Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,862
- 930
MHE. GODWIN MOLLEL - NYUMBA 52 ZA WATUMISHI ZIMEJENGWA MWAKA HUU WA FEDHA
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali kupitia Wizara ya Afya imejenga nyumba za Watumishi 52 zenye thamani ya Tsh. Bilioni 3.417 katika Hospitali za Rufaa za Mikoa na Hospital za Kanda ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuboresha utoaji huduma kwa Wananchi.
Dkt. Mollel amesema hayo leo Aprili 25 Bungeni Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Dkt. Ritta Enespher Kabati katika Mkutano wa kumi na moja.
Amesema “Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imejenga nyumba 52 za Watumishi zenye thamani ya Tsh. 3,417,556,981 katika Hospitali za Kanda na Hospitali za Rufaa za Mikoa ikiwemo nyumba moja katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa”
Amesema Serikali itaendelea kujenga nyumba kwa ajili ya Watumishi ili kuwapunguzia changamoto, jambo linaloongeza hamasa katika utendaji wao na kuboresha utoaji huduma kwa Wananchi.