Nyumba aliyoishi RC wa Iringa Dr. Kleruu kabla ya kuuawa na Said Mwamwindi

Alinyongwa, Mwalimu alimsihii akane awe aliua bila kukusudia alikataa katu. Dr. Kreluu alikua mwasherati wa kutembea na watoto pia wake za watu. Adabu aliipata, shujaa Mwamwindi..
Kwahiyo alivyokataa ushauri wake akaamua kumnyonga! Sidhani kama ni kweli.
 
Africar KAGEMA
Utaifa, Uzalendo, Uwajibikaji na Siasa Safi ndizo nguvu za Maendeleo.
Thursday, June 21, 2012
Kwa nini mkulima Mwamwindi alimpiga risasi RC Dk. Kleruu?
Maggid Mjengwa
IRINGA ina historia ndefu ya harakati za mapambano ya kudai uhuru. Harakati za kijamii, kisiasa na kiuchumi. Wakati huu nchi yetu ikielekea kwenye kuadhimisha miaka 50 ya uhuru si vibaya tukakumbushana tulikotoka ili tuweze kuelewa tulipo sasa na tunakokwenda.
Hakika, simulizi ya Mkulima Saidi Mwamwindi aliyepambana na dola ni moja ya simulizi zilizowagusa wasomaji wangu wengi.
Ni simulizi iliyonifanya nihamasike kutafuta habari zaidi za Watanzania mfano wa Mwamwindi ambao, hata kama huko nyuma jamii ilitakiwa iwaone kama wasaliti, lakini, jamii si mkusanyiko wa watu wajinga. Kuna walioulewa ukweli, waliamua kukaa kimya. Na wakati mwingine walisema na hata kuimba kile ambacho watawala waliwataka waimbe na kusema.
Hata hivyo, mioyoyoni mwao, waliujua ukweli. Kuna walioimba huku wakilia mioyoni. Kuna waliosema huku wakisononeka mioyoni.

Huu ni wakati wa kujaribu kuusema ukweli ili tuweze kwenda mbele kama taifa.
Simulizi ya mkulima, Saidi Mwamwindi ni jaribio la kuutafuta ukweli huo. Na hii ni simulizi shirikishi yenye kukukaribisha ewe msomaji, uje na unachokijua juu ya kilichotokea zaidi ya miaka 40 iliyopita.

Mwamwindi ni kielelezo cha hali iliyokuwepo wakati huo. Mathalan, utekelezaji wa Sera za Ujamaa na kilimo cha ushirika ulitakiwa utekelezwe kwa kuzingatia mazingira ya kila mahala.

Inakuwaje basi kwa mkuu wa nchi unapomweka mkuu wa mkoa kijana anayeanza kwa kuwahutubia wakulima wakubwa mfano wa Saidi Mwamwindi habari za kilimo cha heka nne nne?

Wakulima ambao tayari, hata kabla ya Uhuru wameweza kuwa na matreka na hata kuanzisha ushirika wao wa wakulima. Ndio, inawezekana vipi kwa mkulima wa shamba la ekari mia nne akajisikia furaha kuwa kwenye mkutano na mkuu wa mkoa anayezungumzia kilimo cha ekari nne nne? Mbinu gani ya kiuongozi ilihitajika ili kumfanya mkulima mkubwa kama Mwamwindi ashiriki na kuwasaidia wakulima wadogo wadogo?

Na hapa inaanza simulizi ya Mwamwindi;
Mwanzoni mwa miaka ya 1970 mkulima, Saidi Mwamwindi alikabiliwa na shitaka la kumwua Dk Wilbert Kleruu, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa wakati huo.

Mshitakiwa Mwamwindi alijitetea kuwa alipokuwa anamwua marehemu Kleruu alirukwa na akili . Hivyo, akapotewa na fahamu ya kuweza kuelewa kile alichokuwa anakitenda. Jaji Onyiuke kutoka Nigeria aliukataa utetezi wa Mwamwindi kwa kutilia maanani kwamba baada ya mshitakiwa kughadhibishwa ndipo alipokwenda ndani kuchukua bunduki ambayo aliitumia kumwua marehemu.

