Nyumba kupigwa mnada baada ya kuchelewa kulipa

Morning_star

JF-Expert Member
Apr 21, 2018
4,159
11,466
Jamaa yangu alichukua mkopo benki kwa kuweka nyumba yake kama dhamana. Sasa kashindwa kupeleka marejesho miezi miwili. Leo kampuni ya udalali imekuja na kumpa barua ya kwamba benki hiyo imempa mamlaka ya kuiuza na kumpa notice ya siku 14.
Mkopaji anasema hajashindwa kupeleka marejesho alipatwa na dharula na kwamba wampe muda ataendelea kupeleka marejesho. Sasa wajuzi au wazoefu wa sheria inasemaje na inampa muda gani kabla ya kupiga mnada hiyo dhamana? BoT amabyo ina regulate ( inarekebisha) sheria kandamizi za mabenki inampa mkopaji muda gani kabla ya dhamana kupigwa mnada? Inavyoonekana jamaa wanataka kumnyanganya nyumba bila ya kupewa muda ( grace period)
 
Kazi ya benki sio kuuza mali za wateja pale inapoonekana mteja amechelewa kulipa huanza kumfatilia kwa karibu mpaka wajiridhishe kuwa kweli hawezi kulipa mkopo na kuchukua hatua za kuuza dhamana zake nafikiri kuna kitu hakipo wazi
 
Ukichukua mkopo na ukaweka dhamana ya nyumba hakuna dharula yoyote zaidi ya nyumba
 
Huu Uzi haujakamilika.

Huenda mtoa mada kuna kitu anaficha au umefichwa uhalisia na mhusika
 
Jamaa yangu alichukua mkopo benki kwa kuweka nyumba yake kama dhamana. Sasa kashindwa kupeleka marejesho miezi miwili. Leo kampuni ya udalali imekuja na kumpa barua ya kwamba benki hiyo imempa mamlaka ya kuiuza na kumpa notice ya siku 14.
Mkopaji anasema hajashindwa kupeleka marejesho alipatwa na dharula na kwamba wampe muda ataendelea kupeleka marejesho. Sasa wajuzi au wazoefu wa sheria inasemaje na inampa muda gani kabla ya kupiga mnada hiyo dhamana? BoT amabyo ina regulate ( inarekebisha) sheria kandamizi za mabenki inampa mkopaji muda gani kabla ya dhamana kupigwa mnada? Inavyoonekana jamaa wanataka kumnyanganya nyumba bila ya kupewa muda ( grace period)

Dharura miezi 2 mfululizo usilipe? Aache usanii.
 
Sheria inasemaje ni muda gani miezi au mwaka wa kumpa mteja ndo dhamana ipigwe mnada? ndo anataka kujua kwasababu inaonekana dalali yuko fasta kuliko maelezo! Wajuzi au wazoefu wa mortgage collateral law msaada please!
 
Nyumba yake kupigwa mnada sio tatizo kama kweli kashindwa kulipa! Lakini miezi 2 tu? Kwa baadhi ya kumbukumbu nilizowahi kuona kupiga nyumba mnada ni kwa MDAIWA SUGU. Ikiwa na maana huyo jamaa kapitisha miezi kibao! Nakumbuka wengine hadi mwaka
 
Hakuna benki inayouza nyumba kwa mkopaji kuchelewa kulipa marejesho kwa miezi 2 tu. Kuna kitu huyo mdaiwa hajakwambia.
 
Kazi ya benki sio kuuza mali za wateja pale inapoonekana mteja amechelewa kulipa huanza kumfatilia kwa karibu mpaka wajiridhishe kuwa kweli hawezi kulipa mkopo na kuchukua hatua za kuuza dhamana zake nafikiri kuna kitu hakipo wazi
Upo sahihi mkuu.
 
Siku 14 ni chache sana kumpigia mtu mnada, sheria za nchi gani zina ujinga huu?

Siku 14 kwa mtu anatelipwa mara mbili kwa mwezi, anayetegemea mshahara kulipa deni, kukitokea hitilafu kidogo tu wamwambie "mshahara wako tunao ila utalipwa pay period ijayo" ambayo ni siku 14, maana yake hapo tayari mtu nyumba inapigwa mnada.

Siku 14 maana yake mtu akienda likizo Bahamas akakutwa na kimbunga huko akashindwa kurudi nyumbani on time kwa wiki mbili, anakuta nyumba yake imepigwa kimbunga.

Huu mchakato unatakiwa kumpa mtu angalau siku 90 kuona kweli hawezi kulipa au ni mambo ya dharula ya muda mfupi tu.
 
Back
Top Bottom