Nyumba 300 zabomolewa kata za Mabwepande, madale - Dar es Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyumba 300 zabomolewa kata za Mabwepande, madale - Dar es Salaam

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Annael, Aug 22, 2012.

 1. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,270
  Likes Received: 10,278
  Trophy Points: 280
  Samahani sana wana JF kama nitakuwa nimekosea.
  Jana jioni nilikuwa nasikiliza taarifa ya habari televisheni ya ITV kuhusu hali ya wananchi waliohamishiwa eneo la mabwepande kutoka mabondeni.

  Hali kule sio nzuri vyoo vimejaa, mahema yanaliwa na mchwa na hakuna jitihada yoyote iliyofanywa na wananchi hao.

  Mimi nilianza kujiuliza maswali mengi sana.
  1. Hivi hao wananchi waliohamishiwa huko hawana uwezo wa kuchimba vyoo kwa manufaa ya afya zao na kuanza kulalamikia serikali?
  2. Mimi sielewi zaidi kuhusu makubaliano yao na serikali. Mimi nimekulia kijijini tena usukumani ninachojua wananchi hao wamejengea mahema sio makazi ya kudumu wanachotakiwa wao wenyewe kujenga nyumba zao.
  Yaani hata kufyatua tofali za udongo tu wanashindwa? je hao raia wamekatazwa kujenga na serikali? kama hawajakatazwa wakulaumiwa ni serikali?

  Jamani watanzania wenzangu vitu vingine tunaendekeza mambo yanayotuhusu tusiilaumu serikali. Hii ni aibu kubwa mwanaume aliye na nguvu kulaumu kuwa choo chake kimejaa na anaomba serikali imuchimbie choo.


  Aise hii sikuipenda.
   
 2. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  walitunyang'anya mashamba yetu kule sasa hivi ndio hali imeharibika kabisa...ndo serikali yetu ya ccm hiyo
   
 3. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,270
  Likes Received: 10,278
  Trophy Points: 280
  Hujanielewa ninachoongelea soma kitu ninacho kieleza hapa silaumu serilkali au CCM.
  Usiwapotoshe watu yaani kuchimba choo unalaumu CCM!
   
 4. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hayo maeneo wanayoishi sio ya kwao..yalikua mashamba ya watu wakavamia serikali imeahidi kuwalipa watu mpaka leo hakuna kitu...kwani kujenga choo lazima serikali wafanye...sisi watanzania tushazoea kufanyiwa kila kitu...na hata serikali ikijenga hizo choo zitakaa kwa mda gani..nani atazisimamia?
   
 5. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,270
  Likes Received: 10,278
  Trophy Points: 280
  Usiseme sisi watanzania tumezoea kufanyiwa kila kitu na serikali. Yaani kuchimba choo chako mpaka usimamiwe?
  Ndugu yangu tutafika kweli?
  Mimi sijajua kwann hawa watu hawachimbi choo na wanailaumu serikali.
   
 6. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,333
  Likes Received: 2,328
  Trophy Points: 280
  Hapa lugha gonganaaa bhana.
   
 7. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,333
  Likes Received: 2,328
  Trophy Points: 280
  Waacheni hadi vinyesi viwasogele milangoni mwao ndo watajua dinfi si rafiki wa afya ya mwanadamu.
   
 8. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Kila mtu hupenda anachokitaka. Hawa ndugu zetu wao wanapenda harufu ya mavi kuona mavi yametapakaa kuwazunguka.
   
 9. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Mleta mada kama unajua hayo si makazi ya kudumu kwanini unataka wachimbe vyoo vya kudumu? Hizo tents wamepewa na serikali? Serikali ilikozitoa hizo pesa za kununua tents kwani hazikutengwa za mobile toilets?

  Usitetee ufisadi, mkuu Annael
   
 10. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #10
  Aug 22, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  labda ni sababu ya kukata tamaa ndio maana wanashindwa hata kuimiza wajibu wao.
   
 11. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Watanzania wengi si responsible!
  Yaani ni kulaumu tu kila kitu kila kukicha!
   
 12. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,270
  Likes Received: 10,278
  Trophy Points: 280
  Mkuu Azipa Hujanielewa ninachoongelea. Hili siyo jambo la kisiasa. Je wamekatazwa kujenga nyumba? je wamekatazwa kuchimba vyoo? Hivi Choo chako wewe mwenyewe uchimbiwe na serikali?
  Hivi ni uzembe! ujinga! au kukwepa majukumu?
   
 13. M

  Msendekwa JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 440
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kweli hao wa mabwepande wamezid uzembe.
  Si ndo walitoka Jangwani hawa walikolazimishwa kuhama ili kuokoa uhai wao wenyewe?
  Ndo maana walishindwa hata kumuokoa Ulimboka alipotupwa kwao!
   
 14. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #14
  Aug 22, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Vyoo hivi wameshavijaza tayari?