Oktoba mwaka 2010, nikiwa njiani kwenda Dodoma na Arusha, nilipita kijijini Isimani. Hapo ndipo yalipokuwa makazi ya Mwamwindi. Ni umbali wa kilomita zipatazo 40 kutoka Iringa Mjini. Kijijini Isimani Saidi Mwamwindi bado anaonekana ni shujaa kwa kukataa kunyanyaswa na Mkuu wa Mkoa.

Inasimuliwa, kuwa ilikuwa siku ya Jumapili, tena siku ya Krismasi, pale Mkuu wa Mkoa, Dk Kleruu, alipofika Isimani na kumkemea Mwamwindi mbele ya wake zake kwa vile alifanya kazi za shamba siku ya Sikukuu.

Inasimuliwa, kuwa Dk. Kleruu alifikia hata hatua ya kuanza kudhihaki makaburi ya mababu zake Mwamwindi akimwambia Mwamwindi: “Humu ndimo mlimozika mirija yenu”. Alifanya hivyo huku akionyesha makaburi yake kwa kutumia fimbo aliyoshika mkononi. Mwamwindi alikasirika sana. Akaficha hasira yake.

Kutoka makaburini, Mwamwindi aliongozana na Kleruu hadi nje ya nyumba yake. Akamwomba Mkuu huyo wa Mkoa abaki nje. Mwamwindi akaingia ndani chumbani.

Mke wake Mwamwindi alimwona mume wake akichukua bunduki na kusimama dirishani. Mama huyo alidhani mumewe amepanga kwenda kuwinda. Kumbe, Mwamwindi alitokea dirishani na kumwelekea Kleruu aliyedhani Mwamwindi angetoka nje kwa kupitia mlangoni.

Basi, Mwamwindi akamlenga Mkuu wa Mkoa sawa kichwani. Dk kleruu alinyoosha mikono juu na kuomba asemehewe. Mwamwindi alikaa kimya. Kisha akafyatua risasi. Kishindo kilisikika
kijijini. Baada ya hapo, kwa mikono yake, Mwamwindi akaubeba mwili wa Mkuu wa Mkoa na kuuweka nyuma
 
iliyo mnyonga ni sheria ya nchi mzee, au hujui kama rais still yuko chini ya katiba!
Kuna watu wamehukumiwa kunyongwa lakini imeshindikana kunyongwa kwa sababu rais hajasaini hukumu kutekelezwa au hujui? Kwahiyo angetaka hasinge nyongwa
 
Mkuu hebu funguka, niliwahi kuwaukiza wenzangu same question why alienda mwenyewe? Why ali drive mwenyewe?

Mkuu sheria yetu inani-limit kwenda beyond. Lakini ukitafakari jibu liko wazi na wala halihusiani na kazi
Kwanini alienda pekee yake kwa mkulima huyo

Kwanini aendeshe gari yeye mwenyewe

Kwanini hakukuwa na mtu yeyote zaid ya mkuu mwenyewe

Kwanini zipo nyingi sana, ukiweza kuzipa sababu ukweli utaupata.
 
Munyalukolo mwamwindi akakamata riffle akasema this my riffle, this my gun, tis for fighting, this for fun. Akamtandika Dr kleruu akarest in peace.......

Nani kakwambia jamaa ali rest in peace???? Teh
 
Na taarifa juu ya siku ile ya tukio la mauji zimekuwa zikiwachanganya wengi hadi hii leo. Kupitia mfululizo wa simulizi hizi, zimeanza kujitokeza taarifa mpya zinazotoa mwanga wa kilichotokea. Mathalan, kuna polisi mstaafu aitwaye Mushi na ambaye kwa sasa anaishi Moshi akiendesha kampuni ya ulinzi ana haya ya kusema; Bwana Maggid, mimi nilikuwa kaunta siku ile ya tukio; Jumapili ya Krismasi, Desema 25, 1971. Bwana Butunini uliyeongea naye tulikuwa naye pale polisi Iringa. Siku ile ya tukio, asubuhi kabisa Dk. Kleruu alifika pale polisi baada ya kutoka kwa RPC Aboubakar.

Kleruu na mimi tulikuwa marafiki baada ya kumsaidia kwenye upepelezi wa wizi uliotokea nyumbani kwake na nikafanikiwa kupata vitu vyake karibu vyote vilivyoibwa nyumbani kwake. Ulikuwa wizi wa ajabu maana nyumba ya Mkuu wa Mkoa ilikuwa inalindwa,” anasema Mushi. Kisha anaendelea kusimulia; Tangu hapo tukawa na uhusiano wa kirafiki na Mkuu wa Mkoa Kleruu. Nakumbuka siku ile ya tukio alipofika pale kituoni aliniaga kwa kuniambia anaenda Nyang’olo kwenye mambo ya kilimo. Kisha akanikaribisha jioni hiyo niende nyumbani kwake nikale Krismasi. Basi, baadaye tukajua kuwa afande RPC Aboubakar alimwambia ampe walinzi wa kwenda nao, lakini Kleruu alikataa.”
 
Uoga upi wa kuishi nyumba hiyo? Alafu naona kama nyumba imetelekezwa kama gofu vile. Watenge bajeti waikarabati watumishi wa serikali wanahangaika na uhaba wa nyumba za umma

..Magufuli hakuipiga bei hiyo nyumba?

..nashangaa kwanini mafisadi hawakuiona hiyo nyumba wakainunua kipindi kile Dr.Magu anauza nyumba za serikali.

Cc Bukyanagandi
 
Huyu mtoto wake Said Mwamwindi ambaye alikuwa meya na sasa ni diwani wa kata ya Mlandege nitamuuliza ili anisimulie kisa hiki nami niwajuze kwa upande mwingine.
 
..Magufuli hakuipiga bei hiyo nyumba?

..nashangaa kwanini mafisadi hawakuiona hiyo nyumba wakainunua kipindi kile Dr.Magu anauza nyumba za serikali.

Cc Bukyanagandi

Mkuu J.kuu, kitu cha kwanza wanasema ina mizimu sijui ghost ya mtu gani - watu uogopa kuinunua inanikumbusha English farmhouse.

Tukija suala la Dk.Magufuli tukumbuke yeye alikuwa ni mtekelezaji wa amri za Waziri mkuu one F. Sumaye na Rais - kama nakumbuka vizuri Sumaye aliwahi kusema kwamba yeye ndiye anaweza kuwapa ufafanuzi wa kina kuhusu uuzwaji wa nyumba za Serikali kwa seating tenants ambao ni waswahili wenzenu, je, wangewauzia matajiri/ wafanya biashara tungeweza kulalamika kweli? - Ukweli ni kwamba tungekaa kimya.

Binafsi huwa sielewi upinzani mkubwa wa zoezi hili, mashirika mengi yaliwauzia nyumba wafanyakazi wao mfano: Tazara na Bandari just 2 mention a few sasa tatizo ni nini hasa - nikisema labda tatizo ni la kisaikolojia zaidi yaani la "KWA NINI" je, ntakuwa nimekosea?

Siyo kwamba watu wana uchungu wa kweli wa nyumba hizo kuuzwa kwa Watanzania wenzao, nyumba zenyewe za enzi za ukoloni nyingi zinahitaji facelift ya kufa mtu - nikienda nikaziagalia zinazidiwa na nyumba iliyo jengwa na mzee wangu kijijini mwaka 1946 ingawa vigae zinafanana.

Sasa lawana kubwa kwa nini huwa inaelekezwa kwa mtu mmoja, huwa sijui kwa nini members wengi wa JF upenda sana ku - "KILL THE MESSENGER" (JPJM) na kuwahacha Waziri mkuu, Rais na baraza lote mawaziri - it was a collective decision I guess - why pick on Dk.Magufuli if I may ask?
 
..it was a collective decision lakini Magu ndiye alikuwa mtekelezaji.

..ppl want to get to the bottom of this issue na ndiyo maana wanamchokonoa huyu bwana.

..ni kweli nyumba zile zilikuwa zimechakaa. Lakini je ingekuwa mali binafsi ya Magu angeuza kwa bei ile ya hasara??

..je walikuwa hawajui kwamba wanakwenda kuitia nchi hasara?

