Nyumba ya Ahmed Adam aliyofikia Baba wa Taifa wakati wa kupigania Uhuru inakarabatiwa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,881
30,226
NYUMBA YA AHMED ADAM ALIYOFIKIA MWALIMU NYERERE MIKINDANI INAKARABATIWA

Mwaka ulikuwa ni 1955 na katika mkutano mkuu wa kwanza wa TANU ulifanyika Ukumbi wa Hindu Mandal Dar es Salaam Lindi iliwakilishwa na Salum Mpunga na Ali Ibahim Mnjawale.

Baada ya mkutano wawili hawa walibakia kwa ajili ya mazungumzo na Mwalimu Nyerere na viongozi wakuu wa TANU agenda ikiwa upinzani uliokuwa unatoka kwa wamishionari wakiwatisha waumini wao wasiunge mkono TANU kwa sababu ilikuwa inataka kuleta vita vingine vya Maji Maji.

Makao Makuu ya TANU New Street iliamua kumpeleka Mwalimu Nyerere, Ali Mwinyi Tambwe na Rajab Diwani Southern Province kumaliza tatizo hili.

Mwalimu alikwenda Lindi kisha kutoka Lindi akaelekea Mikindani na mwenyeji wake hapo Mikindani alikuwa Msham Awadh mmuza uzuri maarufu.

Hapo Mikindani nyumba ambayo ilionekana ina hadhi ya kufikia President wa TANU ilikuwa nyumba ya Ahmed Adam, jengo la gorofa moja.

Hii nyumba ilisahauliwa kwa miaka mingi ikawa mithili ya gofu na kama historia ya TANU yenyewe hakuna aliyeijali wala kutambua umuhimu wake.

Siku moja mjukuu wa Ahmed Adam na yeye kachukua jina la babu yake, Ahmed aliniandikia na kunionyesha picha kadhaa za nyumba ya babu yake na mimi nikaziweka katika mitandao.

Katika kuifufua historia ya TANU na wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika, nyumba hii hivi sasa inafanyiwa ukarabati kwa kumbukumbu hii ya kuwa Baba wa Taifa alipata kulala nyumba hii wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mtuchaka Ally amenirushia picha ya nyumba hii ikiwa katika matengenezo.
Namshukuru Mtuchaka kwa hisani hii.

Picha ya mwisho nyumba ilivyokuwa kabla ya matengenezo.

Screenshot_20220304-195853_Facebook.jpg
 
Safi

Ama kwa hakika Msham Awadh aliupiga mwingi
 
Back
Top Bottom