Nyumba ndogo inaharibu familia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyumba ndogo inaharibu familia

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by carmel, Oct 30, 2009.

 1. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kuna mama mmoja, ni mtu mzima ana watoto wakubwa tu, jana kaniambia mambo ambayo hata kumshauri siwezi. Mumewe anapenda kwenda casino na mama wa watu kampa ruksa siku hizo zote, so akawa anarudi saa saba au nane.

  And she was ok with it, naona aliamua kumpa space, sasa siku hizi ana miezi kama miwili halali home kabisa akija atakuja asubuhi, akiulizwa hajali. Mama wa watu kafuatilia amemfuma dada mmoja ofisini kwake mara mbili na namba zake za simu kazikuta kwenye simu ya mumewe mara kadhaa.

  Jamaa ni member gymkana, anaendaga na mkewe so mkewe anajulikana pale, mbaya zaidi na huyu nyumba ndogo nae anapelekwa pale. Imetokea siku kijana wao kamaliza form four akiwa na baba yake na nyumba ndogo ikaitwa wakala dinner lakini dogo akaambiwa ni secretary wake while hana secretary ofisini maana ni ofisi binafsi.

  The woman is confused hajui afanye nini, ameshaenda hadi kwa padre, mambo yaleyale. Cha ajabu sasa mwanamke anajituma sana na familia yake, yaani housegirl hapiki chakula cha home, kwa sababu mumewe hapendi, yaani anafanya kila kitu mke anachotakiwa amfanyie mumewe mwenye wivu wa ajabu.

  Sasa mimi sikujua nimwambie nini maana ni mtu mzima kunishinda, ana over twenty years kwenye ndoa nikabaki tu mdomo wazi.

  Sasa wadau mnachangiaje?
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hahahaha!carmel nimecheka kwa uchungu mkuu!ngoja niirudie kusoma!

  hujambo?
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  unajua carmel,the following is the fact about marriage!
  marriage is a NO EXIT SYSTEM!once you are in YOU ARE IN!sana sana watu wa nje watashauri VUMILIA TU!
   
 4. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  mi sijambo Geof. najua inauma sana, kwa mtu kama mimi jambo la kwanza ningemuuliza what are you still doing there, but then i thougt oh, i need time to think.
   
 5. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Lakini hata biblia imeandika ndoa haivunjiki unless kwa uzinzi ama?
  Tatizo huyu kaenda mbali sana, eti mkewe akimpigia simu hata saa tisa za usiku hizo siku za kwanza kwanza,, anamjibu nimetoka casino nimeshikwa na trafic niko polisi ila usijali ntajitoa mwenyewe, dont worry at all.
   
 6. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #6
  Oct 30, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Yes it USED to be na dunia hii ya magonjwa tukishikilia hili si tutaishia kuteketezana? Unless mkubali mkishagundulika mna mapoozeo huduma ya shakula cha usiku msipewe au mpewe ndani ya ganda la pipi!
   
 7. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Kwanza Carmel naanza kwako,Ninavyokuelewa kiasi humu JF ninadhani unayo hekima ya kuweza kumshauri,udogo sio hoja unaweza kuwa kubwa jinga lakini mdogo ndio ana busara.Huyu mama mpaka kuja kwako lazima atakuwa ameona kitu cha ziada,kwani hana majirani wengine waliokuzidi umri.Wewe ni mshauri,hivyo nakuomba jiamini na utawasaidia wengi wanaokuzunguka.
  Kuhusu huyo mama ,ni kama alivosema Geoff hapo kikubwa ni kuvumilia.Cha zaidi ajichunguze zaidi anaweza kujiona yupo sahihi lakini kuna kosa analofanya ndio linamfanya mumewe akimbie.Akishajua tatizo,ajirekebishe pia atafute muda mzuri aongee na mumewe kuhusu matatizo hayo.Asitumie ukali au kufanya revenge yoyote bali azidishe mapenzi.
  Zaidi ya yooote aendelee kumwomba Mungu.
   
 8. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #8
  Oct 30, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  huyu alikuwa mshenzi haswa! Hata haya hana

  Ila kosa lilifanyika tangu mwanzo hawa viumbe hawatakiwi kupewa uhuru wa aina hiyo hawaendi pasipo kamba ya mguu hata kama ni mkali namna gani

  Angetaka kubakia na uhuru wake asingeoa in the first place!
   
 9. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  jamani wanaume muwe na heshima kwa familia zenu jamani,sasa unatoka na kijana wako mkubwa kama huyo then unamwita na hawara nae aje hapo? ni heshima kweli hiyo, Carmel mwanaume hata umfanyie nini kama wa kutoka nje atatoka tu ndio mana mie nafanyaga yaliyopo ndani ya uwezo wangu cwez kujitutuma na vitu nicvyoweza kisa kumridhisha wakati kamwe hawaridhiki hivi viumbe, 25yrs ndani ya ndoa na bado mambo ni yale yale kama ndoa ya miaka 3-4 hivi ni kwanini lakini hawa watu wanataka kutuulia ndani jamani, watoke huko watuletee na magonjwa, huyu baba anahangaikia nini sasa, na ukute huyo mdada anaetoka nae ni kama bintiye, kama Nyamayao naliambiaga lifanye lakini niclifume, magonjwa ya wazi wazi naogopa mie nije niwaache wanangu wanataabika, huyo mama apambane na hilo limwanaume lake yeye mwenyewe alikalishe chini waongee vzr, yanatia hacra sana sana ctaki kuendelea.
   
 10. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  mimi nadhani huyo jamaa alijiexpozi sana private-affairz zake!ai miin kwa mtu anayeona hawezi kuishi bila kucheat ni bora akawa msiri kidogo,au sio wapwa?
   
 11. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Thanks ZD. Ninafanya naye kazi ofisi moja hapa, hapa ofisini kila mtu anamjua jamaa yake kwa wivu, ana wivu hakuna mfano. siku moja alikuja ofisini kavimba jcho, unajua tena mdada mwenyewe white, sasa jicho lilikuwa jekundu, mie nikaropoka, vp umepigwa ngumi nini, kumbe ndo ukweli wenyewe bwana yani ilibidi nione aibu. kisa alikuwa anamsimamia rafiki yake kparty akaomba ruhusa akaruhusiwa, akapelekwa na mumewe mwenyewe, akarudi home saa nne, unaambiwa alikutana na ngumi getini mbele ya 6years old daughter wake. thats the kind of a man he is.
   
 12. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hapo penye redi umenena!nitagonga thenksi kabisa:D
  kha!
  umeongea kwa hasira sana dada yake mimi!tumekusoma!vipi kheri inapatikana?
   
 13. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  sasa hapa ndipo makosa makubwa!kupigana ngumi ni out of fasheni!lol
   
 14. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Tuko pamoja Nyamayao. Yani anasema dem ana kama 25 yrs, sme age na binti yake wa kwanza. Yani siku ingine tena dogo akiwa na baba yake akamuona nyumba ndogo anakuja, baba akamtuma nenda kaagize chakula (gymkana) akiwa anarudi akaona dingi anatoa mshiko kwa demu, kisha dem akatimua, sasa dogo akamwambia mamake, nimemuona tena secretary wa baba kaja akapewa pesa, yani mama mtu kamwambia mwanae siku ukimuona tena hapo we nipigie simu. so mama wa watu kahire detective awafatilie na kuwapiga picha nyendo zake zote. It pains as if ni mimi, i could kill them.
   
 15. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  haaa ckutegemea hiyo, kwani kama kuna kasoro soln ndio kutoka nje ya ndoa yako? kwanini acmweleze kwamba hapa ni hivi na vile waende sambamba? sio wote wanatoka nje coz kuna kasoro ndani wengine wanajickia tu kutoka ili mradi wametoka hawana maelezo.....
   
 16. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hata mimi namlaumu alipompa uhuru wa kwenda casino, hell no, my husband cant go to the casino with my acknowledgement. that was the biggest mistake, akapata uhuru wa kujua i can go home anytime that i want, how would i be sure that he is not doing it at the casino with all the temptations?
   
 17. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Dah, basi msalaba anao,Kweli viumbe wengine wazito hawabebeki.Lakini ndio tayari yupo kwenye ndoa inabidi avumilie,Na kuhusu hayo magonjwa ni balaa,inabidi atafute mbinu watengane vyumba kwanza kwa muda huku wakifanya taratibu za kwenda angaza kujua status zao japo itakuwa ngumu kidogo kwa vile anaonekana ni mwanamieleka.
   
 18. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  lakini dada zangu kiapo cha kanisani mnakikumbuka?
   
 19. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  heri inapatikana baby boy lakini kuna vimaudhi kama hivi.
   
 20. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #20
  Oct 30, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kaka tunakikumbuka sana na kinasema katika shida na raha siyo katika uzinzi na upuuzi.

  Tuwe realistic hapa angeyafanya mwanamke haya mngemwuliza huyo mumewe masuala ya kiapo cha kanisani? maana wote tunaapa the same!
   
Loading...