Tito kihodombi
Member
- Apr 1, 2019
- 58
- 56
Asante mkuu steve
Mkuu, acha bana hayo mambo. Riwaya imekamilika mpaka mwisho na naituma hapahapa. EnjoyRiwaya za steve hasa za kijasusi huwa hazikamiliki ukiondoa ANGA LA WASHENZI zinazobakia huwa ni magumashi tu.
Ni bora aachane na uandishi wa riwaya kama yupo bize na shughuli zingine.
Endeleza story bas mzeebaba!!!*NYUMA YAKO (MSIMU WA PILI) --- 02*
*Simulizi za series*
ILIPOISHIA
Nilipojongea zaidi, mmoja ambaye alikuwa mbele kabisa ya mlango, akapiga hatua kuuendea mlango na kisha akaufungua kunikaribisha humo. Nami pasipo kuuliza wala kuongea nao, nikasonga ndani humo na kumkuta mwanaume mmoja mwenye makamo ya miaka arobaini.
Mwanaume huyo alikuwa amevalia suti na kulaza vema nywele zake. Alikuwa amekunja nne akin’tazama kwa uso ulioficha hisia. Nilipomkaribia akatabasamu na kusema, “Karibu, uketi bwana Marshall.”
Nikamkosoa kwa kumwambia, “Naitwa Tarrus.”
Akatabasamu zaidi.
ENDELEA
Nilipomtazama ndipo nikamwona mwanaume mwenye macho madogo ya paka. Lips nyembamba na kidevu kilichochongoka kana kwamba kiwiko. Masikio yake yalikuwa makubwa na hata ukitazama kwa wepesi waweza kuona yalikuwa na nywele ndaniye.
Kitu hiko kilin’shangaza kidogo kwani sikuona kama umri wake unasadifu yeye kuanza kuchomoza nywele masikioni. Lakini sikuwa na muda wa kuwaza sana kwani nalikuwapo eneo hatari. Na huyo aliyekuwa amekaa mbele yangu sikuwa namtambua kwa namna yoyote ile.
Kitu pekee ambacho nilikuwa na uhakika nacho ni kwamba anahusika na kumhifadhi Katie. Katie aliyenifanya niwapo hapo.
“Habari yako kijana? Naitwa Rodney Rufus. Karibu sana,” alisema bwana huyo akin’tazama kwa macho ya kirafiki.
“Nashukuru kwa kukufahamu, bwana Rodney. Unaweza kuniambia kwanini unanitakia nini tafadhali? Na kama kulikuwa na haja ya wewe kumteka mtu asiye na hatia?”
Akasafisha koo lake na kutazama chini.
“Bwana Marshall --”
“Naitwa Tarrus!”
“Unaitwa Marshall - Anthony Marshall,” bwana yule akasema akinikazia macho. “Kama hutojali, waweza kuniruhusu nijitambulishe kwako. Nilidhani utakuwa unanikumbuka hata kwa kuniona,” aliposema hivyo akan’tazama kwa maswali, “Vipi kwani wanikumbuka?”
Nikabinua mdomo wangu na kutikisa kichwa. Sikutia neno.
“Sawa, kama nilivyokuambia hapo awali naitwa Rodney Rufus. Mimi ni afisa wa shirika la ujasusi la Marekani, CIA. Nipo hapa Ujerumani kwa ajili yako.”
“Kwa ajili yangu?” nikarudia kauli yake kisha kidogo akili yangu ikakunjuka upesi na kukumbuka ile amri ya kumuua balozi wa Marekani ambayo nilipewa na wale watu walioniambia kama sharti la kupata vidongea vya kurejesha kumbukumbu. Kidogo nikapata mashaka.
“Ndio, tupo hapa kwa ajili yako, na ni kwasababu wewe ni mtu wetu.”
“Mtu wenu kivipi?” nikauliza na bwana yule akan’tazama kidogo pasipo kusema jambo. Alikuwa anafikiri jambo. Akajikuna kidevu chake na kusema, “Bwana Marshall ina maana haukumbuki chochote?”
“Sikumbuki kama mimi ni mtu wa CIA,” Nikamweleza. Basi akatoa nyaraka zinazonihusu na kunionyeshea. Ikiwamo na kitambulisho changu kama kielelezo. Nilipozitazama nikamuuliza bwana yule ni nini anajua zaidi kunihusu mimi na kwanini nipo pale ikiwa Katie amakamatwa nao?
Akiwa amefumbata viganja vyake, bwana Rodney akamwaga maneno akininasibu kuwa mimi ni ajenti wa CIA na nalikuwapo Ujerumani kwasababu za kutafuta taarifa zaidi juu ya upatikanaji wa Raisi wa Marekani ambaye alipotea kwenye mazingira ya kutatanisha.
Lakini ningalipo kwenye misheni hiyo nikapotea kwa kitambo pasipo maelezo yoyote. Walipojaribu kunifuatilia ndipo wakabaini kuwa nafanya kazi kwenye klabu kama mlinzi.
“Bwana Marshall, tutakuhitaji kwa ajili ya majadiliano zaidi. Tunakuomba utupe ushirikiano,” alisema bwana yule kumalizia habari yake.
“Bwana Rodney, natoaje ushirikiano na sifahamu wala sikumbuki kilichotokea?” nikatahamaki. Nikamtaka bwana Rodney anieleze wapi nilipokuwa nimefikia kwenye kesi yangu hiyo. Nani nilikuwa nashirikiana naye na mpaka mwisho ni taarifa gani nilikuwa nimeifikisha kwenye ofisi za CIA.
Kwanza kabla hajasema jambo, bwana Rodney akatazama baadhi ya karatasi zake kwa kama dakika tatu. Macho yake yalikuwa yakikatiza karatasini kwa upesi. Alipomaliza akan’tazama na kuniambia, “Bwana Marshall, una kesi kubwa ya kujibu nchini Marekani. Wewe ni mtuhumiwa mkubwa wa jaribio la kumuua Raisi, hivyo unahitajika kwa ajili ya maulizo zaidi.”
Habari hiyo ikanivuruga kichwa kabisa. Ndio sikuwa nakumbuka lolote lakini nilijiuliza kwanini nifanye kitendo kama hicho? Japo sikuwa na tone ya kumbukumbu, bado sikuafiki.
“Sijawahi kufikiria hilo bwana Rodney, nadhani utakuwa umekosea,” nikasema kwa kujiamini. Bwana yule akanitazama akitikisa kichwa kisha akaniambia kuna nyaraka kadhaa zikinituhumu kama msaliti wa taifa. Nyaraka na maelezo yote yapo nchini Marekani hivyo yawapasa kwenda haraka iwezekanavyo.
Aliposema hayo akan’tolea moja ya gazeti na kulitupia mezani. Nikakwapua gazeti hilo na kutazama, hamaki nikaona moja ya picha yangu na maneno yakiandikwa ‘MSALITI WA TAIFA’. Kabla sijasoma vema gazeti hilo, bwana Rodney akapiga makofi mara mbili na mara wakaja wanaume wawili kunichukua. Walikuwa wamebebelea bunduki.
“Mnanipeleka wapi? Hamtanipeleka mahali popote mpaka nimwone na mumwachie Katie!” nikafoka. Wale jamaa hawakujali, wakanijia wakitishia bunduki zao. “Twende mzima au ukiwa na majeraha,” mmoja akasema akin’tazama kwa umakini.
Nikageuza shingo kumtazama bwana Rodney,
“Nina habari unazozitaka!” nikamwambia kwa kujiamini. Bwana huyo akan’tazama kwa uso wenye mapuuzo na kuuliza, “Zipi hizo?”
“Mwachie Katie huru na mmi nitakueleza,” nikampa sharti. Akan’tazama kwa ufupi kisha akawatazama wale jamaa wawili na kuwapa ishara ya kichwa, mara mmoja akaenda zake na kurejea na Katie. Alikuwa salama salmini pasipo na jeraha.
Nikamkumbatia na kumuuliza kama yuko sawa. Akaniambia yuko sawa lakini hajui anafanya nini pale. Alikuwa na uso wa kukanganyikiwa. Aliniuliza kama nawajua watu wale, nami nikamjibu siwafahamu.
“Sikia, Katie. Nitazame. Usihofu, sawa? Utakuwa salama, nitakuwa salama, sawa?” baada ya kumwambia hivyo nikamnong’oneza sikioni juu ya nini afanye. Akachukue pesa kadhaa nilizoziweka mahali fulani na ahame pale anapokaa haraka iwezekanavyo.
“Vipi kuhusu wewe?” akaniuliza. Macho yake yalikuwa mekundu. Ndani yake niliona amejawa na hofu. Nikamshika kichwa chake na kumwambia kwa kujiamini kabisa, asijali kunihusu. Mimi nitakuwa salama kabisa na nitarejea kwa ajili yake.
Kwa muda ule aende kwanza nyumbani na ahakikishe hamna mtu yeyote anayemfuata nyuma, basi akaenda zake japo kwa shingo upande.
“Naam,” Bwana Rodney akapaza sauti yake akin’tazama. “Sasa waweza kuniambia una habari gani ninazozitaka?”
Ulikuwa umepita muda kidogo tangu Katie aachiwe huru na kujihakikishia hilo kwa macho yangu. Nikashusha pumzi ndefu nikiwa nimeshakagua eneo na kuamua nini la kufanya kichwani. Niliadhimia kutoroka nikamkute Katie.
“Sina habari yoyote,” nikasema na kisha upesi nikawageukia wale jamaa wawili walinzi waliokuwa karibu yangu, upesi nikawadhibiti kwa mapigo ya haraka mno, lakini kabla sijamalizana nao, nikahisi kutobolewa shingoni.
Nilipopapasa nikabaini nimechomwa sindano ya kufyatua. Bwana Rodney alikuwa ameshikilia bunduki ya silaha hiyo. Nikamwona akinijongea na mimi nikipoteza nguvu kwa haraka sana.
Mara nikajikuta nikipiga magoti na huku kichwa kikinizunguka kana kwamba pia. Sikuweza kusimama japo nilijitahidi. Macho ni kama yalijawa na ukungu, hayakuwa yanaona vema. Nilihii misuli yangu inasinyaa kudhoofika.
Kwa mbali nilisikia kishindo cha mtu kikinijongea na kukomea mbele yangu kisha sauti ya mtu ikininong’oneza, “Umekwisha, Marshall.”
Baada ya hapo nikadondoka na kupoteza fahamu kabisa. Nilikuwa kizani nisielewe chochote kile!
*****
Jibu zuri!Mkuu, acha bana hayo mambo. Riwaya imekamilika mpaka mwisho na naituma hapahapa. Enjoy