#COVID19 Nyuma ya pazia ripoti ya chimbuko la Corona inayotarajiwa kutolewa wiki hii

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Baada ya subira ya muda mrefu, hatimaye ripoti ya timu ya wataalamu wa Shirika la Afya Duniani, WHO iliyopewa kazi ya kuchunguza chanzo cha maambukizi ya virusi vya corona inatarajiwa kutolewa wiki hii.

Ujumbe huo uliwasili Wuhan mwezi Januari kufanya uchunguzi kwa muda wa mwezi mmoja katika eneo ambalo ni kitovu cha maambukizi hayo, na ni katika mji huo ambapo kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya corona kiligunduliwa, ikiwa na lengo la kubaini ni kwa jinsi gani maambukizi ya virusi hivyo yalivyohama kutoka kwa wanyama hadi kwa binadamu.

Mwezi mmoja baada ya Ujumbe huo wa WHO kuondoka China, ripoti hiyo inatarajiwa kutolewa wakishirikiana na timu ya wataalamu wa afya kutoka China, ikitarajiwa kutoa mwanga wa uhalisia wa chanzo cha maambukizi ya virusi vya corona na kuondoa sintofahamu iliyokuwepo duniani kwa miezi 15 sasa.

Kinachotarajiwa kuwepo katika ripoti hiyo
Mapema mwezi Februari kabla ya kuondoka katika mji wa Wuhan, Ujumbe huo uliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutoa matarajio ya ripoti hiyo, ukisema kuwa baada ya kujiridhisha, wamebaini kuwa virusi vya corona havikuanzia maabara kama ambavyo Rais wa Marekani aliyemaliza muda wake, Donald Trump aliwahi kusema.

Awali, iliaminika kuwa virusi vya SARS-CoV-2, aina mpya ya virusi vya corona vilivyosababisha UVIKO-19 iliaminika kutokana na wanyama jamii ya popo, lakini baada ya utafiti wa sampuli kutoka maelfu ya wanyama pori na wa kufugwa kutoka katika eneo hilo, ilionekana kuwa hakukuwa na dalili ya virusi hivyo kutoka kwa wanyama wanaoapatikana hapo, licha ya kuwa kisa cha kwanza kinachojulikana na COVID-19 kilitokea katika mji wa Wuhan.

Utafiti huo umekuja na dhanio kuwa ndege hao [popo] walisafiri kutoka maeneo ya Kusini mwa nchi hadi katika eneo la Wuhan, ambao wamegundulika kuwa na virusi vinavyokaribia sana kufanana na SARS-CoV-2 vilivyopatikana Wuhan.

Hali hiyo inatoa uwezekano wa virusi hivyo kuwaigia binadamu au wanyama wanaofugwa katika eneo la Wuhan hadi kufikia soko la wanyama ambapo ndipo kisa cha kwanza kilihusishwa kuanzia.

Mvutano wa Marekani na China kuhusu uwazi wa ripoti

Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti mzozano uliopo kati ya Marekani na China nyuma ya pazia kuhusu ripoti hiyo, upande mmoja ukitaka uwazi zaidi huku upande mwingine ukidai kuwa utafiti huo usingewezekana bila msaada kutoka Beijing.

Awali kulikuwa na mpango wa kutoa muhtasari pekee wa ripoti hiyo bila kutoa takwimu kamili za ripoti, lakini Shirika la Afya Duniani likatupilia mbali mpango huo bila kutoa maelezo zaidi. Ikulu ya Marekani ilikuwa mstari wa mbele kutaka uwazi zaidi kuhusu ripoti hiyo ikidaiwa kushawishi maamuzi ya Shirika la Afya Duniani ya kutolewa kwa ripoti nzima badala ya muhtasari tu.

Ingawa Rais Biden ameonesha kuipendelea zaidi WHO tofauti na mtangulizi wake aliyekuwa akitamka wazi kuwa Shirika hilo ni kibaraka wa China, Marekani bado imeendelea kuonesha wasiwasi wake kuhusu shirika hilo ikiitaka China kutoa takwimu zaidi.

Ingawa timu hiyo ya wataalamu inasisitiza kuwa imepata ushirikiano wote kutoka China kuandaa ripoti hiyo, kiongozi wa timu hiyo bado anaomba takwimu zaidi kutoka China ili kuendelea kuchimbua kiini cha ugonjwa huo ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu milioni 2.6 kote duniani.

Chanzo: AFP
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom