Nyumba inapangishwa Kiseke, mwanza

Makiyuve

Member
Sep 7, 2010
56
0
Jamani kuna nyumba inayopangishwa Kiseke Mwanza, ni nyumba ya PPF, ila imeongezwa zaidi, imepigwa plasta na rangi nzuri, ina vyumba vitatu masterbedroom na vingine viwili, ina gate na fence, ina garden, ina maji na umeme. Gharama yake ni sh. millioni 3 kwa mwaka
 
Kweli zile nyumba ni za ukweli ila maajabu ni kwamba sehemu ile hakuna soko, hakuna hospitali, hakuna maduka ya vyakula ya kutosha kiasi kwamba unapohitaji mahitaji yako lazima uende kule kiseke A, pia hakuna kituo cha usalama kama kituo cha polisi. hayo yote yana sababisha kutokuweza kuishi maeneo hayo. Lakini sio mbaya, nyumba ni nzuri sasa sijui hiyo yako iko maeneo gani?? Na juzi kumetokea tukio la kutisha baada ya vijana wasiojulikana kumvamia mzee mmoja aliyekuwa anaishi peke yake na kumkata na panga na kumchoma visu na kufa hapo hapo bila kuchukua kitu chochote mle ndani. inasemekana mzee hakuwa mlevi, na alikuwa mlokole so kunani??? tuwaachie polisi ndo wanafahamu hayo.

Huduma za polisi ni lazima urudi hadi pasiansi(8KM) ambapo kituo kinafungwa saa 12 jioni (Sina uhakika siku hizi) na kingine hadi AIRPORT ya mwanza(12KM). Ukiwa na imejensi utawakoma polisi wa bongo kufika hadi tukio likamilike ndo utawaona so unayetaka kuishi KISEKE ukubaliane na hayo.

Je unamshawishi vipi yule anayetaka kupanga kwenye hiyo nyumba yako, mwambie ukweli kuwa haku huduma zifuatazo:

  • Hospitali
  • Polisi
  • soko
  • duka la madawa (Nimeona juzi linaandikwa so soon will be)
Pia nyumba nyingi hazina watu na hakuna mtu wa kufanya usafi hivyo sehemu kubwa ya maeneo yale ni misitu ya kutisha na nyika yaani majani marefu mita 2.5 na kuendelea.

Wajuze watu mazingira kwanza kisha wape muda wafikirie.

Kiseke ni pazuri sana, ila kasoro ndio hizo hapo juu.

Wako Omuntunamuntu
 
Dear Omuntunamuntu

As per all the concerns you have raised most of them are realities but you have exagerrated some especially issue ya majirani. Nyumba imezungukwa na watu kote. Actually it has been so long na mtu alishahamia since December last year, but I am still thanking you atleast after almost six months you still remember and advise.

Aliyeuawa PPF inasemekana alikuwa na visa na hao walomuua coz hawakuiba kabsaaaaaaaaaa si rahisi sana na haya mambo hutokea kokote haijalishi unaishi Bwiru au Capripoint hata mabatini yapo.

Have a lovely day
 
Back
Top Bottom