Nyumba tatu zinampatia kodi ya 3,500,000/=

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,272
Jamaa alipata kiwanja Mbezi Beach siku nyingi sana. Kazini alikua anafanya kazi kwenye mradi wa Danish, alikutana na mke wake hapo. Walienda kuishi wote Denmark baada ya mkataba wa mke wake kuisha.

Kule jamaa alijifunza kazi za kulea wazee. Alianza kujenga nyumba yake ya Mbezi Beach kwa ramani ya Denmark. Alileta basic furniture kama fridge, jiko na washing machine.

Ile nyumba ilichukuliwa na kampuni kwa 1.5m kwa mwezi. Aliweza kununua viwanja vingine viwili Mbezi Jogoo na kujenga nyumba mbili nyingine. Amepata kampuni imechukua zote mbili kwa 1m kwa mwezi.

Biashara ya Real Estate inategemea eneo nyumba ilipo na ubora wa nyumba.
 
Watanzania elimu ya fedha inatupiga chenga. Hizo nyumba alijenga kwa Tsh ngapi? Na anazihudumia kiasi gani?
Hakunieleza gharama za ujenzi ila katika maongezi alinieleza kuwa, alifanya kazi na kuweka. Akifikisha m 20 ana chukua likizo bila malipo miezi miwili anarudi bongo kusimamia ujenzi.
 
Kampuni zote zinampipa milioni 42 kwa mwaka na anazitumia kuongeza nyumba nyingine. Anasema portfolio yake ikifika nyumba 20 anaachana na ujenzi.
Ndio umejibu nini

Hizo ni pesa anazopata ofisini...tuoneshe faida anayopata kwenye nyumba ndio mada
 
Biashara za kwenye makaratasi hizo. Hadi kuwa na nyumba ambayo ofisi ama ngo wanakuja kupanga lazima iwe potential area. Hayo maeneo uliyotaja kwa muda mrefu yapo juu bei yake lets say alinunua potential plot kwa milioni 100 enzi za kikwete. Nyumba ije icost millioni 150 hadi 200 inategemea ni aina gani ya nyumba. Na kwa kodi ya milioni 1.5 haiwezi kuwa nyumba ya kawaida finishing ni ya uhakika.

Bado hajaweka cost za kusimamia na kusafiri. Then ukija kusema kajenga zingine mbili na client ni makampuni nazidi pata mashaka kwamba nawe unatunga stori.

Na by the way reak estate inahitaji mtaji mkubwa sana na return yake ni ndogo sana. Kitu utakayofaidika nayo overtime ni valuation.
 
Nimekuwekea hapo chini link za bei za nyumba zinazopangishwa mbezi beach. Kuna ghorofa ambapo apartment ni laki 2 na nusu, na mpaka luxury apartment ya milioni moja.
Sasa hapo useme hiyo nyumba ni nzuri zaidi ya hizo na kama ni hivyo basi mill 500 hadi bill zimemtoka.





 
Hakunieleza gharama za ujenzi ila katika maongezi alinieleza kuwa, alifanya kazi na kuweka. Akifikisha m 20 ana chukua likizo bila malipo miezi miwili anarudi bongo kusimamia ujenzi.
ah ah unaweza kuta amefanya kazi miaka 30 mda huu anazeeka anajisifu kupata kodi ya mi 3 kwa mwezi..... anajisifia kua baba mwe nyumba
 
Back
Top Bottom