  [​IMG]
   
 15. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #15
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Siasa haiepukiki, hizo tents inatakiwa ziambatane na mobile toilets. Mtu kishakula pesa hapo

  Halafu mkuu, wewe mwenyewe umekiri hujui mapatano yao. Je watajengaje vyoo ikiwa labda hata viwanja havijagawanywa rasmi?

  Just a thought, mkuu
   
 16. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #16
  Aug 22, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,270
  Likes Received: 10,278
  Trophy Points: 280
  Jamaa langu sikiliza Mimi jana nilikuwa nasikiliza taarifa ya habari tatizo hapa sio wamezuiliwa. Sijasikia hata mmoja akisema waruhusiwe kujenga vyoo. Wangekuwa na nia ya kujenga vyoo ninge sikia. Walikuwa wanalaumu kuwa serikali imewaacha na wanataka kujengewa vyoo.
  Nadhani umenipata.
   
 17. kupe

  kupe JF-Expert Member

  #17
  Aug 22, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 1,025
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  wanataka kikwete na ccm wakawachimbie kudadadeki zao
   
 18. Tungaraza Jr

  Tungaraza Jr Senior Member

  #18
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  Nyumba takribani 300 zikiwamo za kifahari, zimebomolewa baada ya kubainika kujengwa katika maeneo mbalimbali yaliyovamiwa katika Kata ya Mabwepande na Madale wilayani Kinondoni, mkoani Dar es Salaam.

  Operesheni ya kuwaondoa wavamizi wa mashamba iliyoanza jana saa 12 asubuhi, ilifanywa na Serikali ya Wilaya ya Kinondoni chini ya ulinzi mkali wa askari polisi waliokuwa na magari yapatayo 30 yakiwamo matingatinga manne na gari la wagonjwa.

  Baada ya kuanza operesheni hiyo, kulitokea tafrani kidogo baada ya wananchi waliokuwa katika vikundi kutumia silaha za jadi kama mishale, mapanga kuwashambulia polisi, jambo lililolazimu jeshi hilo kutumia mabomu ya machozi katika kuwatawanya.

  Katika operesheni hiyo iliyofanyika kwa awamu, wananchi ambao maeneo yao yalivamiwa, walikuwa wakiongoza kuonesha wavamizi na kisha kubomolewa nyumba na baadaye kuchoma moto nyumba hizo zilizokuwa zimejengwa kwenye eneo hilo ambalo lina vilima vingi.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema wametumia nguvu ya wastani katika kusimamia operesheni hiyo na watu takribani 20 wanashikiliwa na jeshi hilo baada ya kuanzisha vurugu.

  "Tulipata upinzani kidogo wakati tunaanza, jambo ambalo tulilazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya na kuendelea na kazi hiyo. Kazi imefanyika vizuri na hakuna askari wala raia yeyote aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa," alisema Kamanda Kenyela ambaye katika awamu ya pili ya bomoabomoa, alitaka kusiwapo na uchomaji moyo nyumba zilizobomolewa.

  Alisema katika operesheni hiyo, wamekamata mitambo ya pombe haramu ya gongo na walichobaini ni kuwa eneo hilo lilikuwa maficho ya wahalifu wa ubakaji, ukabaji na ujambazi uliokuwa ukifanyika hapo.


  Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana alisema eneo hilo limekuwa na mgogoro wa ardhi wa muda mrefu na kuwa kazi waliyoifanya ni kuwaondoa wavamizi wapya katika eneo hilo lililovamiwa la kata za Mabwepande na Madale.

  "Mgogoro wa hapa ni tofauti, zamani kulikuwa na tatizo la umilikaji wa watu zaidi ya mmoja katika eneo moja, lakini sasa kuna kundi la vijana ambao wanavamia maeneo ya watu na baadaye wanayauza, wengi wa waliobomolewa ni wale waliouziwa na wavamizi," alisema Rugimbana.  Source:
  wavuti - wavuti
   
 19. shegaboy

  shegaboy JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana Mh. Rugimbana na kamanda Kenyela inakuwaje askari wako baada ya kulinda mali za watu wao wanaanza kupora mali za watu? kuna jamaa mmoja anaonyesha video pale madale serikali ya mtaa (Flamingo) sio huko waliko wavamizi ila chakushangaza ni kuwa maaskari walipokuja walichukua tv yake na jenereta na kumtishia kuwa watampiga risasi kama anabisha. na wengine walikuwa wanakunywa vinywaji mbali mbali pale flamingo. unasemaje kamanda kweli ndio maadili haya na leo tena nasikia kazi imeanza tena ngoja niende nyumbani kwangu maana awaaminiki kabisa
   
 20. C

  Cisauti Member

  #20
  Aug 23, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Naona kama kichwa cha habari na maelezo vyatofautiana vile......adha za wahanga wa mafuriko na kubomolewa kwa nyumba.....!!!!????
   
Loading...