni mwa matatizo yanyowakabili ni ukosefu wa nafasi za masomo ya juu kutokana na uhaba wa vyuo hapa nchini na dhuluma iliyopo dhidi ya Waislamu.[/SIZE][/FONT][FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1][/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Walimuomba mgeni rasmi kuangalia uwezekano wa kuwatafutia nafasi za masomo nje ya nchi ili kuweza kuutumikia Uislamu hapo baadaye.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1][/SIZE][/FONT]
  [​IMG][FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1] [​IMG][/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Bonyeza hapa[/SIZE][/FONT][FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji[/SIZE][/FONT]
   
 20. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #20
  Apr 18, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyu Bwana sio siri ana agenda ya Uislamu.
  Nimecheck hayo ni matamshi aliyoyatoa ,na nimenukuu kutoka source hii:www.igs.net/~kassim/an-nuur2/201/201-12.htm


   
Loading...