Nyuma ya Pazia: Kobe Bryant, sura yake na fumbo la kifo

Johnny Sins

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,538
3,826
Aliandika mahala, John Hoyer Updike, mwandishi mahiri wa mashahiri wa Marekani, alisema ‘Ukitaka kuhesabika uwe nguli, inabidi ufe mapema’. Mapema ni umri gani? Hatuwezi kujua. Labda miaka 41. Labda.

Sijui kwanini alisema alichosema. Umauti ulimkumbuka Updike miaka 11 iliyopita katika kitanda cha hospitali moja jijini Massachusetts. Inawezekana aliondoka duniani huku akiamini kwamba walimwengu hawakumkubali sana kama ilivyotakiwa.

Inaweza ilikuwa hivyo kwake, lakini maandiko yake yametimia kwa mtu aliyeitwa Kobe Braynt. Ameiaga dunia Jumapili asubuhi kwa ajali ya chopa akiwa na umri wa miaka 41. Kabla yake nyuma, takribani miaka 40 iliyopita, Bob Marley aliiaga dunia akiwa na miaka 36 tu. Utawahesabu wengi na wengi. Utakwenda hadi kwa Tupac Shakur aliyefariki akiwa na miaka 25.

Kobe ametuacha utajiuliza kwanini naandika kuhusu Kobe na sio soka. Nikukumbushe kwamba utotoni Kobe alicheza soka pale Italia na alikuwa shabiki mkubwa wa AC Milan. Wakati huo baba yake, Joe alihamia Italia na familia yake. Familia iliporudi Marekani akajikita katika kikapu. Hakuwahi kuacha kuwa shabiki wa soka.

Juzi AC Milan imeilaza jezi namba 24 ya timu yao kwa ajili ya kumkumbuka Kobe. Lakini pia Kobe hakuwahi kuacha kuwa shabiki wa soka na pia rafiki wa wanasoka. Amepiga picha na mastaa kibao wa soka wasiohesabika. Ukianzia kwa Ronaldinho, Neymar, Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na wengine.

Lakini pia kwanini Kobe yupo katika ukurasa huu leo? Jibu ni rahisi zaidi. Ni kwa sababu ya ‘ile sura yake’. Ndio, ile sura. Kuna sura zipo kila siku na zinakatiza katika macho ya kila mtu kwa sababu ya vipaji maridhawa walivyojaliwa navyo. Kobe anaingia katika mkumbo huu.

Hii ni tafsiri halisi ya kuitwa nguli, au wazungu wanaita icon. Kobe yupo katika kiwango cha kina Messi, Ronaldo, Tiger Woods, Tupac Shakur, Mike Tyson, Michael Jordan, Serena Williams na wengine wa kariba hii. Nadhani umenielewa.

Unakaa kando ya televisheni yako, unatazama mchezo usiouelewa au taarifa ya habari, inapita sura ya mtu unajisemea ‘Huyu namfahamu’. Sio kila mwanamichezo anafikia hatua hii. Anapofikia ujue yeye ni icon. Ujue yeye ni nguli. Kobe alifika huku.

Kuchambua uhodari wa Kobe katika uwanja wa kikapu unahitaji uwe mtaalamu zaidi wa mchezo wenyewe lakini inatosha kuzitaja rekodi chache tu. Kama vile, Kobe alikuwa mchezaji wa kwanza wa kikapu kufunga vikapu 80 ndani ya mechi moja ya NBA. Haijawahi kutokea kabla ya hapo. Alifanya hivyo katika pambano dhidi ya Toronto Raptors mwaka 2006.

Kobe ni mchezaji wa kwanza NBA kufikisha vikapu 30,000. Kobe ni mchezaji wa kwanza NBA kutoa pasi za vikapu 6,000. Katika umri wa miaka 37, Kobe alikuwa mchezaji mkubwa zaidi kuwahi kufunga vikapu 60 katika mechi moja. Watu wa soka wakitafsiri haya katika takwimu za kisoka za kufunga, kupiga pasi za mwisho, na pia kufunga mabao mengi ndani ya mchezo mmoja huku ukiwa na umri mkubwa watagundua kwamba Kobe alikuwa mchezaji wa aina gani.

Kobe ameondoka katika mazingira ambayo yanayotatanisha zaidi. Kwanza kabisa ni namna gani ambavyo inabidi tuendelee kumuabudu Mungu. Kwanza kabisa ameacha utajiri wenye thamani ya Dola 500 milioni. Hii ni siri ya Mungu. Kobe amechuma mabilioni ya pesa akiwa na Lakers. Alistaafu akiwa na umri wa miaka 34 Mungu amemchukua akiwa na miaka 41. Watoto wa mjini wanaamini hakuifaidi pesa yake. Kumbe pesa sio kila kitu.

Haiwezi kununua uhai. Kobe pia hakuwahi kuwa na mtoto wa kiume. Alijaliwa watoto wanne wa kike. Mtoto mmoja wa kike, Gigi aliamua kumfuta machozi kwa kufuata nyayo zake za kucheza kikapu. Huyu alikuwa naye karibu zaidi.

Alionekana angekuja kuwa staa mkubwa wa kikapu siku za usoni. Huzuni iliyoje, ameondoka naye katika ajali! Lakini kuna hili jingine. Kobe ameondoka duniani akiwa haelewani na wazee wake. Wakati fulani akiwa anapata pesa nyingi wazazi wake waliamua kuuza moja kati ya nyumba ambazo aliwanunulia. Kobe hakuwaelewa. Asingeweza kuwaelewa.

Alikuwa anawahudumia kwa kila kitu. Kwanini wauze nyumba? Baadaye aliwapeleka mahakamani akiwa na lengo la kuzuia kuuzwa kwa nyumba. Mgogoro ukawa mkubwa zaidi. Mgogoro huo ulisababisha wasihudhurie harusi yake wakati alipomuoa Vanessa. Mpaka anafariki Jumapili asubuhi Kobe alikuwa haongei na wazazi wake.

Mpaka sasa wazazi wake hawajaposti kitu kuhusiana na kifo cha mtoto wao. Inawezekana wanaumia zaidi. Kwanini hawakusuluhishana na mtoto kabla hajafa? Na labda huko aliko, Kobe ana majuto ya kwanini hakumalizana na wazazi wake kabla hajaondoka? Mungu mkubwa.

Eddo Kumwembe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona umeamua tu kuandika kumhusu Kobe.

Lakini wewe mwenyewe sidhani hata kama ulijua unataka kuandika kuhusu nini ?
NIkweli mkuu, jamaa hakuwa anafahamu anataka kuandika kuhusiana na nini. Mada ya ajabu kabisa. Na hawa ndio waandishi wetu. Wanatujaza madudu tu .
 
kobe Alikuwa poa tu na wazee wake, muda fulani alihitilafiana nao kwa kile wazee wanadai alikuwa anaoa katika umri mdogo hii ni pale alipoamua kumwoa mwanamke wake Vanesa kipindi hicho akiwa under 25 na Vanesa ndo katurn 18...lakini baada ya mtoto wao wa kwanza kuzaliwa mahusiano na wazazi wake yalikaa vizuri.
 
Hiyo nyuma ya pazia ni ipi hapo sasa , mtoa mada kaandika yaleyale yanayoandikwa na wengine sehemu kibao afu yeye kuchwa cha uzi anasema nyuma ya pazia wakati ndo yale yanayofahamika na wala sijaona hilo fumbo la kifo chake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom