Nyumba Imara ni ile yenye msingi imara; Je, Nyerere hakuweza kujenga msingi Imara wa viongozi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyumba Imara ni ile yenye msingi imara; Je, Nyerere hakuweza kujenga msingi Imara wa viongozi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nzi, Nov 7, 2011.

 1. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,867
  Likes Received: 4,545
  Trophy Points: 280
  Salaam wanaJF!

  Inafahamika kwamba, ili nyumba iwe imara na itakayodumu kwa muda mrefu ni lazima msingi wake uwe imara pia. Inamaanisha kwamba, msingi ukiwa mbovu basi nyumba hiyo haitodumu kamwe! Hii ni simple architecture and engineering.

  Tukija kwenye suala la siasa yetu kuanzia enzi za Tanganyika mpaka Tanzania, suala la uongozi na maadili limekuwa likitiliwa mkazo; kiasi hadi Mwalimu Nyerere alifikia kusema kwamba uongozi bora ni jambo la msingi kwa maendeleo ya nchi. Tunaelewa pia jinsi Mwalimu alivyokuwa mstari wa mbele kuwakemea na kuwanyoosha wale viongozi waliokua wakiacha maadili ya uongozi bora. Viongozi wa umma enzi zake wakaonekana wana maadili sana!! (sijui kama kweli walikua na maadili au walimwogopa Mwalimu)

  Enzi za Mwalimu zikipita; akaja Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete. Tangu alipoachia ngazi Mwalimu, suala la viongozi bora na safi likaanza kutoweka taratibu; na sasa lipo katika critical - ready to explode stage. Viongozi hawaitwi viongozi tena, bali wanaitwa watawala; na sasa wanasisitiza juu ya utawala bora!! Kwa sasa hawa "viongozi" si ajabu kumiliki mali ambazo kimsingi wasingeweza kuzimiliki hata kama wangefanya kazi miaka 60!

  Sasa maswali ya kujiuliza hapa; je, Mwalimu hakuweka msingi mzuri wa viongozi wajao baada yake?! Kama hapana, je Mwalimu hakua ni fundi mzuri wa kuandaa mafundi watakaomalizia ujenzi wa nyumba ya Tanzania? Kama Mwalimu aliweka misingi mizuri ya uongozi, je, hao mafundi wanafunzi walielewa somo?! Kama hawakuelewa, je, Mwalimu hakua na mbinu na weledi wa kutoa somo vizuri?!

  Kuna shule ya mawazo inayosema kwamba hakuna mtoto anaezaliwa mtukutu, mwizi au mzinzi. Mtoto akizaliwa, ubongo wake unakua na zero memory (ni ruhusa kukosolewa hapa); hivyo haya mambo ya kidunia atajifunza na kuyaiga kutoka kwa watu wanaomzunguka (wazazi, ndugu, jamaa na marafiki). Na kwavile wazazi ndio watu waliomleta duniani, wao ndio wanaopaswa kumfunza yale yalio mema. Mtoto akitokea akawa mtukutu, mzinzi au kibaka, basi wakulaumiwa ni wazazi (hapa wazazi hawawezi kukwepa hili). Kuna watu wanatabia ya kushangaa kwamba; yule mtoto mbona ni mwizi wakati wazazi wake ni watu wazuri sana?! Ikiwa hivyo basi ni wazi kwamba hao wazazi hawakuweza kumfunza vyema huyo mtoto.

  Sasa kwa upande wa Mwalimu; hawa viongozi wakuu wa taifa hili, karibu wote wametokea katika mikono yake (wengi wao wamefunzwa masuala ya uongozi wakati wake). Sasa wanapokua wanatenda mambo yasiyo mazuri kwa taifa hili, uwa najiuliza sana, mbona Mwalimu alikua mtu mwema (si fisadi, hakujilimbikizia mali n.k.), je, hawa watoto wake wamejifunzia huu uhuni wapi? Je, Mwalimu hakuwafunda vyema?!

  Maswali ni mengi. WanaJF, naomba majibu na msaada juu ya hili suala!

  Asanteni!

   
 2. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Upupu tu, ptuuuuuuu!
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hapana mkuu wangu Nyerere aliacha msingi mzuri tu kulingana na wakati wake. Ni kama mzee aliyejenga nyumba ya vyumba sita Kariakoo kwa ajili ya familia yakemwaka 1960, na alipokufa nyie mlorithi mkaiona nyumba haifai kulingana na masiha yenu, mkauza jengo kwa wageni walioahidi kujenga ghorofa.. jambo kubwa ambalo hamkulitazama ni kwamba ghorofa lilihitaji ramani mpya sii tu ya jengo bali toka msingi, mifereji ya maji, mabomba, nguvu ya umeme na kadhalika..Uchu wa kuuza kwa mallioni ndio ulowaponza na sii nyumba ya vyumba sita kuwa sababu thamani yake ilipanda na haikushuka.

  Sasa ghorofa limesimama lakini matatizo ndio kibao mnaanza kumlaumu Nyerere, ili hali maamuzi mmeyafanya wenyewe ktk ujenzi mpya. Sasa maadam mmezoea maisha ya dhiki na hayo maendeleo ya Kariakoo mnayaona kama mko Ulaya kutokana na kuwepo maghorofa mengi na biashara za uchuuzi ulitegemea nini zaidi?
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Ni wazazi wangapi ambao watoto wao wote wamekuwa vile walivyowalea!? Wakati mwingine ni rahisi kweli kumlaumu mzazi lakini hujui jinsi gani mzazi alijitahidi kulea.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  It does not matter how strong msingi wa nyumba ulivyo kama hukufanya ukarabati utajikuta umebakiwa na gofu! ulishasikia magofu ya Kilwa na hata huko Zanzibar?
   
 6. m

  mharakati JF-Expert Member

  #6
  Nov 7, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Nyerere alitegemea itikadi zaidi ili imsaidie katika kupata viongozi wa kumsaidia na kuwalea hawa wa leo, lakini kama itikadi ikifa unajua na yale maadili yanazikwa moja kwa moja na hiki ndiyo kilichotokea hapa nchini na uongozi wetu.

  Baada ya itikadi ya ujamaa kufa na kuzikwa uliberali ukatawala na Nyerere hakua na nguvu yake ya zamani tena zaidi ya kukemea wale wachache aliowaona hawafai kwa uongozi huku akiwa hana nguvu ya kuzuia itikadi hii ya kiliberali na maadili yake hasi ya uongozi kwa nchi masikini kama yetu.tukumbuke viongozi walafi walikuepo toka enzi zake sema tu walimugopa Mwalimu na walibanwa na maadili ya itikadi ya kijamaa mfano yale ya kutofanya biashara ukiwa kiongozi wa umma.

  Mi nafikiri mwalimu kabla ya kung'atuka angeweka katiba mpya ya kuwabana hawa watu aliowaacha kwa sababu alijua itikadi yake imekufa na maadili yale hayapo tena
   
 7. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #7
  Nov 7, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Mwalimu alikua na udhaifu mkubwa katika uteuzi wa viongozi. Alitumia zaidi hisia zake binafsi na sio sifa zilozowazi katika uteuzi. Alijizungusha na vilaza wasio mpa changamoto ila wanaujua kusema ndio kwa kila kitu. There must be a clear criteria for ascendence to leadership position not huu ujinga wa " fikra sahihi" za mtu mwenyecheo cha mwenyekiti. Udhaifu huo katika uteuzi umeendelea hadi Leo.
   
 8. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #8
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,867
  Likes Received: 4,545
  Trophy Points: 280
  Nyeusi: hili ni tatizo mkuu! Huo msingi aliouacha ulilingana na wakati wake; msingi huo ulivyoeleza, haukuweza kujengwa katika misingi ya kuweza kwenda na wakati huu wa sasa!! Ndio maana nimesema, Mwalimu alikua amezungukwa na viongozi walioonekana wana maadili mazuri sana kwenye macho ya Mwalimu. Wengi wao ndio walikuja kuwa mabazazi waliopo sasa!

  Bluu na nyekundu: hizo ni dalili kwamba hao watoto walikua hawajajengwa katika misingi iliyo bora na imara ya kimaadili na kimaisha. Kwanini waone nyumba waliojengewa na baba yao haiwafai? Huo uchu wa kuiuza hiyo nyumba mbona hawakuwa nayo wakati baba yao yupo?! Mkuu hapo hauoni kuna walakini?!?
   
 9. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #9
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,867
  Likes Received: 4,545
  Trophy Points: 280
  Suala la wazazi wangapi na watoto kukua walivyolelewa, mkuu hili halina mjadala!! Mtoto ambae anakua kinyume na vile alivyolelewa ni mapungufu kwa mzazi; hapa mzazi hawezi kukwepa hili suala.

  Mkuu mzazi hatakiwi kujitahidi katika kulea mtoto; anatakiwa kulea mtoto katika kiwango cha juu cha ubora. Huyo anaejitahidi, ana kasoro mkuu! Watoto umewazaa wewe, halafu kuwalea uanze kujitahidi!!! Am I missing something mkuu!?
   
 10. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #10
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,867
  Likes Received: 4,545
  Trophy Points: 280
  Mkuu gofu na msingi?!? Gofu linaweza kuwa limesimama kwenye msingi ulio imara; nyumba kuitwa gofu hakumaanishi nyumba hiyo ina msingi mbovu. Na ukarabati wa gofu unaweza kufanyika bila hata kuathiri/kugusa msingi! See what is happening in Bagamoyo, hayo unayoyaita magofu yanakarabatiwa huku misingi yake ile ile ikiendelea kutumika.
   
 11. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #11
  Nov 8, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Wakuu hii hoja nimeipenda sana. Hii ili kuielewa mantiki yake inabidi tujikumbushe vizuri sana jinsi tulivyobadilika toka ujamaa na kujitegemea na kuingia uliberali kama alivyouita mkuu hapo huu.
  Kusema kweli ni lazima tukubali kuwa kunatokea udhaifu wa uongozi kwenye nchi wakati kiongozi mwenye lement ya udikteta na aliyekaa madarakani muda mrefu anapotoka madarakani. Mara nyingi wale waliokuwa wajanja wajanja katika kuficha tabia zao ndiyo wanachukua nchi na kuifanya kama walivyodhania wao.
  Kitendo hiki ni cha hatari maana nchi hupoteza dira ya uongozi hadi anapopatikana tena kiongozi mwenye uthubutu na anayeipenda nchi yake. Nyerere aligundua makosa aliyofanya muda mfupi baada ya kukaa Butiama, ikawa ameshachelewa. Hata alipojaribu kukemea kuwa "huko ikulu mnakimbilia kuna nini huko?" Kule siyo sokoni nk. haikusaidia sana ikawa too late! Nyerere aliwaharibu watoto wake mwenyewe. Aliwaonyesha namna ya kuongoza chama kibabe na watoto wakawa wababe kweli! Tanzania inaongozwa na ubabe wa uwt, na wakitaka kutumaliza hata sisi tunaoyatafakari mambo kwa uhuru huku JF wanatumaliza.

  Kuna aliyetoa mfano wa watoto hapo juu na nyumba ya kurithi, ninaamini mtoto au watoto walioachiwa nyumba na baba yao mahali, kama wanabusara na walifundwa sawasawa hawataibomoa hata kama ilikuwa ya mbavu za mbwa! Kinachotakiwa kama wamepata uwezo ni kujenga nyingine jirani yake iliyo bora zaidi na kuendelea kuikarabati ile mpaka kutakapokuwapo na sababu nzuri ya kubomoa iliyosimamishwa na baba yao. Viwanda waliyoua hawa viongozi wa sasa hawana uwezo wa kutujengea vingine. Ni udhaifu usiopingika.

