Nyuma yako (Riwaya ya S. Mollel)

Riwaya za steve hasa za kijasusi huwa hazikamiliki ukiondoa ANGA LA WASHENZI zinazobakia huwa ni magumashi tu.

Ni bora aachane na uandishi wa riwaya kama yupo bize na shughuli zingine.
 
*NYUMA YAKO --- 31*

*Simulizi za series*

ILIPOISHIA

Kidogo kukawa kimya. Walitazamana kwa kama sekunde tano alafu yule jamaa akamgusa mlinzi wake mmoja kwa kiwiko, hapa nikawa ‘attention’ zaidi, mlinzi huyo akatoa mkebe na kuuweka mezani, ulikuwa umejawa na pesa.

Yule bwana akamwambia meneja atazame hizo pesa na yeye yupo radhi kumwachia kama watakubaliana. Bado meneja akashikilia msimamo wake. Mara hii akabamiza meza kwanguvu akiwa anafoka.

“Sirudii nilichosema, Lorenzo!”

Hapa nikaona mlinzi mmoja aliyekuwa ameambatana na yule jamaa akichomoa kitu nyuma ya kiuno chake.

ENDELEA

Nikawa ‘attention’ zaidi. Nadhani mlinzi yule hakuwa anadhani kama anaonekana. Mwangu ulikuwa ni hafifu, taa za klabu zikikatiza na kujiendea lakini kwangu bado hazikunifanya nisione kinachoendelea.

Nilimwona vema bwana yule na kwasababu za kiusalama, lile lilikuwa tishio la uhai. Haikuhitaji ujuzi mkubwa sana kubaini kwamba maongezi kati ya meneja na yule bwana, yani Lorenzo yalikuwa yanaenda kukomea kwenye kushurutishana ama kumwaga damu.

Basi kwa upesi, nikatengua kiti cha meneja na kukibeuzia kwnagu, alafu kwa wepesi wa ajabu nikamvuta meneja na kumweka nyuma yangu kisha nikakita teke kile kiti alichokuwa amekalia meneja, kiti kikaserereka kidogo tu kabla hakijanyanyuka kabisa na kuwavamia wale wajamaa wote kwa mkupuo!

Kwa haraka kabisa nikamtemngua miguu meneja kumlaza chini. Nilifanya hivyo kwasababu ya usalama wake ‘in case’ wale jamaa wakianza kufyatua risasi.

Baada ya kufanya vivyo, nikarusha macho yangu kuwatazama maadui, wanaume wawili walikuwa wamechomoa na kushikilia bunduki. Kama nisingelifanya maamuzi ya haraka basi ilikuwa bayana ningepoteza maisha yangu na ya meneja pia.

Ni upesi, ninaposema upesi namaanisha upesi haswa. Sikuwa nafahamu ni kwanini akili yangu ilikuwa inafanya kazi haraka ndani ya sekunde. Na kama haitoshi mwili wangu ukipokea maelekezo ya akili yangu na kuyafanyia kazi. Yote haya ni kwakuwa nilipoteza kumbukumbu zangu.

Laiti ningelikuwa najua kuwa mimi ni afisa wa CIA, nisingalishangazwa na uwezo wangu huo.

Nilibinua meza iliyokuwa hapo uwanjani, meza iliyokuwa inatumikia kwa ajili ya maongezi, kwa kuisigina tu na uzito wa guu langu alafu nikaidaka meza hiyo na kujikinga nayo. Risasi kama nne zikatupwa. Ni kheri meza ile ilikuwa ngumu sana, haikupenyeza ncha yoyote ya risasi.

Haraka nikawasogelea wale maadui nikiwa na nilipowakaribia nikawatupia meza ile kwanguvu. Upumbavu wakaidaka. Nisijiulize mara mbili nikajitupa juu na kuachanisha mapaja yangu nikituma teke la haja, likakita meza na kuwatupia kando! Bunduki pembeni.

Wanakuja kuamka, tayari nimewaweka chini ya ulinzi. Punde wakafika na walinzi wengine wa klabu kuja kuhakikisha usalama. Wakakuta mambo yote yapo ndani ya kiganja.

Wakawatia kambani maadui wale na kwa maelekezo ya meneja wakawamaliza kwa kuwamiminia risasi isipokuwa bwana Lorenzo peke yake.

“Namhitaji akiwa hai,” alisema meneja akijifuta jasho kwa leso yake ya pamba. Wale waliouawa ikatoka agizo wakatupiwe baharini.

“Well well well, bwana Lorenzo, ni nini ulikuwa unataka kufanya?” akauliza meneja akiwa anamtazama Lorenzo aliyekuwa amejawa na shaka kiasi. Macho yake alikuwa ameyakaza lakini ukiyatazama vema kwa ndani alikuwa na hofu.

“G, tufanye yameisha sawa?” akasema Lorenzo. “Umeshapata pesa zako, nadhani tumemalizana.”

“Tumemalizana?” akastaajabu meneja. “Tunamalizanaje na ulikuwa umekuja hapa kunipora? Deni langu halikukutosha Lorenzo, sio?”

Nikamtazama Lorenzo. Hakusema jambo. Meneja akasimama na kumshika nywele zake kwanguvu, “sikia! Utalipa kwa haya uliyoyafanya. Utalipa mara tatu zaidi, Lorenzo. Umenisikia? Sidhani kama ungetaka habari hizi zimifikie Don Cartel.”

Nikamtazama zaidi bwana Lorenzo, kwa namna fulani alikuwa kama mtu aliyekosa cha kusema kwa kuchanganyikiwa. Hakuwa sawa.

Baada ya kama nusu saa meneja akaachana naye akimuhifadhi kwenye chumba cha chini kisha akaniita na kuwa na maongezi machache pamoja naye.

“Tarrus, leo umefanya kazi nzuri sana. Umenifurahisha hakika. Sasa niambie ni kiasi unataka nawe ukafurahie leo.”

“Usijali, mkuu,” nikamtoa hofu. “Nilikuwa natimiza kazi yangu tu.”

“Najua hilo, kwani kuna ubaya endapo nikakupatia zawadi?” akaniuliza akiwa anafungua ule mkebe wa Lorenzo. Mkebe uliokuwa umejawa na pesa.

“Chochote utakachonipatia nitashukuru,” nikamwambia na kuongezea, “maana ni nje ya ujira wangu.”

Sikufahamu ni kiasi gani alikitoa kwa ule muda. Alinipatia vufurushi viwili vya pesa na kuniambia nikatumie nitakavyo, na kama haitoshi akaniambia nimchukue mwanamke moja wa kwenda kulala naye siku hiyo.

“Hapana, inatosha hiki ulichonipa,” nikashukuru nikitabasamu kwa mbali.

“Kweli?”

“Yah! Inanitosha sana tu.”

Akan’tazama kwa sekunde tatu kisha akatikisa kichwa chake na kuniruhusu niende zangu. Nikahifadhi pesa nilizopewa na kisha nikaendelea na majukumu yangu ya kila siku.

Nilipofika ukumbini wenzangu walinipongeza sana kwa kazi niliyofanya. Niliona kila mtu akinitazama kwa tabasamu na kunipatia ishara ya pongezi. Nilikuwa maarufu ghafla hata kwa baadhi ya wateja.

Lakini nilifahamu wazi swala lile halikumpendeza Mike na wenzake wawili. Walin’tazama kwa macho makavu yaliyojawa na husda.

Sikuwajali.

Asubuhi na mapema nikarudi nyumbani na siku hiyohiyo ndipo tukahama na Katie kwenda kwenye makazi mapya yaliyokuwa bora zaidi. Kila mtu alikuwa na furaha sana. Samani zilikuwa za kupendeza na hata mandhari.

“Sikutaraji kabisa!” alisema Katie akiwa amewekea viganja vyake mashavuni kwa mshangao. Alinikumbatia mara kadha wa kadha. Sikuwahi kumwona akiwa na furaha kiasi kile.

Baada ya kula na kuongea kidogo, nikapumzisha mwili kwajili ya kupata nguvu ya kutenda kazi baadae, lakini nikiwa katikati ya mapumziko yangu hayo, nikahisi mtu akinijongea karibu. Kidogo nikahisi kiganja cha mtu kikinipapasa mgongoni.

Kikipanda juu mpaka kushuka chini karibia na kiuno. Nilipofungua macho yangu kuangaza, nikamwona Katie. Alikuwa amevalia ‘top’ nyepesi ya kulalia ambayo ilisadifu kifua chake ambacho hakikuwa haba.

Macho yake yalikuwa yamelegea na mdomo wake ameuweka wazi kana kwamba amebanwa na mafua.

Hakusema jambo. Nami sikusema jambo. Tulitazamana macho yetu yakisema kila kitu. Sikujua nini kilitokea, nilijikuta nipo mdomoni mwa Katie huku nikiwa nimeuficha mwili wake kwenye mikono yangu mipana.

Alinibusu kwa ustadi na kunishika kiutaalamu. Huwezi amini hatukuongea mpaka lilipotimia lisaa limoja na nusu tena mimi na yeye tukiwa tunatazama kwa macho yaliyo hoi.

“Ilikuwa ni ndoto yangu, Tarrus,” alisema kwa sauti ya puani.

“Kwanini haukuwahi kusema?” nikamuuliza.

“Hauoni kama matendo yanaongea mengi?” akasema kisha akatabasamu na kunibusu, baada ya hapo tukapumzika kwa pamoja mpaka pale nilipokuja kuamka saa mbili usiku. Ulikuwa ni muda sahihi wa mimi kujiandaa kwenda kazini.

Nikamuaga Katie lakini kabla sijaondoka akanitaka nimbusu na kumkumbatia. Nikafanya vivyo na kisha nikaenda zangu. Sikujua kwanini ila siku hiyo nilijihisi mwenye furaha sana.

**
 
*NYUMA YAKO --- MWISHO WA MSIMU WA KWANZA*

*Simulizi za series*

ILIPOISHIA

“Hauoni kama matendo yanaongea mengi?” akasema kisha akatabasamu na kunibusu, baada ya hapo tukapumzika kwa pamoja mpaka pale nilipokuja kuamka saa mbili usiku. Ulikuwa ni muda sahihi wa mimi kujiandaa kwenda kazini.

Nikamuaga Katie lakini kabla sijaondoka akanitaka nimbusu na kumkumbatia. Nikafanya vivyo na kisha nikaenda zangu. Sikujua kwanini ila siku hiyo nilijihisi mwenye furaha sana.

ENDELEA

Nilipofika kazini nikaendelea na majukumu yangu kidogo nikaitwa na meneja ofisini kwake. Alikuwako na wanaume wawili. Aliniambia nimngoje kwa muda kidogo nje ya mlango, na kweli kama baada ya dakika sita, akatoka na kuniambia niongozane naye kwenda kwenye gari. Alikuwa pamoja na wanaume wale wawili.

Tukafika kwenye gari, mimi nikaketi nyuma pamoja na mwanaume mmoja, na kule mbele akaketi meneja na jamaa mwingine. Tukatembea kwenye gari kwa kama lisaa hivi tukikomea kwenye jengo la ghorofa chache. Hapo tukashuka na kuzama ndani.

Humo palikuwa patulivu sana. Sakafu ya chini haikuwa na watu, nadhani japo sikuwa na uhakika. Mwanga wake ulikuwa ni hafifu rangi ya bluu. Sakafu ya pili ilikuwa na watu kadhaa waliokuwa wamesimama kiulinzi.

Sakafu ya tatu kulikuwa kumechangamka. Muziki ulikuwa unapigwa na watu kadhaa, kama vile ishirini na tano, wanaume wachache na wanawake wengi, wakicheza hapo taratibu.

Nilijaribu kwa kadiri ya uwezo wangu kukagua mazingira yale kila nilipopata nafasi. Tukaendelea kusonga na kuja kukomea kwenye sakafu ya nne na ya mwisho. Hapo kulikuwapo na uwanja wenye ukubwa wa wastani, meza kubwa pamoja na wanaume wanne waliokuwa wameketi.

Mwanga wake haukuwa mkali sana wala uliopooza. Ungeweza kumwona kama ungemtilia maanani.

Meneja akasalimiana na wale wenyeji kisha akaketi. Punde kidogo wakawa wanaongelea kuhusu biashara yao ya madawa. Sikuwa napenda kazi hii lakini sikuwa na budi. Nikiwa hapa nikawa nawaza zangu kichwani nifanye namna ya kujipatia pesa za kutosha na kisha nikaendelee na maisha yangu mengine.

Nikiwa hapo nawaza vivyo, nikabaini kuna mmoja wa wale wenyeji alikuwa akin’tazama sana. Nilipomtazama mtu huyo akaondoa uso wake kwa haraka toka kwangu ila tangia hapo nikawa nimemweka kwenye mazingatio.

Nilimtazama na kujiuliza pasipo majibu mpaka pale tulipomaliza kilichotuleta na kurudi kwenye gari. Tuliwaacha watu wale wawili njiani alafu mimi na meneja tukaongozana mpaka kule klabuni.

Nikamfikisha meneja kwenye ofisi yake lakini nilipotaka kuondoka, akaniita kwa sauti ya wastani na kuniagiza nivue shati langu. Sikuelewa ni nini anamaanisha japo sikumuuliza. Nikavua shati na kumtazama.

“Vua na suruali,” akaniagiza tena akipandisha kichwa chake. Hapo nikasita kidogo. Nikamtazama meneja kwa macho ya maulizo pasipo kusema jambo. Akarudia agizo lake. “Vua suruali, Tarrus. Unadhani mimi shoga?”

Basi nikavua suruali na yeye akasimama kunijongea. Akanitazama mguu wangu mpaka mapajani na kukomea kiunoni, kisha akan’taka nijiveshe nguo zangu na nisimame kumtazama. Nikafanya vivyo.

“Tarrus,” akaniita na kuniuliza, “Una hakika wewe ni mwaminifu kwangu?”

Kabla sijafikiria vizuri, nikamjibu, “Ndio, nina uhakika.”

Akawasha sigara yake na kuvuta pafu moja tu, alafu akasema kuhusu kile alichotoka kunifanyia ya kwamba alikuwa anataka kuhakiki kama kile alichokisikia kuhusu mimi ni kweli ama lah.

“Kitu gani hicho?” nikamuuliza kwa hamu.

“Usijali, kaendelee na kazi yako,” alisema akin’tupia mkono kwenye mwelekeo wa mlango. Punde kidogo simu ya mezani ikaita. Nikamtazama kwa muda mfupi na kisha nikajiondokea nikisonga taratibu.

