Nyuma ya Muungano wetu

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
2,646
2,024
Kusherehekea Muungano bila kuyaenzi madhumuni ya TANU yaliyozaa Chama Cha Mapinduzi ni sawa na kufurahia Matokeo ya kuuacha Mchakato

Miongoni mwa masuala ambayo yaliyofanya chama cha TANU kuwa imara sana na kuweza kuzaa chama kilichotokana na Muungano wa vyama viwili ni makusudi na madhumuni yake. Madhumuni hayo ni haya yafuatayo:
 • Kuudumisha uhuru wa Nchi yetu na raia wake
 • Kuweka heshima ya Mwanadamu kwa kufuata barabara Kanuni za Tangazo la ulimwengu za haki za binadamu.
 • Kuhakikisha kwamba Nchi yetu inatawaliwa na Serikali ya watu ya kidemokrasi na ya kisoshalisti;
 • Kushirikiana na vyama vyote vya siasa katika Afrika vinavyopigania uhuru wa bara lote la Afrika;
 • Kuona kwamba Serikali inatumia mali yote ya Nchi yetu kwa kuondoshea umasikini, ujinga na maradhi;
 • Kuona kwamba Serikali inasaidia kwa vitendo kuenda na kudumisha vyama vya ushirika;
 • Kuona kwamba kila iwezekanapo Serikali inashiriki hasa katika maendeleo ya uchumi wa Nchi yetu;
 • Kuona kwamba Serikali inatoa nafasi zilizo sawa kwa wote, wake kwa waume, vila kujali rangi kabila au hali;
 • Kuona kwamba Serikali inaondoa lila namna ya dhuluma vitisho, ubaguzi, rushwa na upotofu;
 • Kuona kwamba Serikali ya Nchi yetu inasimamia barabara njia kuu za kuzalisha mali na inayofuata siasa ambayo itarahisisha njia ya kumiliki kwa jumla mali za Nchi yetu.
 • Kuona kwamba Serikali inashirikiana na dola nyingine katika Afrika katika kuleta umoja wa Afrika;
 • Kuona kwamba Serikali inajitahidi kuleta amani na salama ulimwenguni kwa njia ya chama cha umoja wa mataifa.
..................................
Tangu nipitie madhumuni ya vyama mbalimbali vya siasa sijawahi kuona madhumuni bora zaidi ya haya. Ni madhumuni bora kuwahi kutokea Duniani. Ni msingi wa utu na udugu wenye lengo la kukuza tangamano na hatimaye umajumui.

Chama cha Mapinduzi ni Mtoto aliyezaliwa ndani ya makusudi haya. Ni mrithi wa hazina hii iliyotukuka ambayo kwa pamoja inaweza kutamkwa kwa maneno mawili yakiwa na kiunganishi yaani " UHURU NA UMOJA".

Tunaufurahia Muungano ambao kwa kweli ni matokeo yaliyosukumwa na kusudi na madhumuni. Makusudi au madhumuni hayo kw hakika ni makusudi na madhumuni ya TANU. Naandika haya kwa lengo la kutaka kuweka mizania juu ya namna tunavyouenzi Muungano wetu ili usijekuwa sawa na kumsifia sana Mtoto aliyezaliwa na kumuacha Mama aliyemzaa.

"...nyuma ya kila kitu kuna kila kitu".
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom