nyumba chungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

nyumba chungu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Feb 1, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MUME wa Grace amemtaka mke wake huyo ifikapo mwishoni mwa mwaka huu kama hajafanikiwa kushika mimba basi atalazimika aione nyumba chungu kwa kuwa hataweza kuvumilia kuendelea kuishi nae kama mke na mume.

  Grace alitamkiwa hayo juzi usiku wakati wakila walipokuwa wakipata chakula cha usiku wakiwa pamoja.

  Grace alidai kuwa, wakati wakiwa mezani wakiongea mawili matatu huku wakiwa wanakula chakula cha usiku, ndipo mume wake alimtamkia hivyo na kumwambia azingatie hayo kwani alikuwa hayupo kaitka mzaha.

  Grace alipomuuliza ni kwanini aliamua maamuzi hayo mumewe huyo alidai hana mjadala juu ya hilo kwani alishamueleza.

  Hata hivyo Grace alimtaka mume wake huyo waende kituo cha afya wakaangalie huenda mmoja wao alikuwa na matatizo lakini mume wake alimjibu yeye ana uhakika hana matatizo anayoyafikiria wka asilimia zote na atamthibitishia hilo.

  Alisema mwishoni mwa juma hili ataenda kuripoti tukio hilo kwa wazazi wake .
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  hii ni tamthilia au ni habari kutoka kwenye gazeti la uwazi......
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Kuna jirani yangu nae alimfukuza mke wake kisa eti hashiki ujauzito, wameishi miaka mitano bila kitu. Yule mke akachukuliwa na jirani yake nyumba ya pili, baada ya miezi miwili mke akashika mimba, jamaa hivi sasa kwa aibu hashindi nyumbani, anatoka alfajiri sana na kurudi usiku sana kwa kuona aibu.
  Huyo mume wa Grace aende hospital wakapime!!
   
 4. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kwani gazeti la uwazi si gazet?
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  ndilo gazeti haswaaaa la udaku
   
 6. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  dah
  mume mnyanyasaji jaman
  kuna mwanamke asiyependa kushika mimba jaman?tena ushaolewwa?ahh mbona anamowngozea donda kwenye kidonda?
  ilibd mume wake awe anamfariji sasa si maneno shombo km ayo

  jamaa anajifanya yupo fit kwa uhakika gan?usikute ana mtoto nje tayar?
  dah pole
   
 7. Linamo

  Linamo JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 9,060
  Likes Received: 21,275
  Trophy Points: 280
  Huyo hana lolote,anajua tatizo lake ndiyo mana hataki kwenda kupima,anaamua kujikinga kwa kumfukuza mwanamke.
   
 8. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hv mwanaume au mwanamke akiwa tasa viungo vya uzazi vinafanya kazi?
   
 9. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #9
  Feb 2, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Rose, kama kuna mtoto wa nje anaweza kuwa sio wake vile vile. Ni vizuri wakaenda wote Hospitali
   
 10. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #10
  Feb 2, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Viungo vinaweza kufanya kazi bila wasi wasi, kuna sababu nyingi zina weza sababisha mtoto asipatikane
   
 11. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #11
  Feb 2, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Aniletee huyo nimchakachue aone kama kitu hakitanasa.
   
 12. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #12
  Feb 2, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  angalia unaweza kuchemka wakasema na wewe ukapimwe
   
Loading...