  Katika watu walionishangaza hakuna kama Raisi Mstaafu Mkapa. Huyu alikuwa mtoto halisi wa Mwalimu, huyu alikuwa mwanafunzi wake halisi, huyu akaendelea akawa rafiki yake wa karibu sana, wakicheza hata ping pong pamoja nyumbani kwake. Iweje leo hii abadilike namna hiyo hata kujimilikisha mali za umma? Tena alizozianzisha Mwalimu? Hakika mwalimu alikuwa dhaifu katika kuwafahamu mbwa mwitu waliokuwa wamemzunguka. Na hili ndilo linaloelezea wazi udhaifu unaokuwepo katika nchi isiyokuwa na demokrasia ya kweli. Nchi inayoongozwa kwa kuabudu fikra za mtu mmoja na kwa muda mrefu. Nakumbuka sana kisa kimoja ambacho nilikishuhudia. Nyerere alikua anatembelea wilaya moja hapo nchini, yule Mkuu wa wilaya akaagiza watu walete, kama sikosei ilikuwa migomba, wakaleta mirefu, wakalima shamba kubwa likaoteshwa ile migomba, Mkuu alipofika wakampeleka kutembelea shamba siku ya pili tu baada ya kuoteshwa! Mkuu wa wilaya akajizolea sifa kem kem. Huo ni mfano mdogo tu wa upuuzi wa kuongozwa na chama kisichojali utaalam bali mradi kiwe madarakani. Ndivyo Nyerere alivyowalea viongozi tulio nao sasa hivi. Wengi wa hao viongozi tulio nao waliokuwa uwt, mambo waliyowahi kuyafanya huko nyuma wanayajua wenyewe, sasa ukiishaishi maisha ya kutishia wale unaotofautiana nao kimawazo na hata kuwamaliza kiaina, wale wale watoto uliowafundisha na kuwatuma kuwamaliza maadui zako watambakiza nani? Tena usipokaa sawa watakumaliza hata wewe mwenyewe!!! Kwa mawazo yangu huu ulikuwa udhaifu mkubwa wa Nyerere. Lakini anayo mazuri pia!
   
 12. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #12
  Nov 8, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,785
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Mwalimu alifanya makosa ya kutotuachia taasisi za kidemokrasia zilizo huru na imara. Ndiyo maana leo tunashuhudia watawala wa hovyo wanaongoza nchi hii na inakua vigumu kuwaondoa madarakani na hata kuwashitaki kwa makosa ya kuhujumu nchi.
   
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  Nov 8, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hivi ni Nyerere aliyeondoa leadership code Tanzania? Ni Nyerere aliyeruhusu wafanyibiashara kushika nafasi za juu na kuwa na kauli ya uongozi katika chama tawala? Kwa nini hatuelekezi lawama pale zinapostahiki? Lowassa alikuwa kada wa CCM. Kikwete alikuwa jeshini tena kiongozi mzuri tu wa maadili ya CCM. Sasa unataka kutuambia kuwa Nyerere ndiye aliyewageuza kuwa mafisadi waliokubuhu?
   
 14. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #14
  Nov 8, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Ni kawaida ya watu wenye akili za kawaida kutafuta sababu za wao kusindwa kufanya zaidi ya kawaida. Nyerere alijitahidi kufanya zaidi ya kawaida wakati wake tena kaitika mazingira mgumu sana ya dunia; leo hii dunia imekuwa ni nyepesi lakini sisi tunashindwa kufanya zaidi ya kawaida. Alitufundisha kuwa (a) We must run while they walk - Leo sisi tanakaa kitako wakati wenzetu wanakimbia. (b) It can be done; play your part - Leo sisi hatuamini kuwa tunaweza kufanya bila kuleta mwekezaji. Mlitaka afanye nini? hata hao akina Kikwete na Lowasa aliwaelimisha yeye bure bure akiangalia uhai wa taifa, lakini wao leo wameamua kutoeleimisha taifa tena ili kulinda ya uhai wao binafsi . Angalia nchi zinazeoendelea kwa kasi leo hii: zote zimefanikiwa kutokana na misingi kama aliyokuwa ameacha Nyerere. Tatizo letu ni kuwa tulikuwa wajinga sana kiasi kuwa misingi aliyokuwa akijenga hatukuijua na wala hatukuona thamani yake mpaka pale ilipokuwa imeshatoweka: You never know what you have until you lose it !!

