Nyufa alizoziona Mwalimu Nyerere mwaka 1994 zinaelekea kuzibika au ndo zinaongezeka? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyufa alizoziona Mwalimu Nyerere mwaka 1994 zinaelekea kuzibika au ndo zinaongezeka?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Monasha, Apr 21, 2011.

 1. Monasha

  Monasha JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 508
  Likes Received: 295
  Trophy Points: 80
  [​IMG] HIVI karibuni Chama Cha Mapinduzi kimefanya mabadiliko ya uongozi katika sekretarieti na kamati kuu kwa kile kilichoitwa kujivua gamba.

  Tafsiri hii ya kujivua gamba ilianza kutolewa na Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akihutubia katika kilele cha sherehe za miaka 34 ya CCM mnamo Februari 5 mwaka huu.

  Akieleza haja ya CCM kujivua gamba, Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho, alibainisha kuwapo kwa mchakato wa mageuzi ya ndani ya CCM ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kushindana na kushinda katika uchaguzi ujao.

  Kutemwa kwa baadhi ya viongozi wa CCM kunatokana na viongozi hao kuhusishwa na baadhi ya kashfa za ufisadi kitu ambacho kimekuwa kikichafua chama hicho kwa muda mrefu sana.

  Kashfa hizi zimekuwa zikileta mpasuko ndani ya chama na hata kama hawatakuwa makini na kuendelea kujivua magamba mpasuko utazidi kuongezeka na hatimaye si ajabu miaka ijayo tusione CCM. Kashfa ni nyingi kwa kweli,kwa mfano sijui richmondi, Epa, Dowans n.k. Hizi zooote zinawahusu viongozi wa CCM.


  Mwalimu Nyerere aliyoana haya.

  Hali ya ufisadi ndani ya CCM iliyosababisha kutokea kwa mabadiliko hayo ilitabiriwa na Hayati Mwalimu Julius Nyerere, alikionya CCM kutoendekeza rushwa.

  Katika kitabu chake cha Nyufa chenye hotuba aliyoitoa Machi 13, 1995, Mwalimu Nyerere ametaja nyufa tano zilizoikumba nchi ambapo alisema kuwa ufa wa nne ni rushwa ndani ya CCM na serikali yake.

  Mwalimu Nyerere amebainisha kuwa chanzo cha mpasuko ndani ya CCM ni kutokana na viongozi wa chama hicho kukosa maadili na hasa pale kilipoikana misingi ya Azimio la Arusha.
  “
  Kuna miiko ndani ya Azimio la Arusha…, viongozi wetu walikutana Zanzibar wakaona Azimio la Arusha halifai, wakatutangazia na hawakuzungumzia kwamba tumekutana Zanzibar tumeona Azimio la Arusha halifai. Walikuja kimyakimya tukaona wanaanza kufanya mambo ambayo hayafanani na Azimio la Arusha. Wenye akili tukajua limekwisha hilo”, anasema Mwalimu Nyerere.

  Kwa mujibu wa Mwalimu Nyerere, hakuna serikali popote duniani inayoendeshwa bila miiko. Anazitaja nchi za Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na Japan na kusema kuwa zinaendeshwa kwa miiko.

  “Kwa hiyo nchi zote zina miiko. Hapa sasa hatuna. Wameacha miiko ya Azimio la Arusha, hawakuweka miiko mingine, sasa ni holela tu,” anasema.

  Kutokana na hali hiyo, Mwalimu Nyerere anasema kuwa imefungua milango ya rushwa ambayo awali ilikuwa imebanwa. Anakumbushia enzi za TANU ambapo licha ya kuwa na miiko ya uongozi, kulikuwa na kanuni za TANU. Moja kati ya kanuni hizo ni ile iliyorithishwa CCM inayosema, “Rushwa ni adui wa haki, sitatoa wala sitapokea rushwa”.

  “Usije ukadhani kwamba wakati wa awamu ya kwanza palikuwa hapana rushwa, ilikuwapo lakini tulikuwa wakali sana. Siku za mwanzo kabisa tulitaka watu wajue hivyo. Tukapitisha sheria kwamba mtu akila rushwa, eh kiongozi wetu anakula rushwa: anayetoa, aliyepokea … wote wanapata msukosuko,” anasema Mwalimu Nyerere.

  Akieleza sifa ya kiongozi anayepaswa kuiongoza Tanzania, Mwalimu Nyerere anasema kuwa kiongozi bora si yule anayechukia rushwa tu, bali pia awe na uwezo wa kuwaambia rafiki zake kwa kauli ambayo wataiheshimu na hawatarudia tena.

  “Sasa Tanzania inanuka rushwa. Tunataka kiongozi atakayesema; ‘rushwa kwangu ni mwiko, mwaminifu kabisa hawezi kugusa rushwa na watoa rushwa watamjua hivyo.
  “Ikulu ni mahali patakatifu, mimi sikuchaguliwa na wananchi wa Tanzania kupageuza kuwa pango la wanyang’anyi”, anasema Mwalimu Nyerere.

  Akizungumzia rushwa katika uchaguzi Mwalimu Nyerere anakumbushia enzi ya utawala wake ndani ya TANU na CCM akisema kuwa mali ingeweza kumkwamisha mgombea;
  “Zamani katika CCM na katika TANU, tunapochagua mgombea wetu kama ana mali tunamuuliza ‘hii umeipata wapi?’. Mali ilikuwa kigezo cha kupoteza sifa ya kuwa mgombea,” anasema.

  Kwa misingi hiyo kujivua gamba pekee hakutushi, tunapaswa kuwa na viongozi wenye uadilifu wa kweli, wanaochukia rushwa na jamii iwaelewe hivyo.

  Kimsingi rushwa ikiendekezwa italimong’onyoa taifa.

  Nimeona niwaletee hili wana JF ili mjue na tujue sote pamoja na kuona maoni yenu pia.
   
 2. U

  Upanga Senior Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 135
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Kumbe nyerere aliwavua gamba tanu na ccm yake miaka hiyo,lakini ccm ililivaa tena gamba kule zanzibar?
   
 3. Monasha

  Monasha JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 508
  Likes Received: 295
  Trophy Points: 80
  Huyu mzee alikuwa na uwezo wa kuona mbali sana.
  Just imagine leo hii angekuwa hai, haya madudu ya CCM angeyachukuliaje????????
   
 4. m

  mkulimamwema Senior Member

  #4
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyerere alitumia muda mwingi kukaa nchini na kusimamia watendaji wake tofauti na JK anasafiri mno nje ya nchi sasa hivi kapunguza baada ya kulalamikiwa;lakini ccm ya leo hakuna msafi wote wamejichafua nani asiye na kashifa ya rushwa,jamani tunaposema rushwa ni pamoja na rushwa ya ngono nani ambaye hajatoa au kupokea kwa ccm ya JK?
   
 5. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ema nyinyi watoto hamkupanga mawe ama hamkukimbiza magari ya ugawaji ndiyo maana mnaandika huu UPUPU wenu wa "kusimamia watendaji". Leo angekuwa hai huyu mzee na angelikuwa madarakani badala ya kukaa mbele ya kompyuta na kuandika hapa (vingeitwa vitu vya anasa kama ilivyokuwa inaitwa television) mngelikuwa "mnalangua" sigara na dawa ya mbu mitaani ama mnafukuza mwenge kwenye ofisi za CCM. Mngeishia kusoma katuni ya Abushiri na Chakubanga. Habari pekee nje ya Tanzania ingetoka XINHUA na "Amini Usiamini" kwenye gazeti la James Nhende. Shopping mngekuwa mnaenda kununua viatu vya matairi. Viatu vya kichina mngeita "raba mtoni". Nyerere mnamjua ama mnamsikia?
   
 6. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Katika hotuba ya Mwalimu Nyerere aliyoitoa Kilimanjaro hotel June 14, 1994 ambayo mdau wa libeneke ameipost kwenye you tube (Hotuba ya Mwalimu Nyerere hoteli ya Kilimanjaro June 14, 1994 (Michuzi Blog) - YouTube), mwalimu alizitaja hizi zifuatazo kama nyufa kuu nchini Tanzania;

  1. Muungano-aliona kwamba unatikisika na kuna hatari za Uzanzibari na Utanganyika na alitupa angalizo kwamba hakuna mtanganyika wala Mzanzibari. Huu aliuita ufa mkubwa kabisa, ufa wa msingi.
  2. Kupuuza puuza katiba na ambayo ndo sheria ya msingi na 3. Uongozi usiofuata sheria. Hapa alisema viongozi wanajiamulia mambo yao wenyewe bila kufuata sheria akatolea mfano mtu anapata ushauri kwa mkewa katika kuamua mambo. Watu wanaendesha nchi bila kujali sheria
  4. Rushwa (“kiongozi wetu unakula rushwa?”). Alisema, nchi ikishakua na wala rushwa, maskini hawana kitu na rushwa ya Tanzania haina aibu. Pia alisema serikali corrupt haikusanyi kodi na inatumwa na wenye mali!

  Swali ni Je, mwelekeo wa nchi hii ya Tanzania katika kuziba nyufa hizi toka mwaka 1994 tunaonaje? Je ni nyufa ipi ambayo tunaona tumejitahidi kuiziba au walau kuidhibiti isiendelee? Ni hatari kwa nchi kama tukijitathmini na kuona bado tupo katika hali ya 1994 au nyufa zimezidi kupasuka!

  Nawasilisha.
   
 7. k

  kasinge JF-Expert Member

  #7
  Dec 17, 2014
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Mwalimu alitaja nyufa kadhaa hasa rushwa, na akasema udini na ukabila vinaanza kuchepuka.
  Sina uhakika na uduni ila rushwa nimeona. Rushwa imeshamiri saana kipindi hiki cha awamu ya nne. Hadi tukaja na ka msemo 'Chukua Chako Mapema'.
  Kusema kweli kama CCM inakufa, imefia mikononi mwa mwa Kikwete. Ameshindwa kukemea rushwa, na ndani ya CCM Ukijionyesha kukemea rushwa, wewe ndo unaonekana mbaya. Ka system kamejengeka kuanzia juu kuweka Wagombea wanaowataka wao mpaka serikali za mitaa.
  Kwa Bahati nzuri wananchi wamebadili, wameliona hili. Sasa CCM hawajiandai kwa ushindi 2015, bali ni jinsi gani watafanya hujuma ili wapate kura za kutosha kwa kutumia jeshi na usalama.
  CCM itafia mikononi mwa J.K.
   
 8. brightdramx

  brightdramx Member

  #8
  Jun 28, 2016
  Joined: Feb 1, 2016
  Messages: 8
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  MWL. NYERERE ALIMAANISHA NINI HAPA??????
  “Nchi yetu ni kama nyumba mpya. Nchi changa sawa sawa na nyumba mpya. Mmeijenga vizuri mmetayarisha msingi, mkaijenga mkaimaliza. Mnafurahi. Ndipo mnaridhika nyumba imara, inapendeza. Lakini haijasukumwa. Haijatikiswa. Mara unatokea mtikisiko, ile nyumba inatikiswa.
  “ Ule mtikisiko utawaonyesheni sehemu mbovu za nyumba ile. Ilikuwa kwanza mnaiona yote ni nzuri, inapendeza. Lakini, kama unakuja msukumo wa mtikisiko wa kutosha kabisa, sasa ndipo mtakapoanza kuona maeneo mabovu ya nyumba ile na kutokea nyufa. Nyingine ndogo katika paa, kama ilikuwa ni nyumba imara, nyufa nyingine ndogo zaidi katika paa, nyingine katika dari, hata linta lililokuwako huenda likaanguka chini.
  “Lakini, kama mtikisiko ulikuwa mkubwa, mnaweza kukuta nyufa hata katika msingi: hata msingi wenyewe nao umepata nyufa! Sasa, mtakachotaka baada ya hapo, baada ya kuona hivyo, mambo mawili yanaweza kutokea. La kwanza ni kwamba ule mtikisiko utakwisha: hautakuwapo.
  “ Sasa baada ya hapo mtafanya nini? Mtaziba zile nyufa: mtaziba. Mtaziona sehemu mbovu: mtaziba vizuri sana. Kama zilikuwapo katika paa mtaziba kwenye dari, mtaziba mtatengeneza vizuri. Eh! Zilizoharibika haribika, hizo mtazitengeneza vizuri; zilikuwapo nyufa katika msingi, mtatengeneza sana, hasa zile katika msingi. Maana zile ndizo muhimu sana.
  TUNAITAKA DEMOKRASIA YETU.
   
 9. brightdramx

  brightdramx Member

  #9
  Jun 28, 2016
  Joined: Feb 1, 2016
  Messages: 8
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Tena wafanye haraka....
   
 10. M

  Makambo zali Senior Member

  #10
  Dec 6, 2017
  Joined: Sep 23, 2017
  Messages: 124
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 80
  Taifa lina nyufa kwa sasa,hizi za UDSM ni fumbo tu ambalo mwenyezi Mungu kaliweka,na kama taifa lina manabii,basi wasiishie kuzitafakari nyufa za majengo tu,bali tuangalie nyufa sehemu mbalimbali katika taifa,

  katika katiba

  utawala bora

  utawala wa sheria

  uchumi

  na mengine

  huo ufa UDSM ni kama maandishi aliyoyaona mfalme Nebukdreza ukutani,na. akatafuta wafasiri,na akammpata nabii mmoja,akamtafasiria maandishi hayo ya ukutani,sisii nasi tutafute mfasiri kuhusu nyufa hizo
   
 11. c

  chinembe JF-Expert Member

  #11
  Dec 6, 2017
  Joined: May 16, 2015
  Messages: 4,061
  Likes Received: 3,734
  Trophy Points: 280
  naam,taifa lina nyufa,hatufuati sheria za manunuzi,ndio maana tunapata majengo ya aina hii,

  hata katika kutofata sheria ikiwamo kuzuia bunge live na mikutano ya siasa,kuna ufa mkubwa japo kwa macho hatututouna,
   
 12. k

  kigogo warioba JF-Expert Member

  #12
  Dec 6, 2017
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 1,823
  Likes Received: 1,214
  Trophy Points: 280
  Sheria ya manunuzi inafuatwa wakati wa kununua wapinzani tu.! :))
   
 13. c

  chinembe JF-Expert Member

  #13
  Dec 6, 2017
  Joined: May 16, 2015
  Messages: 4,061
  Likes Received: 3,734
  Trophy Points: 280
  hahahahaaaa
   
 14. Vupu

  Vupu JF-Expert Member

  #14
  Dec 6, 2017
  Joined: Aug 1, 2016
  Messages: 1,332
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Aliyeyazindua hakatoa kauli?
   
 15. M

  Mnasihi JF-Expert Member

  #15
  Dec 6, 2017
  Joined: Oct 9, 2013
  Messages: 3,256
  Likes Received: 1,633
  Trophy Points: 280
  Yote yatapita na hata yeye atapita. Sina uhakika na utetesi na ujenzi ule kama una lengo la kutoa sadaka ya damu au ni taratibu za ujenzi wa ghorofa zilitekelezwa!
  Walizidiwa na sifa hadi zikawatia upofu na sasa ni vipofu wa macho ya nyama na ya rohoni!
   
 16. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #16
  Dec 6, 2017
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,802
  Likes Received: 2,749
  Trophy Points: 280
  Hakika kuna nyufa katika taifa:
  Chuki za kisiasa na kidini;
  Chuki ya polisi dhidi ya wananchi kwa manufaa ya chama dola;
  Chuki ya raisi dhidi ya matajiri, hata wale waliopata Mali kwa shida sana;
  Chuki ya raisi dhidi ya wazalendo wanaoamini kuwa yeye si malaika;
  Chuki ya yule was magogoni dhidi ya wale aliowaita "vilaza" ilhali ni watoto wa wazalendo "wanyonge";
  Chuki ya ccm dhidi ya wengine wenye itikadi tofauti;
  Chuki ya serikali dhidi ya haki ya kuendelea na mchakato wa mabadiliko.
  Nyufa ziko wazi na ni pana kupita kiasi. Zinaonekana katika maneno na matendo ya watawala na wanasiasa; masikini na matajiri;

  Hata ukabila siku hizi unapata kiki toka magogoni;

  Umoja wa kitaifa aliotuachia baba wa taifa uko shakani.
  Woga na hofu unaitwa nidhamu kazini;
  Utulivu na uvumilivu unaitwa amani hata pale palipo na manyanyaso ya wazi;

  Asante Kumbusho kwa kutuonyesha nyufa katika hostel za JPM. Hata hivyo, nyufa hizo ni cha mtoto ukilinanisha na zile zilizo halisi katika taifa letu.
   
 17. Msambwata

  Msambwata JF-Expert Member

  #17
  Dec 6, 2017
  Joined: Nov 20, 2017
  Messages: 1,037
  Likes Received: 1,093
  Trophy Points: 280
  Nyufaa haziwezi kutafutiwa soln maana uchwara ndio silaha yake
   
Loading...