Nikaurudishia mlango wa ofisi lakini kabla sijauacha kwa mbali, nikapata wazo la kuskiza kile ambacho meneja atakuwa anaongea simuni.

Nikasonga mlangoni na kuweka sikio.

“ … Najua cha kufanya … hapana! Sikia, sikia … sikia, najua nini nifanye na kwa muda gani, sawa? …” aliposema hayo akaibamiza simu mezani. Mimi sikukaa tena nikaondoka zangu kushuka chini.

Nikiwa naendelea na kufanya kazi yangu, nikawa nawaza sana juu ya ile safari ya meneja na ukaguzi wake. Nilihisi kuna kitu hakipo sawa. Niliwaza sana na mwishowe nikaamua kupuuzia nisije kujiumiza kichwa.

Kwenye majira ya saa tisa nikaonana na Jolene na kumuulizia hali yake. Alikuwa anendelea vema japo bado hakuwa amerudi kwenye majukumu yake. Alinishukuru tena kwa kunikumbatia na kunibusu.

“Nina zawadi yako, Tarrus,” alisema akin’tazama kwa macho ya furaha.

“Zawadi gani hiyo? Mbona haukun’letea mpaka nije?”

“Nilipanga kukupatia lakini kwasababu umekuja mwenyewe, sina budi kukupa,” alisema akitabasamu. Nami nikanyamaza nikingoja zawadi hiyo.

Punde nikamwona akirejea na chupa kubwa nyeupe yenye kileo cha vodka, akasema, “Ona nimekuletea mpenzi mkubwa kabisa. Natumai utakuwa na wakati mzuri sana pamoja naye!”

Nikatabasamu na kumweleza kuwa mimi si mnywaji. Akastaajabu, “Alah! Bwana Tarrus wewe ni mtu wa aina gani? Haunywi wala haupendi wanawake?”

Nikatabasamu na kumuuliza, “Nani kakuambia sipendi wanawake?”

Akaguna. “Kwani hilo ni mpaka useme, si laonekana tu? … sikia,” akasonga karibu na mimi na kusema, “tangu nifanye kazi hapa hakuna mwanaume ambaye hajawahi kunitaka, isipokuwa wewe. Najisogeza na kujipendekeza lakini haushtuki! Ajabu.”

Nikatabasamu nisiseme jambo. Akan’tazama kwa jicho la pembeni na kuniuliza taratibu, “Tarrus, wewe ni shoga? Siulizi kwa ubaya wala kukuvunjia heshima. Nataka tu kujua.”

Kabla sijajibu nikafikiria hilo neno alilosema nalikuwa nakutana nalo kwa mara ya pili sasa katika siku moja ndani ya masaa machache. Sikuonyesha kukasirika nikamjibu kuwa mimi si shoga na wala sina hisia hizo.

Basi akanilazimu sana nipokee zawadi yake kwani hakuwa na kitu kingine zaidi ya kile. Alin’tazama kwa macho ya huruma kana kwamba mtoto anaomba peremende. Nami nilipomtazama kwa muda kidogo nikaguswa naye, sikuona haja ya kumvunja moyo.

“Sawa, nitaichukua.”

Akafurahi sana. Saa kumi na moja ilipowasili nikaibeba chupa hiyo na kurudi nayo nyumbani.

“Katie, ona nilichokuja nacho!” nilipaza baada ya salamu. Nikatoa chupa ile kubwa ya vodka na kumwonyeshea nikiwa natabasamu.

“Wow!” akakodoa macho akisonga upesi. “Leo tutakuwa na tafrija eenh?”

“Nadhani,” nikamjibu na kumuuliza, “Utakunywa?”

“Kwanini nisinywe!” akajibu upesi. Sidhani kama alilifikiria swali langu, ila baada ya muda kidogo akan’tazama kama mtu aliyejishtukia na jibu lake, akaniuliza kwa sauti ya chini, “Wewe je? Utakunywa?”

“Nitakunywa nawe,” nikamjibu akafurahi. Basi nikala na kupumzika kidogo alafu baadae Katie akanipatia kile kinywaji akiwa amechanganya na juisi ya matunda aliyotengeneza kwa mkono wake.

Tukanywa sana na mwishowe tukaishia kujitupia kitandani na kufanya mapenzi yasiyokuwa na mwisho.

Kwa ulevi wangu nikapitiliza mpaka muda wa kazi. Nilikuja kuamka majira ya saa sita usiku, napo kichwa kikiwa kinanigonga sana. Nikajitahisi kunywa maji mengi na kisha nikarudi tena kitandani. Nilikuwa sijiwezi.

Asubuhi tulipoamka nikamweleza Katie yale yote yaliyon’tokea. Akacheka sana na kuniambia namna ya kufanya endapo siku nyingine ikinitokea hali kama hiyo.

