Nyumba kuwa na mabafu mengi kuliko vyumba ulaya

four eyes

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
905
1,406
Najiulizaga Bila kupata majibu kuhusu huu utamaduni wa majumba ya matajiri huko magharibi kuwa na mabafu mengi kuliko vyumba vya kulala.

Unakuta jumba la pesa nyingi Lina vyumba viwili mpaka vitatu vya kulala lakini mabafu ishirini na moja.na hii ni kwenye majumba mengi ya kitajiri lazima mabafu yanakuwa mara mbili ya vyumba vya kulala tofauti na afrika ambako vyumba vya kulala vinazidi idadi ya mabafu.

Kwa wanaofahamu sababu ya utamaduni huu wa wazungu atupe faida na sisi tusiojua
 
Itakuwa wanalala wanne wanne chumba kimoja hao sasa inapofika asubuhi muda wa kuwahi kazini ndo hapo wanapojiachia kwenye hayo mabafu, tofauti na huku kwetu watoto wakike chumba chao na kaka zao chumba chao na asubuhi kwa sababu hatuna sehemu za msingi sana kwenda km kazini basi hutulazimu kupiga PASPORT size tu na mswaki basi maisha yanaenda kuoga mpaka usiku
 
Wafanyakazi wengi na uwingi wa wana familia muda mwingi kwenye nyumba zao hivyo huweka bathroom nyingi for privacy.
 
Najiulizaga Bila kupata majibu kuhusu huu utamaduni wa majumba ya matajiri huko magharibi kuwa na mabafu mengi kuliko vyumba vya kulala.

Unakuta jumba la pesa nyingi Lina vyumba viwili mpaka vitatu vya kulala lakini mabafu ishirini na moja.na hii ni kwenye majumba mengi ya kitajiri lazima mabafu yanakuwa mara mbili ya vyumba vya kulala tofauti na afrika ambako vyumba vya kulala vinazidi idadi ya mabafu.

Kwa wanaofahamu sababu ya utamaduni huu wa wazungu atupe faida na sisi tusiojua

Matajiri wazungu hawapendi kushirikiana bafu na mtu mwingine.Mfano bedroom kunakuwa na bafu mbili,Moja ya mama na vikorokoro vyake vya kujipoodolea ya pili inakuwa ya mzee .Hakuna kusubiriana foleni wakati wa kuoga wala kuoga pamoja kama uswahilini kwa wapenzi koko wanavyotapeliana .

Kila chumba kinakuwa na bafu mbili ya mwenye chumba na mgeni.Ukiwa mfano na chumba cha mtoto nacho kinakuwa na bafu mbili.moja ya mtoto mwenyewe ingine ya mgeni wa mwanao.

Kwa hiyo nyumba ya kawaida self contained yenye vyumba vinne itakuwa na bafu nane jumla.
 
Mkuu uko sahihi, yani utakuta ukifatilia nyumba za mastaa, utaskia vyumba vya kulala viwili lakini Mabafuu 15 , yani nahsi ni utadunii

√kwa wa africa hayo mabafu yanageuzwa vyumba na vyumba vinageuzwa bafu na choo
 
Nyumba kuwa na vyoo vingi kwanza huongeza thamani ya nyumba kama unalenga kuiuza kwa matajiri au kujenga (tajiri)
Inategemea na ukubwa wa square feet.

Kwani utakuta mtu ana swimming pool lazima bathroom iwe karibu ili asiharibu ndani, Jikoni pia unakuta toilet mpaka dinning room utakuta choo.
Master ina bathroom na toilet yaani full vyoo
 
Back
Top Bottom