  Kama baba yako alijenga nyumba ya familia pale Kariakoo mwaka 1961 halafu leo hii badala ya wewe kuimarisha msingi ule na kujenga nyumba ya kisasa ukaamua kubomoa msingi na kuuza kiwanja basi utabaki huna pa kukaa.
   
 15. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #15
  Nov 8, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Taasisi za kidemokrasia hurithishwi. Huo ni uvivu wa kufikiria. Zinajengwa na watu wenyewe. Tuna mahakama huru, mbona haikuheshimiwa ilipoamua kuwa ni ruksa kuwa na wagombea binafsi? Ulilalamika wapi? Tuna bunge. Umelitumiaje bunge lako kuhakikisha uhuru na demokrasia vinaimarishwa?
  Play your part, it can be done. Mwalimu played his part.
   
 16. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #16
  Nov 8, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Sasa huo walakini alaumiwe mzazi wako? Leo wewe ukiamua kuwa jambazi licha ya kwamba baba yako kakusomesha na kukuwezesha utasema baba yako ndio wa kulaumu? When do we take our own responsibilities?
   
 17. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #17
  Nov 8, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,867
  Likes Received: 4,545
  Trophy Points: 280
  Mkuu haya yote uliyoyasema, ni dhahiri kwamba kulikua na udhaifu wa mzazi katika malezi ya watoto.

  Hapa watu wanafikiri kumkosoa Mwalimu ni kosa; yeye ni binadamu alikua na mapungufu yake; na haya ni kati ya mapungufu yake.

   
 18. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #18
  Nov 8, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,867
  Likes Received: 4,545
  Trophy Points: 280
  Mkuu hawa uliowataja walikua developed wakati wa Mwalimu...sasa huoni kama kulikua na mapungufu katika namna ya kuwalea na kuwajenga kuja kuwa viongozi makini na waadilifu?! Kwanini waje kugeuka mafisadi wakati Mwalimu wao hakuwa fisadi?!

  Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo!!
   
 19. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #19
  Nov 8, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hatujasema kuwa kumkosoa Mwalimu ni kosa. Lakini tusimbebeshe Mwalimu lawama kwa hulka ya wizi aliyo nayo Mkapa, au hulka ya ufisadi aliyo nayo Kikwete. That is all what we are saying. Marekani founding fathers walitunga katiba ambayo tunaweza kusema ni the best in the world lakini Marekani ilikuwa na watumwa na hata baada ya utumwa Wamarekani weusi hawakuhesabiwa kama binadamu kamili. Ilichukua harakati za raia wenyewe kufanikisha kutambuliwa kwa usawa wa watu wote. Hakuna mtu aliyesema kuwa founding fathers mbona hawakuweka misingi imara ya kutokomeza ubaguzi na utumwa. Mwalimu alituwekea misingi ya usawa, Azimio la Arusha, misingi ya maadili, leadership code. Sasa ni nani aliyevifuta hivyo? Mbona sijakusikia unamlaumu lakini eti tu Mwalimu hakutuwekea misingi? Aliweka. Ndiyo, alikuwa na mapungufu yake, lakini hayo unayoyasema si katika mapungufu aliyokuwa nayo Mwalimu. Hapo tutabishana mpaka liyamba.
   
 20. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #20
  Nov 8, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,867
  Likes Received: 4,545
  Trophy Points: 280
  There you are....kawa hao walielimishwa na Mwalimu basi hawakuelimishwa vizuri!! Na Mwalimu hakujua kama hawakuelimika; hapa ndipo shida. Mwalimu/mzazi anapaswa afahamu kama mwanafunzi/mwana wake ameelewa somo; kama hajaelewa atafute mbinu nyingine za kumuelewesha.

  Mtoto wa namna hiyo mkuu hakupata malezi na mafundisho bora kutoka kwa mzazi wake. Mtoto alielelewa na kukuzwa vyema angefahamu namna ya kuimarisha hiyo nyumba au kufanya mambo ambayo yeye na kizazi chake hawawezi kupata shida kutokana na kuuza au kubomoa nyumba ya urithi.
   
Loading...