“Hakutakuwa na siku nyingine, Katie!” nikamwambia nikitikisa kichwa. “Sitakunywa tena mimi. Si kwa mateso yale.”

Basi nikatumia siku nzima kuwa naye mpaka usiku muda wa kwenda kazini. Nilipofika na kusalimu wenzangu ndipo nikapashwa habari kuwa usiku wa jana yake walikuja wanaume wawili kuniulizia.

Kwa mujibu wa taarifa, wanaume hao hawakuketi baada ya kuambiwa sipo, na wala hawakuaga.

“Walikuwa wanaonekanaje?” nikauliza. Wakanielezea lakini nisiambulie kitu. Hakuna niliyekuwa namfahamu.

Nikiwa najiuliza, nikaletewa ujumbe kwamba nahitajika ofisini kwa meneja.

***
 
*NYUMA YAKO (MSIMU WA PILI) --- 01*

Nilipofik nilimkuta meneja akiwa ametulia sana. Bila shaka alikuwa ametingwa na mawazo. Alikuwa mwenyewe ofisini na pakiwa kimya.

Nikaketi na kumsalimu. Kabla hajanijibu akatazama saa yake kwanza ndipo akauliza, “Tarrus, mbona jana hukuja kazini?”

Nikajiuma nikimweleza nini kilitokea. Nilihofia kumwambia kama nililewa na kuzidiwa hivyo nikamwongopea kuwa hali yangu haikuwa sawa kiafya. Akan’tazama kwa muda kidogo alafu akaniuliza, “Ulijua kama utakuja kutafutwa?”

Swali lake likansh’tua kidogo. Kabla sijazungumza nikafikiri kwa sekunde kama nne kisha nikasema, “unaongelea nini?”

“Unajua ninachoongelea, Tarrus?” Meneja akasema akin’kazia macho. “Jana kuna watu walifika hapa kukuulizia. Unawafahamu?”

“Hapana!” nikamjibu na kuongezea, “nimeambiwa na kuelezewa lakini sijapata kuwafahamu.”

Bai meneja akageukia zile video zake za kamera alafu akabonyeza mara tatu na mara video za jana zikajirejea na kucheza. “Tazama,” akaniambia.

Nikasogea na kutazama. Nikapata kuwaona wanaume wawili waliokuwa wamevalia kofia wakiongea na walinzi. Meneja akasimamisha video hiyo na kuivuta kwa ukaribu. Nikatumbua macho yangu kuangaza.

“Siwafahamu,” nikasema baada ya kujiridhisha na kile nilichokiona.

“Una uhakika?” meneja akauliza.

“Ndio, nina uhakika. Siwafahamu kabisa!”

Meneja akan’tazama na kushusha pumzi ndefu.

“Tarrus, unajijua wewe ni nani?”

“Kwani kuna nini meneja?” ikanibidi nimuulize. Sikuwa namwelewa ni nini kipo kichwani mwake.

“Tarrus, sitaki kuongea sana nawe lakini nakusihi uwe makini sana. Kuna vitu havipo sawa, utapata kuvijua kadiri na muda. Waweza kuendelea na kazi yako.”

“Meneja, nadhani itakuwa vema ukiniambia nini tatizo ili nijue namna gani ya kujitazama.”

“Tatizo lipo kwako Tarrus. Si umeona hao watu wamekuja kukutafuta wewe? Vipi kama ni wanausalama? Vipi kama ni watu wanaokujua, huoni itakuwa hatari ukilinganisha unajua vitu vingi kunihusu?”

“Na mbona uliniuliza kama najijua? Niambie tafadhali ni nini unajua kuhusu mimi?”

“Hakuna kipya Tarrus. Hakuna lolote ninalolijua na ndiyo maana nakuuliza wewe. Kama kuna jambo unadhani napaswa kujua basi nijuze.”

Sikuwa na cha kumwambia hivyo nikajiondokea nikiwa na mawazo yangu. Nikafanya kazi muda wot nikiwa nawaza sana juu ya watu wale waliokuja kun’tembelea lakini pia lile ambalo meneja analo kichwani.

Mpakayanafika majira ya saa kumi ndipo nilipopata ahueni baada ya Jolene kunifuata na kunipigiha soga za hapa na pale. Dhumuni lake kubwa lilikuwa ni kujua kama nilikunywa ile zawadi yake.

Akiwa anan’tazama kwa kukejeli akaniambia, “kuwa mkweli Tarrus, ndiyo maana jana ulishindwa kuja kazini, sio?”

“Hapana,” nikajibu lakini kwa uso usiomaaniha. “Yalikuwa ni mambo yangu binafsi tu.”

Jolene akatabasamu. “Usijali, sitasema siri yako. Ni yetu yote. Najua namna gani kinywaji kile kilivyo na nguvu. Najua kitakuwa kilikupelekesha, sivyo?”

Sikusema kitu. Akaniwekea mkono wake begani na kusema. “Pole sana. Ilikupasa unywe glasi moja tu.”

“Sitakunywa hata tone siku nyingine,” nikamwambia vivyo nikitikisa kichwa. “Itakuwa ni mwanzo na mwisho wangu, Jolene. Ulifikiria nini mpaka kumipa kinywaji kile?”

Akapaliwa na kicheko. “Tarrus, unan’shangaza haswa! Mimi huwa nakunywa mpaka chumba mbili na nikaendelea na ratiba yangu. Mbona una kichwa cha mtoto mdogo?”

“Jolene, si kila kitu naweza sawa?”

“Naona ni kweli. Wajua kupambana na wanaume wakubwa wenye nguvu ila chupa moja yakulaza chali! Ni hatari.” akaagua tena kicheko. Sasa alikuwa ananikejeli. Kwa muda kidogo nikataniana naye mpaka pale alipokuja kubadili mada na kuniambia kuhusu wanaume wale waliokuja kuniulizia.

“Hawakuonekana kama watu marafiki. Wanasema kwamba waliishia mlangoni ila hapana, kuna mtu alikuwapo ndani, pengine walitengana ila walikuwa wanafanana kwa mienendo.”

“Walikuaje?” nikamdadisi.

“Wakati ananifuata nilidhani ni mteja lakini kwa namna alivyokuwa ananitazama, kwa muda kidogo, nikajua si mtu mwema. Alinifuata na kunisalimu akilazimisha kutabasamu, alafu akaniuliza kuhusu wewe. Mwanzo aliniambia jina la Marshall na alipoona sina taarifa kuhusu hilo akanieleza kuhusu mwonekano wako.”

“Hakukuambia anataka nini?” nikawahi kumuuliza.

“Hapana,” akanijibu akipandisha bega moja. “alichokuwa anataka ni kujua tu wapi ulipo. Hakuketi sana akapotelea miongoni mwa watu.”

Baada ya maongezi hayo na Jolene, nikaendelea na kazi yangu mpaka majira ya saa kumi na moja nilipotoka kazini na kwenda nyumbani.

Nilipofika nikakukuta ni kimya sana. Niliita jina la Katie pasipo mafanikio na ingali natazama nikaona karatasi nyeupe mezani. Nikaijongea na kuitazama.

‘Hellow Marshall, tunaye Katie,’ Ujumbe uliandikwa kwenye karatasi. Na niliposoma mpaka hapo ikatosha kabisa kukimbiza moyo wangu. Nilihisi tetemeko fulani la ajabu likinipitia mwilini na macho yakinitoka kidogo kutumbua.

‘Kama utakuwa unamhitaji basi utamfuata …’ wakaweka anwani hapo na kisha onyo kwamba niende mwenyewe tu!

Nikaiweka karatasi mezani nikiwa nimejawa na hofu sana. Kichwa changu kilikuwa kimejawa na mawazo na kuchanganyikiwa kwa wakati mmoja. Nilijihisi msukumo mkubwa wa damu. Nikaona nikae chini kwanza na kupata maji nipate kutuliza nafsi.

Nilipoweka glasi ya maji chini nikaenda kupekua mahali ninapoweka pesa zangu, nikazikuta. Kila kitu kilikuwa sawa, hakuna kilichopotea isipokuwa Katie peke yake.

Nikachukua kiasi cha pesa na kukitia mfukoni na alafu kabla sijaenda huko kumkuta Katie nikaona ni kheri nipitie kule kazini nichukue silaha kadhaa za kunisaidia. Nilichukua bunduki moja kwa kuiba na kisha pasipo kuaga nikaondoka zangu huko.

Nilisonga mpaka kwenye anwani elekezi, na kabla sijaingia humo nikakagua eneo hilo kwa undani nikifahamu milango madirisha na njia.

Nilipojiridhisha nikasonga eneoni nikiwa nimechopeka silaha yangu kwenye kiatu, nyuma ya kisigino.

Nilipofika mlangoni nikamkuta mwanaume mmoja aliyevalia ‘casual’, aliponiona nikiwa nakuja alibinyia ‘microphone’ yake sikioni na kuongea maneno kadhaa. Sikuweza kusikia maana nilikuwa mbali.

Nilipomkaribia, pasipo kuniongelesha, akafungua lango na kunielekezea ndani ya ishara ya kichwa.

Ndani kulikuwa kukubwa kukiwa kumejawa na bustani. Wanaume watatu walikuwa wamesimama kiulinzi, macho wameyafunika kwa miwani na masikio yao yamezibwa na ‘microphone’.

Hawakuongea na mimi bali wakin’tazama kwa umakini. Mikono yao walikuwa wameifumbata mbele ya sehemu zao za siri.

Nilipojongea zaidi, mmoja ambaye alikuwa mbele kabisa ya mlango, akapiga hatua kuuendea mlango na kisha akaufungua kunikaribisha humo. Nami pasipo kuuliza wala kuongea nao, nikasonga ndani humo na kumkuta mwanaume mmoja mwenye makamo ya miaka arobaini.

