Nyumba 2 za kisasa zinapangishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyumba 2 za kisasa zinapangishwa

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Respect, Jun 24, 2009.

 1. Respect

  Respect Member

  #1
  Jun 24, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ziko Mwananyamala A, DSM. Ni za kisasa na hadhi ya juu kabisa na vitu vifuatavyo;
  Electrical fence, kwa ujumla mfumo wa kisasa wa ulinzi, A/C full kwenye "master" na sebuleni, vyumba 3 vyakulala na kimoja "master", line mbilimbili za maji hivyo maji ni uhakika 100%, kila moja inaweza kuingiza gari ndogo tatu, barabara ya lami hadi mlangoni ujirani mwema mzuri, eneo lote la ndani ya uzio wa kila nyumba limesakafiwa likiwa na maua hapa na pale n.k
  **Kila moja inapangishwa kivyake.
  Bei ni 700,000/ Tzs kwa kila nyumba kwa mwezi..

  Piga simu 0773 244254, 0787 101961

  Samahani dalali hatakiwi wapendwa!
   
  Last edited: Jul 10, 2009
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Seems they are good houses...but 1,000k/pm?....and how many months to be paid for in advance?
   
 3. Respect

  Respect Member

  #3
  Jun 24, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndiyo ndugu yangu ni nyumba nzuri sana tu, nakuhakikishia.
  Hiyo bei ya milioni1 kwa mwezi inarekebika kidogo ukiongea sawasawa, na hata months to be paid as advance linaongeleka pia.

  Karibu...
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  kwanza karibu sana hapa JF, lakini naomba nikuulize wewe ni dalali au ndio mwenye hiyo mijengo, aisee unajua haya mambo ya kupangisaha inategemea na lication, hata kama nyumba hiko nzuri kiasi gani lakini location in matter, kwa hiyo bei ya 1k kwa mwezi kwa kweli ni kubwa sana hebu jipange vizuri uje na bei ambayo haina maongezi, hii ya kusema pungufu tutaongea ndio inakuwaga na mashaka
   
 5. Respect

  Respect Member

  #5
  Jun 24, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru ndugu yangu, mie sio dalali. Kuhusu Location usitie shaka hilo limezingatiwa, na hiyo Mwananyamala siyo ile yenye patashika tele! Hiyo sehemu imetulia mno, naamini utaipenda kwa asilimia100% na mengine ni kama nilivyoeleza hapo juu.

  Karibu..
   
 6. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2009
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Lete picha zake tuone. Ila Mwananyamala kwa 1M kwa mwezi! Mhhhhhh! Hizo ni bei za Masaki na Oyster Bay rafiki.
   
 7. Respect

  Respect Member

  #7
  Jun 24, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usijali tajiri wangu, ntaziweka hizo picha ngoja nishughulikie hilo. Ndugu yangu, hizo ni bora kuliko hata hizo za Masaki!
  Kuhusu Mwananyamala kwa 1m, zingekuwa masaki ingekuwa bei maradufu! Hata hivyo hiyo mwananyamala ni ile iliyotulia siyo "Uswazi".......

  Narudia kwenye bei mazungumzo yapo.
   
 8. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  bei ni kubwa sana
  tunaomba picha za ndani na nje na area view
   
 9. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  watu mnaotaka picha nk ni wapangaji au basi tu?
   
 10. Respect

  Respect Member

  #10
  Jun 24, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usijali ndugu yangu mteja mfalme, naendelea kushughulikia picha ili niwaridhishe wazee wangu.
   
 11. Grader

  Grader JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 446
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  bei siyo mbaya sana ila nataka ulete picha za hiyo nyumba nje na ndani na ikiwezekana eneo linalozunguka hapo kwenye nyumba,na kuweka wazi mashariti ya mkataba wa hizo nyumba kwani wenye nyumba wengine watata kwani hata wanatakaga namba na picha ya mke wa anayepanga nyumba.
   
 12. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  locatio ni ule mtaa karibu na makaburini kwa manjunju?
   
 13. Respect

  Respect Member

  #13
  Jun 24, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani niseme tu ukweli nimefurahia sana response zenu ni nzuri tu.
  Nitumie meseji au nipigie simu yangu iko hapo juu, bei tutaelewana (punguzo lipo) msitie shaka....
   
 14. M

  Msindima JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135

  Picha Mkuu kama wadau walivyoomba.
   
 15. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  ...Kwa Mwananyamala tunayoijua wengi wetu humu, sioni eneo ambalo linaweza kuwa na nyumba ya kupanga shilingi M 1 kwa mwezi. Pengine angalau ingekuwa vyema wakati tunasubiri utundike picha za hizo nyumba angalau ungetufahamisha ziko Mwananyamala gani na kwa sisi tutumiao usafiri wa jumuiya a.k.a daladala, nitashuka kituo gani?
   
 16. Respect

  Respect Member

  #16
  Jun 25, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zile picha za zile nyumba zetu, hizi hapa.
   

  Attached Files:

 17. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Yap mkuu nimeona vitu vyako.....wadau wa Dar kazi kwenu!
   
 18. Hebrew

  Hebrew JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2009
  Joined: Jul 3, 2008
  Messages: 509
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Mkuu Respect, hii nyumba ipo sehemu gani ya Mwananyamala?
   
 19. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #19
  Jun 25, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kiongozi Respect,
  Marketing skills zako ziko juu.
  Wanaoleta matangazo wengine hapa JF watajifunza mengi toka kwako.
  Shukurani sana.
  Kila la heri katika kutafuta wapangaji.
   
 20. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #20
  Jun 25, 2009
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,701
  Trophy Points: 280
  Wakuu,

  Mauzo ya aina YOYOTE kati ya mwanachama na mwanachama au kati ya yeyote aliyesoma tangazo la mauzo hapa JF na muuzaji kama hayatapitia kwetu kama uongozi wa JF hatutakubali lawama.

  Tangazo lolote ambalo limeidhinishwa litawekwa na Maxence, Admin, PainKiller, Silencer, Invisible au Farida.

  Tofauti na watajwa juu eleweni kuwa ni kuchukua risks katika kununua mali ya aina yoyote.

  Uongozi wa JF upo katika mchakato wa mwisho kumalizia ofisi rasmi kwa ajili ya wauzao na wanunuao ambapo matangazo yatatangazwa rasmi na uongozi baada ya kuwasiliana na wenye mali husika.

  Ni angalizo muhimu kwa wakati huu, iweni macho!

   
Loading...