Nyota ya uzazi inavyotesa mahusiano yangu

Baba jayaron

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
4,007
5,446
Wasalaam,

Wanajamvi jana kuamkia leo usingizi umekua mgumu kwangu kutokana na changamoto ninayopitia katika swala la mahusiano ya mapenzi.

Ikiwa ni muda mfupi toka nitengane na mke wangu tuliozaa watoto wawili kwa mapenzi yetu (japo yeye ndio aliyewahitaji mwanzoni mwa mahusiano yetu). Hali ambayo imenisumbua saana kwakua sikutegemea kupitia uzoefu wa kuvunjika kwa ndoa hasa ndoa yangu.

Shida ni kwamba kila uhusiano nilioanzisha baada ya mtafaruku wa kutengana na mke wangu nimekua nikikutana na wanawake au mabinti wanaonilazimisha niwape mimba au nizae nao kitu ambacho mimi sikifirii na hujikuta nalazimu kuwakimbia, ili nisifanye makosa kwakua wengi kati yao naona hawana vigezo.

Sasa nimepata mtoto wa kipare ambaye nililezwa sifa zake na kuonganishiawa na rafki yangu.

Huyu mpare kwakweli amekidhi vigezo vyote ambavyo mwanaume anahitaji kwa mke. Mkarimu, anaadabu, anajistiri, anajua kubembeleza, mapenzi anayaweza pia na nzuri zaidi familia yake ipo vizuri na amenieleza namna mama yake alivyoipambania ndoa yake pamoja na vituko vya baba yake. Kitu ambacho nitofauti na historia ya familia ya xwife wangu ambaye mama yake ni jino kwa jino na ndoa ilishavunjikaga kitambo.

Kiukweli ni wife material japo sio mwanamke mwenye muonekano wa kushtua, anaishi kwao japo age yake imeenda anakaribia 30, sasa ananililia na kunitolea maneno ya uchungu juu ya hitaji lake la mtoto. Maneno yake yananichoma moyo kwakua mimi sipotayari anashangaa et mimi ni mwanaume gani sitaki mtoto anajihisi kama ana mkosi.... Anajua changamoto niliyopitia anasema hataki uzoefu wangu wa nyuma anachotaka azae kwanza na mimi na yupo tayari kuzaa watoto wengi na mimi na kulea watoto wangu wa mwanzo..

Hu ni uhusiano wa tano au zaid tangu nijaribu kumsahau xwife wangu, na yote niliyavunja sababu ya kudaiwa mtoto ila kwa huyu imenigusa kidogo kutokana na haiba yake, namna anavyojiona hana bahati kutokua na mtoto mpaka umri huo.

Sasa nisaidieni ndugu zangu kama anauzazi, je ni mpe mimba au naye ni mpotezee?
Maana uhusiano wetu ndo kwanza una wiki moja japo yeye anafahamu familia yangu before alisomaga na mdogo angu.
 
We jamaa acha kuzingua basiii...

Kama hutaki watoto si utongoze watoto wa chuo? Ama tongoza vibinti vya mtaani vyenye age 20 mpaka 23.

Hivi kwa akili yako uwe na uhusiano na mdada wa 28+ years halafu asitake mtoto? Hauko serious kijana.

Kama hutaki mtoto basi tongoza visichana vidogo ama mijimama ilozaa na haitaki kuzaa tena. Ila hapo katikati ya 28-33 utategeshewa dakika 0.
 
Wiki moja mapema sana, nilikua na mahusiano na mdada zile wiki mbili zilikua za moto. Baada ya mitombo miwili mitatu kila mtu hana ata muda wa ku text
 
Back
Top Bottom