Mwanaume huyo alikuwa amevalia suti na kulaza vema nywele zake. Alikuwa amekunja nne akin’tazama kwa uso ulioficha hisia. Nilipomkaribia akatabasamu na kusema, “Karibu, uketi bwana Marshall.”

Nikamkosoa kwa kumwambia, “Naitwa Tarrus.”

Akatabasamu zaidi.

***
 
*NYUMA YAKO (MSIMU WA PILI) --- 02*

Nilipomtazama ndipo nikamwona mwanaume mwenye macho madogo ya paka. Lips nyembamba na kidevu kilichochongoka kana kwamba kiwiko. Masikio yake yalikuwa makubwa na hata ukitazama kwa wepesi waweza kuona yalikuwa na nywele ndaniye.

Kitu hiko kilin’shangaza kidogo kwani sikuona kama umri wake unasadifu yeye kuanza kuchomoza nywele masikioni. Lakini sikuwa na muda wa kuwaza sana kwani nalikuwapo eneo hatari. Na huyo aliyekuwa amekaa mbele yangu sikuwa namtambua kwa namna yoyote ile.

Kitu pekee ambacho nilikuwa na uhakika nacho ni kwamba anahusika na kumhifadhi Katie. Katie aliyenifanya niwapo hapo.

“Habari yako kijana? Naitwa Rodney Rufus. Karibu sana,” alisema bwana huyo akin’tazama kwa macho ya kirafiki.

“Nashukuru kwa kukufahamu, bwana Rodney. Unaweza kuniambia kwanini unanitakia nini tafadhali? Na kama kulikuwa na haja ya wewe kumteka mtu asiye na hatia?”

Akasafisha koo lake na kutazama chini.

“Bwana Marshall --”

“Naitwa Tarrus!”

“Unaitwa Marshall - Anthony Marshall,” bwana yule akasema akinikazia macho. “Kama hutojali, waweza kuniruhusu nijitambulishe kwako. Nilidhani utakuwa unanikumbuka hata kwa kuniona,” aliposema hivyo akan’tazama kwa maswali, “Vipi kwani wanikumbuka?”

Nikabinua mdomo wangu na kutikisa kichwa. Sikutia neno.

“Sawa, kama nilivyokuambia hapo awali naitwa Rodney Rufus. Mimi ni afisa wa shirika la ujasusi la Marekani, CIA. Nipo hapa Ujerumani kwa ajili yako.”

“Kwa ajili yangu?” nikarudia kauli yake kisha kidogo akili yangu ikakunjuka upesi na kukumbuka ile amri ya kumuua balozi wa Marekani ambayo nilipewa na wale watu walioniambia kama sharti la kupata vidongea vya kurejesha kumbukumbu. Kidogo nikapata mashaka.

“Ndio, tupo hapa kwa ajili yako, na ni kwasababu wewe ni mtu wetu.”

“Mtu wenu kivipi?” nikauliza na bwana yule akan’tazama kidogo pasipo kusema jambo. Alikuwa anafikiri jambo. Akajikuna kidevu chake na kusema, “Bwana Marshall ina maana haukumbuki chochote?”

“Sikumbuki kama mimi ni mtu wa CIA,” Nikamweleza. Basi akatoa nyaraka zinazonihusu na kunionyeshea. Ikiwamo na kitambulisho changu kama kielelezo. Nilipozitazama nikamuuliza bwana yule ni nini anajua zaidi kunihusu mimi na kwanini nipo pale ikiwa Katie amakamatwa nao?

Akiwa amefumbata viganja vyake, bwana Rodney akamwaga maneno akininasibu kuwa mimi ni ajenti wa CIA na nalikuwapo Ujerumani kwasababu za kutafuta taarifa zaidi juu ya upatikanaji wa Raisi wa Marekani ambaye alipotea kwenye mazingira ya kutatanisha.

Lakini ningalipo kwenye misheni hiyo nikapotea kwa kitambo pasipo maelezo yoyote. Walipojaribu kunifuatilia ndipo wakabaini kuwa nafanya kazi kwenye klabu kama mlinzi.

“Bwana Marshall, tutakuhitaji kwa ajili ya majadiliano zaidi. Tunakuomba utupe ushirikiano,” alisema bwana yule kumalizia habari yake.

“Bwana Rodney, natoaje ushirikiano na sifahamu wala sikumbuki kilichotokea?” nikatahamaki. Nikamtaka bwana Rodney anieleze wapi nilipokuwa nimefikia kwenye kesi yangu hiyo. Nani nilikuwa nashirikiana naye na mpaka mwisho ni taarifa gani nilikuwa nimeifikisha kwenye ofisi za CIA.

Kwanza kabla hajasema jambo, bwana Rodney akatazama baadhi ya karatasi zake kwa kama dakika tatu. Macho yake yalikuwa yakikatiza karatasini kwa upesi. Alipomaliza akan’tazama na kuniambia, “Bwana Marshall, una kesi kubwa ya kujibu nchini Marekani. Wewe ni mtuhumiwa mkubwa wa jaribio la kumuua Raisi, hivyo unahitajika kwa ajili ya maulizo zaidi.”

Habari hiyo ikanivuruga kichwa kabisa. Ndio sikuwa nakumbuka lolote lakini nilijiuliza kwanini nifanye kitendo kama hicho? Japo sikuwa na tone ya kumbukumbu, bado sikuafiki.

“Sijawahi kufikiria hilo bwana Rodney, nadhani utakuwa umekosea,” nikasema kwa kujiamini. Bwana yule akanitazama akitikisa kichwa kisha akaniambia kuna nyaraka kadhaa zikinituhumu kama msaliti wa taifa. Nyaraka na maelezo yote yapo nchini Marekani hivyo yawapasa kwenda haraka iwezekanavyo.

Aliposema hayo akan’tolea moja ya gazeti na kulitupia mezani. Nikakwapua gazeti hilo na kutazama, hamaki nikaona moja ya picha yangu na maneno yakiandikwa ‘MSALITI WA TAIFA’. Kabla sijasoma vema gazeti hilo, bwana Rodney akapiga makofi mara mbili na mara wakaja wanaume wawili kunichukua. Walikuwa wamebebelea bunduki.

“Mnanipeleka wapi? Hamtanipeleka mahali popote mpaka nimwone na mumwachie Katie!” nikafoka. Wale jamaa hawakujali, wakanijia wakitishia bunduki zao. “Twende mzima au ukiwa na majeraha,” mmoja akasema akin’tazama kwa umakini.

Nikageuza shingo kumtazama bwana Rodney,

“Nina habari unazozitaka!” nikamwambia kwa kujiamini. Bwana huyo akan’tazama kwa uso wenye mapuuzo na kuuliza, “Zipi hizo?”

“Mwachie Katie huru na mmi nitakueleza,” nikampa sharti. Akan’tazama kwa ufupi kisha akawatazama wale jamaa wawili na kuwapa ishara ya kichwa, mara mmoja akaenda zake na kurejea na Katie. Alikuwa salama salmini pasipo na jeraha.

Nikamkumbatia na kumuuliza kama yuko sawa. Akaniambia yuko sawa lakini hajui anafanya nini pale. Alikuwa na uso wa kukanganyikiwa. Aliniuliza kama nawajua watu wale, nami nikamjibu siwafahamu.

“Sikia, Katie. Nitazame. Usihofu, sawa? Utakuwa salama, nitakuwa salama, sawa?” baada ya kumwambia hivyo nikamnong’oneza sikioni juu ya nini afanye. Akachukue pesa kadhaa nilizoziweka mahali fulani na ahame pale anapokaa haraka iwezekanavyo.

“Vipi kuhusu wewe?” akaniuliza. Macho yake yalikuwa mekundu. Ndani yake niliona amejawa na hofu. Nikamshika kichwa chake na kumwambia kwa kujiamini kabisa, asijali kunihusu. Mimi nitakuwa salama kabisa na nitarejea kwa ajili yake.

Kwa muda ule aende kwanza nyumbani na ahakikishe hamna mtu yeyote anayemfuata nyuma, basi akaenda zake japo kwa shingo upande.

“Naam,” Bwana Rodney akapaza sauti yake akin’tazama. “Sasa waweza kuniambia una habari gani ninazozitaka?”

Ulikuwa umepita muda kidogo tangu Katie aachiwe huru na kujihakikishia hilo kwa macho yangu. Nikashusha pumzi ndefu nikiwa nimeshakagua eneo na kuamua nini la kufanya kichwani. Niliadhimia kutoroka nikamkute Katie.

“Sina habari yoyote,” nikasema na kisha upesi nikawageukia wale jamaa wawili walinzi waliokuwa karibu yangu, upesi nikawadhibiti kwa mapigo ya haraka mno, lakini kabla sijamalizana nao, nikahisi kutobolewa shingoni.

Nilipopapasa nikabaini nimechomwa sindano ya kufyatua. Bwana Rodney alikuwa ameshikilia bunduki ya silaha hiyo. Nikamwona akinijongea na mimi nikipoteza nguvu kwa haraka sana.

Mara nikajikuta nikipiga magoti na huku kichwa kikinizunguka kana kwamba pia. Sikuweza kusimama japo nilijitahidi. Macho ni kama yalijawa na ukungu, hayakuwa yanaona vema. Nilihii misuli yangu inasinyaa kudhoofika.

Kwa mbali nilisikia kishindo cha mtu kikinijongea na kukomea mbele yangu kisha sauti ya mtu ikininong’oneza, “Umekwisha, Marshall.”

Baada ya hapo nikadondoka na kupoteza fahamu kabisa. Nilikuwa kizani nisielewe chochote kile!

*****
 
Endeleza story bas mzeebaba!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom