nyumba kubwa anaposalimu amri kwa nyumba ndogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

nyumba kubwa anaposalimu amri kwa nyumba ndogo

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Kongosho, Jan 28, 2012.

 1. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  pedeshe mmoja akiwa na mkewe walikwenda muziki, binti mzuri alipita na kumsalimu pedeshe. Kuona hivyo mama akapata shaka, basi yakaanza mahojiano

  Mama: Yule nani?
  Pedeshe: Huyo ni nyumba ndogo yangu
  Mama: nataka talaka yangu
  Pedeshe: Pouwa nitakupa, lakini kumbuka safari za uchina na dubai ndio zitakuwa basi tena na ishu za kwenda saluni mara mbili kwa wiki utazikosa. Sijui utakuwa unatumia gari gani maana sitakuachia hata moja.

  Mara kimya.

  Basi mara akapita binti mwingine.
  Ikaanza awzmu nyingine ya mazungumzo.

  Pedeshe: Mama watoto huyo aliyepita punde ni nyumba ndogo ya rafiki yangu.

  Mama: Mmmmh, huyu siyo mzuri kama kama ile nyumba ndogo YETU.

  Kazi kweli kweli, :)
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hahahahahaaha. . . .
  Kweli utegemezi TABU.
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Kweli utegemezi gunia la misumari

   
 4. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Siku akiletewa magonjwa ndiyo atajua utegemezi haufai.
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hata ugonjwa ukivamia bado hakutakua na kujua maana hata pesa za matibabu atatakiwa ategemee.
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Plus balanced diet.

   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Jan 28, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Hakuwezeshwa tu huyo mama. majibu yangekuwa mengine kabisa.
  Safari za uchina na dubai angeenda mwenyewe.
  Kama kuna mwanaume anatabia ya namna hiyo ambayo inaweza kusababisha presha au hata kifo kwa mwenzie basi hafai kuwa mwanaume, na alaaniwe.
  watu tunafanya mambo lakini kwa siri bila mpenzi kujua.
   
 8. Ziltan

  Ziltan JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Asilimia kubwa ya nyumba kubwa ni za kawaida ,why?
  Ndio kusema unapokuwa kijana totoz kali zinawashinda au hawajui kuchagua?
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Umri umeenda, majukumu ya kifamilia.

  Kumbuka Ocol alivyokuwa anamsifu Lawino wakati anaenda kumchumbia, baada ya kumpata Clementina, kila kitu kikabadilika.

   
 10. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,046
  Likes Received: 6,492
  Trophy Points: 280
  Mwacheni akome amezoea vya kupewa ipo siku atapewa vyote.
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Jan 29, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  hata hivyo Lawino alikuwa amezidi ushamba bana.
   
 12. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Umri ukienda kwani nyumba kubwa umri wake una-stop!? Dawa yake unahakikisha uko kwenye order wakati wote, eboo! Mbona atakaa mguu sawa yeye mwenyewe kama mgambo wa jiji!
  Kuzaliwa maskini sio dhambi, dhambi ni kufa maskini! Source: prof flani hivi bazazi bazazi
   
 13. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #13
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Pamoja na ushamba, kwani Ocol hakumuona wakati anamchagua?!
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  Jan 29, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  maisha yanabadilika na mazingira pia yanabadilika. Lawino was supposed to change according to the situation, rather than maintaing traditional culture in the wake of modern cultures.
   
 15. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Ofcoz nakubaliana na wewe somehow. Swali: mkeo akikuambia anataka uwe na kg 50 wakati ulimuoa ukiwa na kg 100 utaonaje? Ama akikuambia uvae kata k na zile viatu za plastic za pink utajionaje?
  My take: kuna vitu ambavyo vinaku-define wewe kama wewe na hauko tayari kuviachia hata kwa ajili ya mwenza wako. So long papaa!
   
 16. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #16
  Jan 29, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  he he eh hapo kasalimu amri mwenyewe
   
 17. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #17
  Jan 29, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,218
  Trophy Points: 280
  chezea pesa!
   
 18. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #18
  Jan 29, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,114
  Trophy Points: 280
  watu wanapenda pesa kuliko kumpenda Mungu.
   
 19. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #19
  Jan 29, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mfano Mumeo anakuambia tuweke umeme kwenye nyumba tuachane na koroboi na yeye anakataa anakuambia hayo ni mambo ya kizungu utajionaje? Mumeo anakuambia mama nimekununulia khanga ujisitiri, mama anakataa anakuambia nimezoea kuficha makalio tu, khanga ni mambo ya kizungu utajionaje? Mumeo anakuambia tununue gari mambo ya kusafiri na punda imepitwa na wakati, yeye anakataa anakuambia punda ndiyo utamaduni wetu, gari ni utamaduni wa kizungu utajionaje mbele za jamii ya mabadiliko? Lazima tubadilike kulingana na mazingira, japo baadhi ya tamaduni zetu zenye maadili lazima tuhifadhi.
   
Loading...