..HASARA hiyo ndiyo inayowafanya wengi tuhoji uhalali wa zoezi lile.
 
Mkuu J.Kuu, watu wanacho sahau ni kwamba kinacho fanyika ni kwamba unangalia nyumba ulijengwa kwa gharama gani, je tangu wakazi/tenants waanze kulipa kodi, je, sum total ya kodi over the years ilishavuka return of investment na kuhanza kuvuna faida au la?

Tukiweka maanani kwamba nyumba hizo zilijengwa zamani sana ni dhahili ziliisha jilipa na faida juu, hivyo Serikali ikiwahuzia wapangaji kwa bei ya kawaida haitapata hasara after all lengo la Serikali lilikuwa ni kuwawezesha wapangaji kumudu kununua nyumba hizo kwa bei ndogo siyo Serikali kupata faida ya ziada.

Zamani hata National Housing Corp iliwahi kuwauzia tenants nyumba, hata Ulaya specifically Uingereza huwauzia wapangaji Council flats bila ya kujali kama mpangaji ni raia au la - what counts ni hela yako tu.

Kwa hiyo suala hili ya nyumba za Serikali tusilivalie njuga sana, hakuna haja ya kulichukulia kama ni suala la uhaini vile, mimi mpaka sasa nina imani kwamba Serikali ilikuwa na nia safi kuwauzia wapangaji nyumba.
 
..nimeuliza swali ambalo hujalijibu.

..je, mkapa, kikwete, sumaye, lowassa, magufuli, au mtanzania yeyote, angekuwa anamiliki moja ya nyumba zile je angeuza kwa bei ya hasara kiasi kile?

..ule ulikuwa ni WIZI na HUJUMA ya waziwazi. Cabinet ilikuwa inajua nini kinakwenda kutokea.

..Waziri mwenye dhamana na nyumba zile ambaye alipaswa kuupinga uamuzi huo naye akawa mstari wa mbele kutekeleza hujuma hiyo.

..sasa sijui kama unafahamu kwamba Dr.Kawambwa alipata kuliambia bunge kuwa serikali haikufikia lengo la mapato ililokuwa imejiwekea walipochukua uamuzi wa kuuza nyumba.

..Yaani hiyo ni hasara juu ya hasara.

..ni kweli ulaya, marekani, canada, etc wana programs za kuuzia WANANCHI WA KAWAIDA nyumba za bei nafuu.

..sijawahi kusikia wakina Bill Clinton, George Bush, Tony Blair, na wakubwa wa serikalini za nchi hizo wakisuka mipango ya kujitwalia assets za serikali zao kwa bei ya hasara.

..tena huko magharibi wakiwa na mpango wa kuuza nyumba kwa wananchi wa kawaida wasimamizi wa mpango huo hawaruhusiwi kununua nyumba hizo au kufaidika kwa namna yoyote ile.

..mwisho, hii nchi ina matatizo mengi sana. Sasa sitegemei serikali yetu ikauza assets zake kwa mtindo wa kihasara-hasara kama ilivyofanyika ktk kuuza nyumba za serikali.

..nyumba zile zingeuzwa kwa bei ya SOKO tungeweza kutatua baadhi ya matatizo yetu mfano ujenzi wa maabara, maktaba, madawati etc etc.
 
Wewe ndo unayepotosha. Toka lini mkuu wa mkoa akaenda oparesheni peke yake, na gari la ofisi, bila walinzi hata dereva!!!!

Fikiria mara mbili kabla ya kuubishia ukweli

Halafu ilikuwa siku ya sikukuu za mwisho wa mwaka ni krismas kama sijakosea.
 
Someni kisa hicho kipo gazeti la mwananchi la wiki hii yote...
Wacheni kupotosha.
Mwamindi alikua shujaa pekee aliepinga siasa za ujamaa za kunyanganya watu mashamba yao na kuwataka watu kulima ujamaa
Kaka usipate tabu watoto wengi wa juzi humu JF. Mbaya zaidi, hawapendi kusoma wao hukurupuka kwa conclusion zao bila kuulisha ubongo vema maarifa.
 
Back
Top Bottom