Nyumba 17 zakarabatiwa kwa gharama zinazotosha kujenga 20 zenye hadhi sawa !! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyumba 17 zakarabatiwa kwa gharama zinazotosha kujenga 20 zenye hadhi sawa !!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Jul 27, 2009.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mbunge aanika ufisadi mpya wa kutisha TANESCO

  Na Sharon Sauwa

  [​IMG]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  Ufisadi mpya na wa kutisha ndani ya Shirika la Umeme nchini TANESCO umebainika leo baada ya Mbunge mmoja kuuanika bungeni leo asubuhi.[/FONT]

  Aliyeanika ufisadi huo mpya ni Mbunge wa Sumve (CCM), Mheshimiwa Richard Ndasa, ambaye alidai kuna ubadhirifu wa zaidi ya shilingi Bilioni 1.4 ndani ya shirika hilo la umma.

  Mheshimiwa Ndasa amesema shirika hilo limetumia kiasi hicho kikubwa cha pesa (Sh. Bilioni 1.4) kwa ajili ya kukarabati nyumba 17 zilizopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam, fedha ambazo kimahesabu, zinatosha kujenga nyumba kama hizo zaidi ya 20.

  Akazitaja nyumba hizo zenye harufu kali ya ufisadi kuwa ni ni pamoja na ile iliyopo katika kiwanja namba 13 , Mtaa wa Pore, ambayo ilikarabatiwa kwa shilingi Milioni 600 na nyumba namba 89 iliyopo katika barabara ya Guinea, ambayo imekarabatiwa kwa shilingi milioni 250. Nyumba nyingine ni yenye namba 65 palepale Oysterbay iliyokarabatiwa kwa zaidi ya shilingi milioni 195.Nyingine ni nyumba namba 459 iliyopo katika Mtaa wa Mawenzi ambayo imekarabatiwa kwa zaidi ya shilingi milioni 130.

  Akasema Mheshimiwa Ndassa kuwa matumizi hayo ni mabaya na yanalitia doa zito shirika hilo. Aidha, akasema mbaya zaidi nyumba moja iliyokarabatiwa kwa zaidi ya shilingi milioni 600, hivi sasa iko mbioni kuuzwa kwa bei poa ya shilingi milioni 60 kwa kigogo mmoja.

  Mhe. Ndasa akasema cha kushangaza ni kwamba wakurugenzi wa shirika hilo, hadi sasa hawaujui ufisadi huo.

  Chanzo:
  Nipashe

   
 2. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Haa kwani Mheshimiwa Ndasa mara hii kasahaU kuwa Tanesco inaongozwa na mtuhumiwa wa ufisadi,leo ndo atabadilika au atabadilisha shirika lililobo ea kwenye ufisadi?Ndasa aha usanii nyumba nini kulinganisha na skendali kibao za Tanesco na ulikuwa kimya muda vote,umechelewa baba huna jipya
   
 3. Alwatan

  Alwatan JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Nchi kama tambara bovu, kila unaposhika pameoza...
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kabisa, tatizo ni usiri wakati tumezungukwa na less patriots with far less qualities to handle masuala muhimu kama public expenditure. Soma auditor report vizuri halafu chukua halmashauri tatu tu uzijuazo, utakuta yalioanikwa hayazidi asilimia 15%

  Na kubadilika kwa sasa haiwezekani.... Ni overhaul tu ya system nzima, angalia wamarekani wanavyohangaika na utawala bora kwetu, wakati sie wenyewe tunakula shushu!!!!

  Ukitaka kujua mengi nenda pale mission yao halafu tafuta taarifa za tarafani kwenu, zipo clear kuliko hata za katibu tarafa wa sehemu husika

  IT CAN BE DONE, LETS PLAY OUR PART AND SHOUT EVERYDAY.... HATA KELELE ZA CHURA HUONDOA HAMU YA MAJI YA KISIMA!!!!!!!!!
   
 5. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Huku tulikofika sasa mbali...nyumba inakarabatiwa millioni 600..kisha inatakiwa iuzwe kwa millioni 60......?

  Kisha tunashangaa tunapoambiwa kuwa ikifika August kutakuwa na mgawo nchi nzima au alisema watazima umeme?
   
 6. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Ni hapo ndipo nashindwa kuwaelewa hawa Wabunge wa chama tawala - shuhudia wanavyopigana vikumbo katika kuikosoa serikali lakini mwisho wa siku ndio wanaobariki hivi vitendo vya kifisadi vinavyofanywa na serikali hiyo hiyo. Wanalo rungu la kuiwajibisha serikali lakini wakitishiwa nyau hulowa kama vile wamemwagiwa maji baridi - hivi wanasukumwa na nini hasa ?

  Bilioni 1.4 kukarabati nyumba 17 ni sawa na wastani wa milioni 80 kwa kila nyumba - ni ukarabati gani huo ? Je kuna wadau wenye picha za hizi nyumba angalau tuzione zilivyokuwa kabla na baada ya ukarabati. Huu mwaka kabla ya uchaguzi tutashuhudia mengi tu - wakati serikali inadai kupiga vita uagizaji wa mashangingi, Spika wetu yuko mbioni anasubri gari la milioni 300.
   
 7. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,868
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Hizo nyumba zinakarabatiwa ili kupewa wakubwa! Ndo hivyo!

  Tutapiga kelele..ila je itasaidia???

  Tungejua hizi nyumba atapewa nani TANESCO- ni aibu!

  sasa kama Spika analipiwa 10m kodi pango..na funicha 200m za kwake ameshanunuliwa wakati mwal. mprimary anapata 150,000 kwa mwezi!

  Kwani kelele zetu zinasaidia nini?

  Kama ilivyokuwa jana, leo na kesho hali ndo itakuwa hivyo!

  Ndo Tz!!!!!
   
 8. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2009
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Nyumba hizo karibu watanunua wakubwa, sasa ni lazima ziwe katika condition nzuri . Yaani hii nchi imeoza kabisa, yaani wizi umekuwa ni part and parcel of many Tanzanian's lives. This is pathetic, no wonder Tanesco is on the verge of collapsing.
   
 9. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133

  • Sidhani kama itasaidia kumnyamazisha kwa kuwa hapo mwanzo hakusema. Tunahitaji kumpongeza hata kwa hii ndogo aliyoitoa.

  • Wizi mwingine unaofanywa katika nchi hii, hauhitaji hata elimu yoyote kuugundua, hata mtoto mdogo anaujua, cha kushangaza unabarikiwa na vikao vyote, wakaguzi, bodi na wote. Kwa kweli inatisha sana.
  • Mtu aliyeiba mali ya umma ndio husifiwa mtaani, na hupewa heshima zote.
  • Hatujachelewa tunaweza kuanza sasa, lakini si kwa kuwaachia wachache ni vita ya kwetu wote.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Jul 28, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,390
  Trophy Points: 280
  u guys are still missing the point! nani amewaambia tatizo la Tanzania au ukosefu wa fedha? Once you past that initial shock then move towards the real problem otherwise we will barking at the symptoms!
   
 11. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Napenda tu kusema, manunuzi yote ya taasisi za umma yanasimamiwa na PPRA yale yanayozidi 7.5 million, hivyo hii ilikuwa ni competitive tender , tembelea website ya PPRA for more info on how this came out to be, its better to argue with informed facts.
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi hapa cha ajabu ni nini?
   
 13. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mpita Njia!

  Uko sahihi kabisa. HAKUNA cha kushangaa hapa kama Ndasa bado anataka huo ubunge wa Sumve aachane na kumchaMua pweza. Kwani hajui ya kwamba kwa uswahiba mkubwa uliopo kati ya JMK na Dr. Idris Rashid ni lazima apatiwe nyumba Oysterbay kama wenzake!! Yeye alipostaafu mchezo wa kupeana nyumba haukuwepo.

