Nyufa kubwa na mfumo mbaya wa maji taka vya hatarisha udom | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyufa kubwa na mfumo mbaya wa maji taka vya hatarisha udom

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Albano, May 24, 2011.

 1. A

  Albano Member

  #1
  May 24, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Faculty of social sciences and Humanities ya chuo kikuu cha Dodoma, ina nyufa kubwa sana zinazohatarisha maisha ya wanafunzi wa chuo hicho. Pia mifumo ya majitaka ni mibovu kiasi cha kusababisha harufu mbaya kwenye ma bweni na kuna muda hata maji hayapandi kwenye vyoo na baadhi ya vyoo vimefungwa kiasi cha kuwafanya wanafunzi wahamie facult nyingine kwa ajili ya kupata huduma hiyo muhimu.

  Hayo yote yameshuhudiwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM ndugu Nape baada ya msafara wake uliokuwa umetoka kwa Mkuu wa Chuo Pro. Kikula kusimamishwa na wanafunzi na kumwambia aende akaone hali halisi na kumuomba aongee na Rais ili serikali itatue hili haraka iwezekanavyo.

  Nape alijionea mwenyewe na kuwa ahidi vijana wa UDOM kuwa suala hili atalishughulikia kwani lengo la CCM ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu katika mazingira mazuri na pia alisisitiza mifumo hiyo mibovu ya maji taka ni hatari kwa magonjwa ya milipuko kama kipindupindu.

  Vijana wa UDOM wamekuwa na imani sana na huyo kiongozi kijana anayekuja kwa kasi katika kuisimamia serikali kutekeleza wajibu wake.
   
 2. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hicho ni chuo kimoja tu! Vipo Vingi vyenye uozo mkubwa kuliko hiki mwambieni Nape azunguke vyuo vyote atashangaa,
  Lakini pia yeye (Nape) Siyo Gamba?
   
 3. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisaaa, Nape anakuja kwa kasi sana ya PROPAGANDA NA AHADI ZISIZOTEKELEZEKA ZA CHAMA CHAKE
   
 4. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hakuna mwanachuo hata mmoja aliyemsifia Nape. Jamani tuache unafiki. Nape alikuja kufanya udom?
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Ndiyo ndiyo, anakuja kwa kasi kweli na siye tunamuona......

  [​IMG]
   
 6. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Uyo Nape alikuja lini na saa ngapi? Kwanza habari yenyewe ndo naioa humu JF so we uliyeandika acha unafiki pia Nape ana hadhi gani kuja chuoni na kutatua matatizo? Ila kwa Nyufa na maji taka hayo ni kweli ila la Nape usidanganye umma!
   
 7. Edson Zephania

  Edson Zephania Verified User

  #7
  May 24, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Umeanza post vzr ila la Nape umetuongopea. Ni ukweli usiopingka kua mifumo ya maj taka pale social ni mibov mpk kupelekea hata mazngira yake kunuka vibaya ukianzia stend ya dldl na uktaka kujua harufu mbaya tembea nyakat za usiku.
   
 8. M

  Msharika JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hiyo VX V* ndiyo ya katibu mwenezi?
   
 9. A

  Albano Member

  #9
  May 24, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Faculty of social sciences and Humanities ya chuo kikuu cha Dodoma, ina nyufa kubwa sana zinazohatarisha maisha ya wanafunzi wa chuo hicho. Pia mifumo ya majitaka ni mibovu kiasi cha kusababisha harufu mbaya kwenye ma bweni na kuna muda hata maji hayapandi kwenye vyoo na baadhi ya vyoo vimefungwa kiasi cha kuwafanya wanafunzi wahamie facult nyingine kwa ajili ya kupata huduma hiyo muhimu.

  Hayo yote yameshuhudiwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM ndugu Nape baada ya msafara wake uliokuwa umetoka kwa Mkuu wa Chuo Pro. Kikula kusimamishwa na wanafunzi na kumwambia aende akaone hali halisi na kumuomba aongee na Rais ili serikali itatue hili haraka iwezekanavyo.

  Nape alijionea mwenyewe na kuwa ahidi vijana wa UDOM kuwa suala hili atalishughulikia kwani lengo la CCM ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu katika mazingira mazuri na pia alisisitiza mifumo hiyo mibovu ya maji taka ni hatari kwa magonjwa ya milipuko kama kipindupindu.

  Vijana wa UDOM wamekuwa na imani sana na huyo kiongozi kijana anayekuja kwa kasi katika kuisimamia serikali kutekeleza wajibu wake.
   
 10. E

  Eng Mayeye Member

  #10
  May 24, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naamini kuwa kunahaja ya mh. Kikwete kuwafanyisha interview baadhi ya watendaji wake wakuu kabla ya kuwapa uongozi, pia wawe na muda wa probation ya miezi 6 huku akiwataka wamuonyeshe action plan ndan ya mwezi moja na kuwataka wawe wanampelekea weekly and monthly reports na asiye meet target every month kwa Muda wa miezi 3 mfululizo apewe hatua za kinidham kama warning pia kuwajibishwa kwa manufaa ya umma... WATENDAJI wa serikali wamekuwa wakiipaka matope serikali yake... Unataka kunambia kuanzia warden, mkuu wa chuo, mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho hawaliona hili hadi aje alione mhe. NAPE? Haya wizara husika na watendaji wake hawalion hili? Je ni kweli pesa za ukarabati hazitolewi? AIBU GANI KUIFANYIA HUJUMA SERIKALI YETU?? Ni aibu kama ili suala litamfikia mhe Kikwete na ndo maana anawafukuza maofisin waende kushughulikia kero za wananch... BIG UP NAPE, Kama kazi yao ni kusisinzia maofisin na kula pesa za umma hilo halikubaliki.. Ni lazima kupinga kwa nguvu zote... Ukarabati ndo uhai wa majengo ya chuo.
   
 11. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #11
  May 25, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Poor Serikali ya Kikwete walisema UDOM ni mafanikio yake ataacha sifa kumbe Majengo yananyonyofoka... na kwanini anatumwa Nape?
  Kuna picha za Slaa Bwenini

  Tuesday, 24 May 2011 20:04 newsroom

  NA BASHIR NKOROMO, DODOMA

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewaagiza viongozi wanaohusika kwenda kukagua majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ili kulipatia ufumbuzi tatizo la nyufa zilizoanza kujitokeza kwenye baadhi ya majengo. Chama pia kimewaagiza viongozi hao kukagua miundombinu ya majitaka katika baadhi ya maeneo chuoni hapo, ili ifanyiwe marekebisho na kuondokana na adha ya harufu mbaya. Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, aliagiza hayo jana baada ya kutembelea chuo hicho na kukagua baadhi ya majengo ambayo yana nyufa. Majengo yenye nyufa ni ya
  mabweni ya wanafunzi wa Shule ya Sayansi ya Jamii yaliyoko Block 2 na 3. "Kujengwa kwa chuo hiki ni uamuzi wa
  [​IMG]

  Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, hivyo ni lazima kuuenzi uamuzi huu kwa kuhakikisha mazingira na majengo yanakuwa katika hali bora," alisema. Nape alishangazwa na nyufa hizo katika majengo ambayo hayajatimiza hata miaka mitano tangu yalipojengwa, jambo alilosema ni la hatari kwa usalama wa wanafunzi. Awali, Makamu Mkuu wa UDOM, Profesa Idris Kikula, akizungumza na Nape, alisema chuo hicho kina wanafunzi 20,000 ambao kati yao asilimia 50 wanalipiwa gharama za masomo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.

  Profesa Kikula alisema chuo hicho kina wanafunzi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Msumbiji, na kina walimu kutoka Russia, India, Kenya, Nigeria, Korea, Japan, Poland na Sweden. Alisema chuo kina uhaba wa walimu kwa kuwa wengi waliopo sasa ni wazee na wengine wanaugua magonjwa yanayoambatana na utu uzima. Profesa Kikula alisema tatizo hilo limewafanya kuendelea kupokea wanafunzi wasiozidi 20,000, wakati kina uwezo wa kuwa na wanafunzi hadi 35,000. Alisema katika kukabiliana na tatizo hilo, chuo kimeajiri vijana zaidi ya 300, lakini zaidi ya 200 wapo masomoni ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuwa na wahadhiri wasaidizi wengi.

  Last Updated ( Tuesday, 24 May 2011 20:29

  Tuesday, May 24, 2011

  NAPE ATEMBELEA UDOM LEO, AAGIZA MAJENGO YENYE NYUFA YASHUGHULIKIWE HARAKA  CCM imewaagiza viongozi wanaohusika kwenda kukagua majengo ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) ili kulipatia ufumbuzi wa haraka tatizo la nyufa zilizoanza kuitokeza kwenye baadhi ya majengo.

  Chama kimewaagiza pia viongozi hao kukagua hali ya miundombinu ya majitaka katika maadhi ma maeneo chuoni hapo ili ifanyiwe marekebisho kwa kuwa inatuamisha maji kutoka katika majengo na kusababisha adha ya harufu mbaya kwa wanafunzi, walimu na wafanyakazima,m wengine chuoni hapo.

  Maagizo hayo yalitolewa leo, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, baada ya kutembelea chuo hicho na kagua baadhi ya majengo ambapo alishuhudia baadhi ya majengo yakiwa na nyufa.

  Majengo yaliyoonyesha kuwa na nyufa ni katiba mabweni ya wanafuzi wa Shule ya Sayansi na Jamii yaliyoko Block 2 na 3 ambapo alionyeshwa na wanafunzi wanaoishi katika mabweni hayo.

  "Kujengwa kwa chuo hiki ni uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, hivyo ni lazima kuuenzi uamuzi huu kwa kuhakikisha mazingira na majengo yake yanakuwa katika hali bora", alisema Nape.

  Nape alionyesha kushangazwa kwake kuona majengo ambayo hayajatimiza miaka mitano tangu kujengwa kwake, kuanza kupata nyufa jambo ambalo alisema ni hatari kwa usalama wa wanafunzi wanaoishi katika majengo hayo.

  Mapema akizungumza na Nape, ofisini kwake, Makamu Mkuu wa UDOM Profesa, Idrisa Kikula alisema, sasa chuo hicho kina wanafunzi 20,000 ambao kati yao asilimia 50 wanalipiwa gharama zao zote za masomo na Bodi ya Mikopo.

  Profesa Kikula alisema, wakati chuo hicho kina wanafunzi pia kutoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Msumbiji, Walimu wapo kutoka nchi za Russia, India, Kenya, Nigeria,Korea, Japan, Poland na Sweden.

  Alisema, moja ya changamoto zinazokabili chuo hicho ni uhaba wa walimu kwa kuwa waliokuwepo zamani wengi ni wazee au wanaugua magonjwa mbalimbali yanayoambatana na utu uzima.

  Profesa Kikula alisema, changamoto hiyo ya uhaba wa walimu imesababisha chuo hicho kuendelea kupokea wanafunzi wasiozidi 20,000 tu, wakati kina uwezo wa kuwa na wanafunzi hadi 35,000.

  Alisema, katika kukabiliana na changamoto hiyo, chuo kimeajiri vijana zaidi ya 300, lakini ili walimu zaidi ya 200 kati ya hao 300 wapo masomoni ndabi na nje ya nchi kwa lengo la kuwa na wahadhiri wasaidizi wengi.

  Ziara ya Nape mjini Dodoma amabayo ilimalizika jana, ilianza Jumatatu wiki hii, ambapo alihudhguria sherehe za kuagwa wanafunzi wa UDOM wa mwaka wa tatu ambao ni makada wa CCM.

  Posted by: Bashir Nkoromo at Tuesday, May 24, 2011 0 Comments [​IMG][​IMG] Mtumie mwenzako Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz

  SIASA ZINAPOINGIZWA NDANI YA MABWENI CHUO KIKUU CHA DODOMA  [​IMG]
  Wanafunzi wa Sayansi ya Jamii, Chuo Chadema walizopamba katika chumba chao namba 0388 kwenye chuo hicho leo
  [​IMG]
  Upande mwingine wa chumba hicho pamepambwa kama unavyoweza kuona upande wa kushoto nembo za Chadema na Picha ya Katibu Mkuu wa Chama hicho Dk. Slaa. Kwa mujibu wa sheria wanafunzi wa vyuo, sekondari na msingi hawaruhusiwi kuendesha siasa katika maeneo hayo, ingawa wanaruhusiwa kuwa wanasiasa nje ya chuo.
  [​IMG]
  Jengo la Utawala UDOM

  Posted by: Bashir Nkoromo
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,478
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  hii picha namtumia Dokta Slaa, kumbe tunawapambanaji dam dam, sijui Nape alijisikiaje
  inabidi hawa vijana wetu wakipata matatizo tuwapiganie kwa nguvu zote ,hawa ndio future yetu
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  May 25, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ndio maana alikwenda UDOM wakati wa graduation wanaogopa wanafunzi 20,000 majority Chadema
   
 14. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #14
  May 25, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Poor Serikali ya Kikwete walisema UDOM ni mafanikio yake ataacha sifa kumbe Majengo yananyonyofoka... na kwanini anatumwa Nape?

  Kuna picha za Slaa Bwenini

  Tuesday, 24 May 2011
  NA BASHIR NKOROMO, DODOMA

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewaagiza viongozi wanaohusika kwenda kukagua majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ili kulipatia ufumbuzi tatizo la nyufa zilizoanza kujitokeza kwenye baadhi ya majengo.

  Chama pia kimewaagiza viongozi hao kukagua miundombinu ya majitaka katika baadhi ya maeneo chuoni hapo, ili ifanyiwe marekebisho na kuondokana na adha ya harufu mbaya.

  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, aliagiza hayo jana baada ya kutembelea chuo hicho na kukagua baadhi ya majengo ambayo yana nyufa. Majengo yenye nyufa ni ya
  mabweni ya wanafunzi wa Shule ya Sayansi ya Jamii yaliyoko Block 2 na 3.

  [​IMG]

  "Kujenga chuo hiki ni uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, hivyo ni lazima kuuenzi uamuzi huu kwa kuhakikisha mazingira na majengo yanakuwa katika hali bora," alisema.

  Nape alishangazwa na nyufa hizo katika majengo ambayo hayajatimiza hata miaka mitano tangu yalipojengwa, jambo alilosema ni la hatari kwa usalama wa wanafunzi.

  Awali, Makamu Mkuu wa UDOM, Profesa Idris Kikula, akizungumza na Nape, alisema chuo hicho kina wanafunzi 20,000 ambao kati yao asilimia 50 wanalipiwa gharama za masomo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.

  Profesa Kikula alisema chuo hicho kina wanafunzi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Msumbiji, na kina walimu kutoka Russia, India, Kenya, Nigeria, Korea, Japan, Poland na Sweden. Alisema chuo kina uhaba wa walimu kwa kuwa wengi waliopo sasa ni wazee na wengine wanaugua magonjwa yanayoambatana na utu uzima.

  Profesa Kikula alisema tatizo hilo limewafanya kuendelea kupokea wanafunzi wasiozidi 20,000, wakati kina uwezo wa kuwa na wanafunzi hadi 35,000. Alisema katika kukabiliana na tatizo hilo, chuo kimeajiri vijana zaidi ya 300, lakini zaidi ya 200 wapo masomoni ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuwa na wahadhiri wasaidizi wengi.

  Last Updated ( Tuesday, 24 May 2011 20:29

  Tuesday, May 24, 2011

  NAPE ATEMBELEA UDOM LEO, AAGIZA MAJENGO YENYE NYUFA YASHUGHULIKIWE HARAKA

  CCM imewaagiza viongozi wanaohusika kwenda kukagua majengo ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) ili kulipatia ufumbuzi wa haraka tatizo la nyufa zilizoanza kuitokeza kwenye baadhi ya majengo.

  Chama kimewaagiza pia viongozi hao kukagua hali ya miundombinu ya majitaka katika maadhi ma maeneo chuoni hapo ili ifanyiwe marekebisho kwa kuwa inatuamisha maji kutoka katika majengo na kusababisha adha ya harufu mbaya kwa wanafunzi, walimu na wafanyakazima,m wengine chuoni hapo.

  Maagizo hayo yalitolewa leo, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, baada ya kutembelea chuo hicho na kagua baadhi ya majengo ambapo alishuhudia baadhi ya majengo yakiwa na nyufa.

  Majengo yaliyoonyesha kuwa na nyufa ni katiba mabweni ya wanafuzi wa Shule ya Sayansi na Jamii yaliyoko Block 2 na 3 ambapo alionyeshwa na wanafunzi wanaoishi katika mabweni hayo.

  "Kujengwa kwa chuo hiki ni uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, hivyo ni lazima kuuenzi uamuzi huu kwa kuhakikisha mazingira na majengo yake yanakuwa katika hali bora", alisema Nape.

  Nape alionyesha kushangazwa kwake kuona majengo ambayo hayajatimiza miaka mitano tangu kujengwa kwake, kuanza kupata nyufa jambo ambalo alisema ni hatari kwa usalama wa wanafunzi wanaoishi katika majengo hayo.

  Mapema akizungumza na Nape, ofisini kwake, Makamu Mkuu wa UDOM Profesa, Idrisa Kikula alisema, sasa chuo hicho kina wanafunzi 20,000 ambao kati yao asilimia 50 wanalipiwa gharama zao zote za masomo na Bodi ya Mikopo.

  Profesa Kikula alisema, wakati chuo hicho kina wanafunzi pia kutoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Msumbiji, Walimu wapo kutoka nchi za Russia, India, Kenya, Nigeria,Korea, Japan, Poland na Sweden.

  Alisema, moja ya changamoto zinazokabili chuo hicho ni uhaba wa walimu kwa kuwa waliokuwepo zamani wengi ni wazee au wanaugua magonjwa mbalimbali yanayoambatana na utu uzima.

  Profesa Kikula alisema, changamoto hiyo ya uhaba wa walimu imesababisha chuo hicho kuendelea kupokea wanafunzi wasiozidi 20,000 tu, wakati kina uwezo wa kuwa na wanafunzi hadi 35,000.

  Alisema, katika kukabiliana na changamoto hiyo, chuo kimeajiri vijana zaidi ya 300, lakini ili walimu zaidi ya 200 kati ya hao 300 wapo masomoni ndabi na nje ya nchi kwa lengo la kuwa na wahadhiri wasaidizi wengi.

  Ziara ya Nape mjini Dodoma amabayo ilimalizika jana, ilianza Jumatatu wiki hii, ambapo alihudhguria sherehe za kuagwa wanafunzi wa UDOM wa mwaka wa tatu ambao ni makada wa CCM.

  Posted by: Bashir Nkoromo at bashir-nkoromo.blogspot.com

  SIASA ZINAPOINGIZWA NDANI YA MABWENI CHUO KIKUU CHA DODOMA

  [CENTER[​IMG]
  Wanafunzi wa Sayansi ya Jamii, Chuo Chadema walizopamba katika chumba chao namba 0388 kwenye chuo hicho leo

  [​IMG]
  Upande mwingine wa chumba hicho pamepambwa kama unavyoweza kuona upande wa kushoto nembo za Chadema na Picha ya Katibu Mkuu wa Chama hicho Dk. Slaa. Kwa mujibu wa sheria wanafunzi wa vyuo, sekondari na msingi hawaruhusiwi kuendesha siasa katika maeneo hayo, ingawa wanaruhusiwa kuwa wanasiasa nje ya chuo.

  [​IMG]

  Jengo la Utawala UDOM

  Posted by: Bashir Nkoromo
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  May 25, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,478
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  May 25, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Labda kuna matetemeko ya ardhi; hivi likipiga tetemeko la ardhi hapo wamejiandaa; na majengo hayo yamejengwa na nani?
   
 17. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #17
  May 25, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Tulidhani Majengo yamejengwa na Wachina...
   
 18. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #18
  May 25, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kama kawa, ni wazee wa feki feki feki Wachina ndiyo waliojenga. Unajua watanzania tunapenda mambo mazuri 'at low cost' ndiyo maana wanaoshinda zabuni nyingi za ujenzi hapa nchini kwa sasa ni wachina. Lakini pia, inawezekana ni suala la uaminifu wa watanzania wenzetu wanaosimamia miradi kwamba inawezekana wanakula na wachina. Sasa mchina lazima nae apunguze quality ya kazi ili afidie mlungula aliotoa. Hasara tunayopata ndiyo hiyo, kabla ujenzi wa barabara haujaisha utaona mashimo yameanza kujitokeza. Kabla ujenzi wa nyumba haujaisha, utaona nyufa zimeanza kujitokeza. Kama ni mradi wa maji utaona mabomba yanapasuka mara kwa mara muda mfupi tu baada ya kuuzindua. Sasa pale UDOM ndiyo balaaa. Hata mtu ambaye siyo Civil Engineer akiona yale majengo atabaini kasoro kubwa. Ninawaonea huruma vijana wetu siku tetemeko la ardhi litakapotokea, sijui itakuwaje! Eeehhh Mwenyezi Mungu tuepushe na balaa hilo.
   
 19. A

  ACHEBE JF-Expert Member

  #19
  May 25, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 348
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni,Nape alishambuliwa sana hapa Jf kwamba kilaza,hajui lolote hana uwezo wa nafasi aliyonayo.... Kafanya jambo la maana hapa kila mmoja amekimbia,tujenge utamaduni sio wa kushambulia tu bali hata kupongeza mtu akifanya vizuri.
  Hongera Nape kwa mwendo huo unakuwa msikivu sasa.
   
 20. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #20
  May 25, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  katika uongozi huu wa ccm usitegemee mradi wowote kutekelezwa kwa umakini kwani kila mradi ni"deal"ya viongozi kujinufaisha.
   
Loading...