Nyota ya uzazi inavyotesa mahusiano yangu

Ungempuzika kwanza mahusiano mpaka u heal break up na uache kutesa wanawake kihisia then ndio uje utafte mahusiano mapya ukiwa umepona. Bila hivo utakuwa na 100 ka wakukusahaulisha ila maumivu yatakuwa pale pale
Mi hua nawaambia situation niko nayo kwamba inahitaji muda kufanya maamuzi ya ndoa ama kuzaa.... Nadhini wenyewe katika kuniaminisha kwamba naweza pendwa na kujaliwa wanakimbilia kwenye kubeba mimba kitu ambacho sitaki kukisikia kabisa kwa sasa.
 
We jamaa acha kuzingua basiii...

Kama hutaki watoto si utongoze watoto wa chuo? Ama tongoza vibinti vya mtaani vyenye age 20 mpaka 23.

Hivi kwa akili yako uwe na uhusiano na mdada wa 28+ years halafu asitake mtoto? Hauko serious kijana.

Kama hutaki mtoto basi tongoza visichana vidogo ama mijimama ilozaa na haitaki kuzaa tena. Ila hapo katikati ya 28-33 utategeshewa dakika 0.
Nilikua na mwanafunzi wa mwl nyerere age 23 naye akawa anataka mtoto na kuishi kwangu kabisa alikua anakuja kwa speed ya sgr nikapita kushoto.

Pengine ni aina ya wanawake nawachagua mimi ni tofauti na unaowachagua wewe.
 
Wasalaam,

Wanajamvi jana kuamkia leo usingizi umekua mgumu kwangu kutokana na changamoto ninayopitia katika swala la mahusiano ya mapenzi.

Ikiwa ni muda mfupi toka nitengane na mke wangu tuliozaa watoto wawili kwa mapenzi yetu (japo yeye ndio aliyewahitaji mwanzoni mwa mahusiano yetu). Hali ambayo imenisumbua saana kwakua sikutegemea kupitia uzoefu wa kuvunjika kwa ndoa hasa ndoa yangu.

Shida ni kwamba kila uhusiano nilioanzisha baada ya mtafaruku wa kutengana na mke wangu nimekua nikikutana na wanawake au mabinti wanaonilazimisha niwape mimba au nizae nao kitu ambacho mimi sikifirii na hujikuta nalazimu kuwakimbia, ili nisifanye makosa kwakua wengi kati yao naona hawana vigezo.

Sasa nimepata mtoto wa kipare ambaye nililezwa sifa zake na kuonganishiawa na rafki yangu.

Huyu mpare kwakweli amekidhi vigezo vyote ambavyo mwanaume anahitaji kwa mke. Mkarimu, anaadabu, anajistiri, anajua kubembeleza, mapenzi anayaweza pia na nzuri zaidi familia yake ipo vizuri na amenieleza namna mama yake alivyoipambania ndoa yake pamoja na vituko vya baba yake. Kitu ambacho nitofauti na historia ya familia ya xwife wangu ambaye mama yake ni jino kwa jino na ndoa ilishavunjikaga kitambo.

Kiukweli ni wife material japo sio mwanamke mwenye muonekano wa kushtua, anaishi kwao japo age yake imeenda anakaribia 30, sasa ananililia na kunitolea maneno ya uchungu juu ya hitaji lake la mtoto. Maneno yake yananichoma moyo kwakua mimi sipotayari anashangaa et mimi ni mwanaume gani sitaki mtoto anajihisi kama ana mkosi.... Anajua changamoto niliyopitia anasema hataki uzoefu wangu wa nyuma anachotaka azae kwanza na mimi na yupo tayari kuzaa watoto wengi na mimi na kulea watoto wangu wa mwanzo..

Hu ni uhusiano wa tano au zaid tangu nijaribu kumsahau xwife wangu, na yote niliyavunja sababu ya kudaiwa mtoto ila kwa huyu imenigusa kidogo kutokana na haiba yake, namna anavyojiona hana bahati kutokua na mtoto mpaka umri huo.

Sasa nisaidieni ndugu zangu kama anauzazi, je ni mpe mimba au naye ni mpotezee?
Maana uhusiano wetu ndo kwanza una wiki moja japo yeye anafahamu familia yangu before alisomaga na mdogo angu.
Yani week moja umeshaji verify kwamba huyo ni wife material na kila kitu mmejuana!

Wasichana wa kipare japo ni dada zangu ila kwa hilo hapana 😅~in JPM vocals!
 
we jamaa unaanzisha mahusiano kwanini? ili umsahau ex-wife wako au ili kuendeleza familia.... fumbua hilo fumbo kwanza.
 
Maana uhusiano wetu ndo kwanza una wiki moja japo yeye anafahamu
Wiki moja!!

Bado ni mapema sana.

Kaa naye, zungumza naye kwa kina, kubaliana naye kuwa nawe pia wahitaji watoto, ila ni wajibu wake kusubiria wakati sahihi, hasa baada ya kuwa tayari mko katika ndoa, na mahusiano yenu yana muda wa kutosha, kwa sasa mjipe muda zaidi , nina hakika ukizungumza naye kwa dhati atakuelewa na atafuata kile unachotaka.
 
Back
Top Bottom