  JMK alipomteua kutoka retirement kwa amri ya RA KULIONGOZA SHIRIKA la UMMA kitu ambacho ni kinyume cha sheria alitaka kupata nafasi ya kuhalalisha ukwapuaji wa hiyo nyumba iliyokarabatiwa kwa zaidi ya Tshs. 300m/= ili aweze kuhamia huko na baadae mkataba wake unapokwisha November auziwe kama RA hataamua kumwongezea mkataba.

  Hilo jambo liko wazi kabisa. Kama Net Group walipewa mkataba wa miaka mitatu kwa mshahara wa Tshs.20m/= kwa mwezi na hawakuruhusiwa kukaa kwenye nyumba za TANESCO iweje Dr. Rashid anayelipwa Tshs. 18m/= kwa mwezi apewe nyumba iliyowekwa Gymm kama sio mpango mkakati wa kumwuzia nae afaidi matunda ya uhuru!! Haingiii akilini kwa mtu wa mkataba kutumia kiasi hicho kukarabati nyumba ambayo ilikuwa nzuri bila ya agenda ya siri!!

  Kwa nini watalaam mahiri wanaambiwa wastaafu at 60 wakati huyu mbabaoshaji na fisadi wa rada anapeta tu .
  Richard Ndassa angemwuliza Dr. Rashid kuhusu zile Tshs. 300bn/= CONSOLIDATED LOAN kutoka mabenki ya hapa TZ amefanya nazo nini. Ndasa aache usanii staili ya CCM kuhoji 1.6bn/= na kutoulizia hayo mabilioni ambayo yakianza kulipwa yataliotumbukiza shirika kaburini ni uendawazimu tosha . The stupid young lawyer turned minister by RA anajua fika na huenda kapewa kitu as usual na aendelee kumwaga shikamoo kwa DR!!
   
 14. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Hii sio NEWS kwetu wengine.

  Tatizo la Tanzania sio Umasikini wala ukosefu wa fedha. Maliasili, nishati, maji, ardhi bora, bahari, maziwa, milima, wanyama na hata fedha tunazo.

  Tatizo Tanzania hatuna BIN Adam (sijui ni seme ma binadamu?), tuna WATU.

  Poleni sana!
   
 15. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Sioni tatizo katika hayo uliyoongea hapo juu.
   
 16. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #16
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  NI kweli mh. Lakini kuna mtu anayeweza kuzoea hizi shocks? Maana sasa zimekuwa kila kona, na ndio maana nikaomba tuweke forum ya Ufisadi.
   
 17. Mopao Josee

  Mopao Josee JF-Expert Member

  #17
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  [​IMG]KELELE HIZI TUMECHOKA KUZISIKIA,
  NAOMBA UFAFANUZI NI NANI WA KUWAWAJISHA WATUHUMIWA KAMA HAWA!!!!!!!!!!!!!!
  NA KWA NINI HATEKI ACTION?????????
   
 18. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #18
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hakika nchi inajengwa na wenye moyo na inaliwa na wenye meno.
   
 19. Tshala

  Tshala JF-Expert Member

  #19
  Jul 28, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 246
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35

  Ze newz iz zat !!!
   
 20. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #20
  Jul 28, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Watanzania wote tunalawama.wabunge wanapiga kelele halafu wananyamazishwa.wapiga kura wanalalamika uchaguzi ukifika ccm inashinda 80%.wengine wanalalama hawajiandikishi kupiga kura matokeo yake only 4mil people ndio wanavote out of potential 17mil.dawa ya mtu aliyekaa sana mdarakani ni kumtoa kwa kura.hao kina mwakyembe mbona hawatoki ccm wakaanzisha cha kwao kisicho na ufisadi?tena mwaka huu ungekuwa mzuri ili watusomeshe vizuri tuwape nchi mwakani.tatizo eti huwezi kuwa mbunge wa kweli kama hauko ccm...mbaya sana.ccm ilifanya yake mazuri kwa muda wake(1961-1991) baada ya hapo madudu tu.viko wapi kanu(kenya),unip(zambia),upc(uganda),mcp(malawi) vyote vilisahmaliza kazi zao....huku kwetu mmmh
   
Loading...