Nyuma ya Pazia: Ni uenyekiti ulibadili nia ya Lissu kurudi?

Dankbar

Member
Jul 11, 2015
98
113
Uwepo wa Lisu ulitegemea kuongeza ushindani na hamasa ya uchaguzi, hasa baada misukosuko aliyopambana nayo. Wanachama na wasio wanachama wanatambua msimamo wa Lissu usioyumba lakini kwa upande mwingine ni mwaminifu na mtii kwa chama na viongozi. Kimempata nini hata akabadilisha msimamo wa kurudi?

Kilichopo nyuma ya pazia: Hofu mwenye kiti zidi ya Lisu kuwania uenyekiti au watu kumshawishi awanie uenyekiti, zilipelekea kumshauri asirudi kwa hoja ya ya usalama (mbele ya pazia) licha ya nia yake aliyotangaza kuwa atarudi.

Mafanikio ya mpango wa nyuma ya pazia: Umefanikiwa kwa 95% kwani umaarufu wake na jina lake limefifia baada ya kumshauri atangaze kuwa hatarudi.

Mwenye kufaidika na mpango wa nyuma ya pazia: Mwenye hati miliki ya uenyekiti ambaye kila anayeibuka kutangaza nia ya kuwania nafasi hiyo hasa kama ni maarufu kudidimizwa au huzamishwa mara.

Mwaliko: Chungulieni nyuma ya pazia, baada ya uchaguzi mpango wa Lissu kurudi utaendelea
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom