Nyumba 175 zabomoka kufuatia mvua kali -Mwanza

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108
Wednesday, March 10, 2010 10:20 AM
NYUMBA zipatazo 175 zimebomoka kutokana mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha usiku wa kuamkia juzi mkoani Mwanza na watu wane wameripotiwa kufariki ka mafuriko. Kufuatia tukio hilo watu 600 wamebaki hawana makazi wakitaabika.
Waliofariki wametajwa kuwa ni Martha Samwel (25) na Yunis Peter (25) ambao ni wakazi wa Kisesa wilayani Magu, Wankuru Kilali (65) mkazi wa Kiseke na Mashauri Masasila (60)

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro, alisema watu hao kwa sasa wamehifadhiwa katika Shule ya Sekondari ya Ihushi kwenye jengo la utawala pamoja na nyumba za mwalimu
 
Back
Top Bottom