Nyumba 128 zilizouzwa kinyemela zarejeshwa serikalini

Bado kuna utata katika hili swala la nyumba. Wangetwambia ni nyumba ngapi za serikali na mashirika ya umma zilizouzwa ili tujue kama hizo zilirudishwa serikalini ni asilimia ngapi ya nyumba zilizouzwa.

Kuna uwezekano kabisa hizo 128 zilizorudishwa ni aslimia ndogo sana ya nyumba zilizouzwa. Mkapa inasemekana alinunua nyumba tatu je naye karudisha? Magufuli naye aliyevalia njuga swala la kuuza nyumba karudisha ngapi? Majina yaliyowekwa hadharani ni machache mno ukilinganisha na nyumba zilizorudishwa.

Jibu ni kweli ni asilimia ndogo, lakini hiyo ndiyo ya asilimia ya nyumba zilizouzwa kinyume na taratibu walizojiwekea...

Ikumbukwe kwamba uamuzi wa kuuza nyumba za serikali hauja-be-nullified... kilichokuwa kinapingwa ni kuuza kinyume cha utaratibu huo ulikuwa umepitishwa na baraza la mawaziri la wakati huo..

Ukisoma kwa makini kidogo, utaona kwenye post yangu yenye quote ya habari leo... ina kisehemu hiki...

Takwimu zilizowasilishwa na Waziri Kawambwa kwa Bunge zinaonyesha kuwa hadi Juni mwaka huu serikali ilikuwa imeuza nyumba 7,159 na ilikuwa imepata Sh bilioni 38.6 kutokana na mauzo hayo kati ya lengo la Sh bilioni 57.

Si vyema tukurupuka kuandika tu bila kusoma post za nyuma
 
Nyumba za serikali zote zirudishwe serikalini bila masharti yoyote. Madai ya kuuzwa kinyume cha utaratibu hayana maana, ukweli ni kuwa nyumba zote za serikali, bila kujali nyumba hizo ziko wapi, ziliuzwa kimakosa. Kama serikali ilikuwa haitaki kumiliki nyumba basi ingeuza nyumba zake zote halafu ianze kupanga. Yaani hata Ikulu nayo ingeuzwa kwa Mkapa halafu Kikwete apange!! Vile vile majengo yanayotumiwa kama ofisi za wizara na idara mbalimbali nazo zingeuzwa kabisa ili tujue moja.
 
Moja ya masharti ya ununuzi ya nyumba hizo za serikali ilikuwa kutofanya ukarabati wowote mkubwa mpaka baada ya miaka 25, sasa kama kuna aliyefanya ukarabati mkubwa atakuwa ameliwa mchana kweupe.

Ushi

Kinachonipa wasiwasi ni kauli ya waziri kuwa watalipa fidia kwa wale ambao wamefanya renovations ya hizo nyumba. Mfano nimenunua nyumba millioni 20, nikafanya renovation ya millioni 100, je serikali itanilipa milioni 120? Watajuaje renovation yangu ilikuwa ya millioni 100?
 
Zimerudishwaje? Waliouziwa wamerudishiwa fedha kiasi gani? Zile walitoa kununua au na riba na fidia ya usumbufu? Isije ikwa tunafanya biashara kichaa, kuuza nyumba kwa bei ya chee halafu kuirejesha kwa zaidi ya fedha tulizouzia.
Naona kuna mmoja kaamua kwenda mahakamani, serikali itaingia gharama kubwa katika maamuzi haya na hata uamuzi wa kurejesha nyumba hizi utakuwa na gharama kubwa sana

Mkuu ndio maana yake yaani wamenunua bei rahisi sasa hivi serikali itawafidia tena kutokana na market value na sinsi walivyo zitengeneza yaani hawa mafisadi wamekamata kila sehemu
 
Kinachonipa wasiwasi ni kauli ya waziri kuwa watalipa fidia kwa wale ambao wamefanya renovations ya hizo nyumba. Mfano nimenunua nyumba millioni 20, nikafanya renovation ya millioni 100, je serikali itanilipa milioni 120? Watajuaje renovation yangu ilikuwa ya millioni 100?
Mkuu hapo kwenye kujua thamani ya renovation inawezekana.
 
..uuzaji wenyewe ulikuwa makajanja.

..sasa katika kuzirejesha watalipa market value ya nyumba na kiwanja au???
Ndio mkuu, huwezi kutenganisha nyumba na kiwanja. Na kiwanja huwa kinapanda bei tu hakishuki....tafakari toka miaka hiyo
 
Je, Nyumba alizonunua fisadi Mkapa nazo zimerudishwa? Wekeni hizo address za hizo nyumba ili tufanye uhakiki kama hii habari ina ukweli maana hii serikali haiaminiki hata kidogo.

Date::8/29/2008
Nyumba 128 zilizouzwa kinyemela zarejeshwa serikalini
Tausi Mbowe, Dodoma
Mwananchi

SERIKALI imezirejesha nyumba zake 128 zilizouzwa kwa watu mbalimbali kinyume cha utaratibu na kwa watu ambao hawakuwa watumishi wa umma zikiwemo zilizopo kwenye maeneo maeneo nyeti nchini kote.

Hatua hiyo ilitangazwa bungeni na Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa jana na kusema kuwa nyumba hizo zinarudishwa serikalini na wahusuika kurudishiwa fedha zao.

Miongoni mwa nyumba zilizorejeshwa serikalini ni ya aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Raia, Harith Bakari Mwapachu na za viogogo wengine akiwamo Jaji Stephen Ihema na Balozi Adam Marwa ambao waliuziwa nyumba za Halmashauri ya Kinondoni.

Waziri Kawambwa, alisema, wakati wa utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete kwamba nyumba zote za serikali zilizouzwa kinyume cha utaratibu zirejeshwe.

Dk Kwambwa alitaja makundi hayo kuwa ni pamoja na nyumba zilizopo katika makambi, nyumba

ziliozouzwa kwa watumishi binafsi ambao si watumishi wa serikali na watumishi wa umma na nyumba zaidi ya moja zilizouzwa kwa familia moja ya watumishi wa umma.

Nyigine ni nyumba za taasisi mbalimbali zilizouzwa kwa watumishi wa serikali kuu na zilizoko katika maeneo nyeti ya serikali na ambazo ziliuzwa kwa watumishi wa umma.

Waziri Kawambwa alisema, nyumba 52 zilizopo katika makambi ziliuzwa kwa makosa, idadi hiyo ikihusisha nyumba nane zilizoko katika maeneo ya makambi ya polisi, nyumba 10 za maeneo ya Magereza na nyumba 34 katika maeneo ya Hospitali.

Alisema wahusika wote wameandikiwa barua ya kusitisha mikataba na kuwataka wasiziendeleze kuzikarabati kwa kuwa serikali inafanya utaratibu wa
kukagua na kutathmini maendelezo yaliyofanywa na wahusika ili kupata thamani halisi kwa ajili ya kuwafidia .

Alisema wakati wa kuuza nyumba za serikali pia ilibainika kuwa nyumba nne ziliuzwa kimakosa kwa watu ambao si watumishi wa serikali jijini Dar es Salaam, baada ya wahusika kutoa taarifa zisizokuwa sahihi.

“Katika hatua za kurekebisha kasoro hiyo, serikali imefuta mikataba yote ya mauzo ya nyumba hizo na nyumba tatu kati ya nne tayari zimerejeshwa kwenye miliki ya serikali na nyumba moja iliyobaki, muhusika amefungua kesi Mahakama Rufaa ya ardhi,” alisema.

Alisema kasoro nyingine iliyojitokeza wakati wa zoezi hilo ni baadhi ya familia na watumishi wa umma waliuziwa nyumba zaidi ya moja na kwamba uchunguzi uliofanywa na serikali umebaini kuwa kuna familia sita na watumishi wanne waliuziwa nyumba zaidi ya moja.

Alisema kati ya familia sita zilizouziwa nyumba zaidi ya moja, tano zimerudisha nyumba tano na kubakiwa na nyumba tano badala ya 10 kama ilivyokuwa awali na kwa upande wa watumishi wanne serikali imetoa muda hadi Septemba 15 mwaka huu kwa wahusika kurejesha nyumba za ziada na kubakiwa na nyumba moja.

Alisema pia serikali iligundua kuwa nyumba 27 zilizokuwa za serikali kuu ziliuzwa kwa watumishi wa umma, nyumba hizo ni pamoja na na nyumba 21 za serikali za mitaa, nyumba mbili za Shirika la Viwanda vidogo (Sido), nyumba moja ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na nyumba tatu za Shirika la Nyumba la Taifa.

Waziri Kawambwa alisema jumla ya nyumba 35 zilizouzwa zipo katika maeneo nyeti ya serikali na ambazo hazikupaswa kuuzwa kutokana na unyeti wa kazi za watumishi wanaostahili kuzitumia.

Alisema serikali kupitia Wizara yake imeorodhesha nyumba za namna hiyo na waliouziwa wote wameandikiwa barua za kusitisha mikataba yao ili kuzirejesha nyumba hzio kwa matumizi ya serikali kwa mantiki hiyo numba za namna hiyo hazitauzwa tena.

Katika zoezi hilo la uuzwaji wa nyumba jumla ya Sh bilioni 38.69 zilikusanywa katika kipindi cha miaka mitano hadi mwezi Juni mwaka huu kati y ash bilioni 57.05 ikiwa ni sawa na asilimia 67.81 zinazotarajiwa kukusanywa katika kipindi cha miaka kumi kutokana na mauzo ya nyumba 7,159.

Azimio hilo la Bunge linafuatia hoja binafsi ya uuzwaji wa nyumba za serikali iliyowasilishwa bungeni katika mkutano wake 11 uliofanyika Aprili mwaka huu na Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro.
2008
 
Takwimu zilizowasilishwa na Waziri Kawambwa kwa Bunge zinaonyesha kuwa hadi Juni mwaka huu serikali ilikuwa imeuza nyumba 7,159 na ilikuwa imepata Sh bilioni 38.6 kutokana na mauzo hayo kati ya lengo la Sh bilioni 57.

Kasheshe,

..umesoma kwa makini hiyo taarifa uliyonukuu?

..umesahau ku-highlight kwamba lengo lilikuwa kupata Bilioni 57 lakini serikali ikapata Billion 38.6.

..maana yake ni kwamba kuna hasara mbili. kwanza kuuza kwa bei ya kutupa, halafu kuna hasara ya Billioni 18.3 ya kutokufikia lengo.

..hivi hili siyo JIPU kweli? huu siyo UFISADI na UHUJUMU UCHUMI?

cc The Boss, MsemajiUkweli, Ritz, Remote, chew, Nguruvi3, Bukyanagandi
 
Back
Top Bottom