Nyumba nzuri inapangishwa Tegeta- nyaishozi

Reasoning

Member
Mar 7, 2009
57
15
Nyumba inapangishwa iko Tegeta -Nyaishozi- karibu mita 500 tu kutoka barabara ya lami -bagamoyo road (upande wa beach). Ina vyumba viwili vya kulala-mojawapo ni selfcontained, ina sebule, dining, jiko na choo/bafu la public. Nyumba iko ndani ya fence ya ukuta wa matofali na ina geti imara. Pia ina umeme wa luku na maji ya uhakika. Ndani ya fence kuna sehemu kubwa ya wazi inayoweza kulaza magari zaidi ya 8. Pia ina banda dogo pembeni inayoweza kutumika kama jiko la nje. Nyumba yote ina ceiling board ya gypsum. Nyumba iko kwenye plot iliyopimwa na ina Hati.
Malipo kwa mwezi ni 150,000 na yanalipwa kwa mkupuo wa mwaka. Mawasiliano ni kupitia namba 0713 315808
 
Weka picha mkuu watu tuone nyumba ilivyo na madhari yake. Hiyo ndo biashara rafiki yangu.
 
picha zinaweza kudanganya macho, mkitaja si muende kuiangalia! ameshatoa maelekezo ilipo
 
picha zinaweza kudanganya macho, mkitaja si muende kuiangalia! ameshatoa maelekezo ilipo

Samahani MN, picha tu inatosha mtu kujua anakutana na nini, ndipo atakwenda wengine view ya nyumba tu inaweza mfanya asiende au aende sio maelezo. Tembelea Belleview, mybeach websites uone wanavyozitangaza hadi site zina picha, hata bila hati mtu unaipenda utaitafutia. Kama ni biashara kweli iboreshwe.
 
Mfahamisheni namna ya kuweka picha hapa ,labda haelewei,natumai pingine picha anazo kwenye hadi diski ila kuziweka Jamii forums ndio kindende :D
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom