Nyumba aliyoishi Baba wa Taifa baada ya kuacha kazi ya Ualimu 1955

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,913
30,255
ALIPOISHI BABA WA TAIFA BAADA YA KUACHA KAZI YA UALIMU 1955

Hapo ilipo nyumba hii ilikuwapo nyumba ya kawaida ingawa kwa wakati ule nyumba hiyo ilikuwa nyumba ya kuvutia pia.

Nyumba hiyo ilikuwa na duka la mwenye nyumba hiyo na barazani palikuwa na barza maarufu ya wazee wa mjini maarufu.

Watu maarufu waliokuwa wanabarza walikuwa Aziz Ali, John Rupia, Ali Jumbe Kiro, Mzee bin Sudi kwa kuwataja wachache.

Hapa ndipo ilipokuwa nyumba ya Mzee Kleist aliyojenga mwaka wa 1942.

Yaliyopitika nyumba hii Bi. Aisha "Daisy" Sykes kayaeleza vizuri katika makala aliyoandika mwaka 2018 katika kumbukumbu ya baba yake Abdulwahid Kleist Sykes.

Msikilie Daisy anavyokumbuka baadhi ya yale anayokumbuka kuyaona kati nyumba hii wakati akiwa msichana mdogo:

''Wageni hawa mashuhuri waliokuwa wakija nyumbani ni pamoja na Mangi Mkuu Thomas Marealle, Machifu Abdiel Shangali, John Maruma kutoka Moshi, Adam Sapi Mkwawa kutoka Iringa, Kidaha Makwaia kutoka Usukuma, Abdallah Fundikira, Harun Lugusha kutoka Tabora, Humbi Ziota kutoka Nzega, Michael Lukumbuzya kutoka Ukerewe na Patrick Kunambi kutoka Morogoro na wengine wengi. Hawa machifu kwa kawaida walikuwa wakija na wake zao, wanawake warembo ambao hawakuacha kunifanya mimi kuwashangalia.

Nakumbuka katika machifu wale, alikuwapo chifu mmoja na wa pekee mwanamke - Mwami Theresa Ntare kutoka Kasulu Kibondo. Katika hali kama hii iliyokuwa tabu kufahamika, tukiwa watoto tulipata kujua maisha ya jamii nyingine, lugha zao, utamaduni wa makabila mengi ya Tanganyika kabla ya watu wengi kutoka sehemu nyingine za pwani hawajajua chochote kuhusu watu hawa.

Nilibahatika kukutana na katika utoto wangu na lile tabaka la Waafrika waliokuwa watumishi wa serikali, kundi dogo makhsusi lililokuwa linakua na liliopembuka kwa elimu zao kutoka Chuo Cha Makerere, Uganda na vyuo vingine.

Hiki ndicho kilikuwa kizazi kipya cha Watanganyika wasomi waliohusika na kuasisi siasa fikra ya uhuru itakayopelekea Waafrika kujitawala - Hamza Mwapachu, Zuberi Mtemvu, Mzee John Rupia, Steven Mhando, Dunstan Omari, Dossa Aziz kwa kuwataja wachache.

Kulikuwa pia na tabaka jingine la watu maarufu kutoka Zanzibar kama Ahmed Rashad Ali and Abdul Razak Abdul Wadud ambao walikuwa kama sehemu ya familia yetu.

Siwezi kumsahau Maloo, Mburushi kutoka Congo ya Mashariki ambae alikuwa anakaa nyumbani na baba kwa muda mrefu sana kiasi tuliamini ni mmoja katika familia ya Sykes.

Lakini aliyeshika nafasi ya juu kabisa katika fikra zangu nikiwa mtoto alikuwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na ni kupitia kwake ndipo tukapata kujua kwa mara ya kwanza kuwa kuna kabila linaitwa, ‘’Wazanaki.’’

Kila alipokuwa anakuja nyumbani kwetu kuja kwake kulikuwa jambo maalum kulikosababisha minong’ono watu wakizungumza kwa sauti za chini wakipeana taarifa kuwa, ‘’Nyerere anakuja au keshafika.”

Kwangu mimi hii ilikuwa ishara ya kutimiza kazi yangu kwani siku zote nilikuwa nikiambiwa kutengeneza kifungua kinywa cha chai na mayai kila alipokuja nyumbani akitokea Shule ya Mt. Francis,Pugu alipokuwa akisomesha.

Nakumbuka katika akili yangu ya kitoto kumuona Mwalimu Nyerere akiishi nyumbani kwetu kwa muda katika nyumba yetu ya Mtaa wa Stanley baada ya kuacha kazi wakati marafiki zake wa karibu baba na Dossa Aziz walikuwa wanamtafutia nyumba ya kuishi.

Nyumba yetu ya Stanley kwa kuwa ilikuwa kwenye makutano ya barabara mbili ilikuwa na mjengo wa kipekee kwa nyakati zile.

Nyumba kubwa na yenye vyumba kadhaa ilikuwa upande wa Mtaa wa Stanely na upande wa Mtaa wa Sikukuu ilikuwa nyumba nyingine inayojitegemea ikiwa na sebule na chumba cha kulala hapo hapo.

Ingawa upande huu wa nyumba ilikuwa na nafasi ya kutosha ilikuwa vigumu kwa wanaume wawili wakubwa kuishi pamoja.

Naamini baba yangu Abbas ambayo sehemu ile ndiyo aliyokuwa akiishi ikabidi ahame kwenye nyumba ile aende kweye nyumba yetu nyingine Mtaa wa Kipata au ajibane nyumba kubwa ili Mwalimu Nyerere apate utulivu na faragha katika nyumba ile.''

Nyumba hii anayoihadithia Daisy ilivunjwa miaka mingi na badala yake sasa familia imejenga nyumba hii tuionayo hapa.

Nyumba hii imeondoka katika uso wa mji wa wa Dar es Salaam na historia yake na wala hakuna hata kibao cha kueleza umuhimu wa nyumba hii.

Picha ya pili inamwonyesha Prof. Mohamed Khalil Timamy ambae baada ya kumfikisha hapo na kumwelea historia ya nyumba hii aliniomba nimpige picha sehemu ile ya upande wa nyumba ya ambao Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliishi na Abdul Sykes mwaka wa 1955 baada ya kuacha kazi ya kufundisha.

Picha ya tatu na nne ni Mangi Mkuu Thomas Marealle na Mwami Theresa Ntare, picha ya tano ni nyumba yenyewe ya Abdul Sykes kama ilivyokuwa miaka.ya 1950 na picha ya sita ni nyumba ambayo TANU ilimtafutia Nyerere Magomeni Maduka Sita ambako alihamia.

Upande wa kulia wa nyumba hiyo ndipo ilipokuwa sehemu katika nyumba alipoishi Julius Nyerere.

Muhimu kwa kuweka kumbukumbu kuwa hapa sasa iliposimama jumba hili ndipo mikakati ya kumng'oa Mwingereza ilipokuwa ikifanyika.

Angalia picha ya sita na ya mwisho nyumba aliyotafutiwa Nyerere na TANU akahamia Magomeni Maduka Sita.

Nyerere anaonekana nje ya nyumba hiyo akiingia ndani.

Screenshot_20210913-181833_Facebook.jpg

Screenshot_20210913-182055_Facebook.jpg

Screenshot_20210913-182417_Facebook.jpg

Screenshot_20210913-191453_Facebook.jpg
 
View attachment 1936239
View attachment 1936242
View attachment 1936245
View attachment 1936311
Natumai utakuwa umeandika vitabu kuweka kumbukumbu kwa vizazi vya sasa na vijavyo
 
Duh kuna bonge la gorofa pembeni ya hiyo nyumba aliyoishi Nyerere na Sykes 1955.

Kumbe wakati wa mkoloni tayari kulikuwa na watanzania matajiri wakubwa.
Cash...
John Rupia, Dossa Aziz na Abdul na Ally Sykes walikuwa watu wa nafasi toka miaka ile ya kupigania uhuru na ndiyo walikuwa wafadhili wakubwa wa TANU.
 
Ugumu wa katiba tunapitia kutokana na tabia za Kambarage. Hana ubaba wa taifa wowote.
 
Back
Top Bottom