Nyota ya Hichilema yazidi kung'ara , aitwa Bunge la Marekani , World Bank , aonana pia na maofisa wa EU na IMF

Tumpe mda kwanza
Niliwahi tabiri kitu kama hichi hata kwa nchi yetu:

Mwulize Hangaya akwambie nani kalamba dume kwa kwenda UN.

Hichilema katimba huko akitumia Qatar Airways na delegation ya mtu 3:

Zambia’s President leaves for New York on commercial flight with three delegates | The Citizen

Hangaya na dreamliner bila shaka moja Msigwa ndani na timu ya wawekezaji wa ndani kwenda kukutana na mwekezaji Mange.

Hangaya kaenda kusoma takwimu za Corona za UN, hana jipya, hana sera wala agenda; kapuuzwa.

Hangaya kakumbwa na aibu ya karne ya kudaiwa haki na demokrasia visivyokuwapo nchini:

View attachment 1952379

Hichilema huko ndiyo habari ya mjini. Kama vipi hata mkijinyonga haitakuwa mbaya sana.

Tanzania ya kuheshimiwa ilikuwa hii:

View attachment 1952382

Eti Tanzania ni ile ile. Tanzania ile siyo hii.

Mnakera!
Hapana unatenda dhambi mkuu, alienda na Emirates
 
Hawanaga urafiki mzuri hao watu, ukiwa na urafiki nao mwisho wako lazima uwe wa hasara...
 
View attachment 1952325

Wakati viongozi wengine kutoka nchi za kidikteta barani Africa wakirejea makwao mikono mitupu , kutokana na kupuuzwa na Jumuiya za kimataifa kwa sababu ya unyama unaotendwa nchini mwao na uminyaji wa Demokrasia na haki za binadamu , Rais wa Zambia Mh Haikainde Hichilema kwake mambo ni tofauti kabisa .

Hichilema yeye baada ya kutoka WHITE HOUSE , akaitwa bunge la USA kwenye kamati ya mambo ya nje ya seneti , kama haitoshi ameitwa World Bank , akavutwa pia kuonana na maofisa wa juu wa EU , na kwa kumalizia ametinga IMF .

Mungu ibariki Zambia

Mkuu you have no idea how crafty wazungu walivyo, wasikie kwenye radio na luninga, usiombe uingie kwenye kumi na nane zao,baadhi yetu tunawajua vizuri walivyo, especially malengo yao kuhusu bara la Afrika na viongozi wake ambao wanaonyesha dalili za kukosa msimamo dhabiti watakuchezea kisaikolojia mpaka ujute kuzaliwa.

Yaani hata hamjiulizi inakuwaje kiongozi wa Zambia anafuatwa fuatwa na IMF,World Bank, EU nini sijui, kumbuka genge lote hilo lengo lao ni moja tu, nalo ni kutaka kuiitwisha mzingo wa madeni Zambia kwa kumulubuni na Mickey Mouse stories za uongo na kweli mpaka atajikuta anaingia mkenge.

Cha ajabu hapa naona baadhi ya Waswahili wanafurahi sana Hichilema kukaribishwa White House, yaani hawana habari kwamba alikaribishwa huko kwenda kulubuniwa na maafisa wa propaganda ndani ya WH kuhusu ubaya wa ujio wa Wachina barani Afrika, watamshauri afanye juu chini kuachana na Wachina kabisa, badala yake ashirikiane na Merikani kwenye masuala ya kiuchumi, maendeleo possibly na kijeshi. Sio siri kwamba hivi sasa US hiko overly determined kuhujumu ujio wa Wachina Barani Afrika wako radhi kufanya lolote ili kutekeleza azma yao. Hata Hichilema akienda kuhutubia Congress watamzonga na adithi hizo hizo za kumpa somo kuhusu ubaya wa ujio wa Wachina barani Afrika - hakuna kitu cha maana kita zungumuzwa hapo zaidi ya ku-demonize Wachina na viongozi wao, haya mambo ya kusema kakaribishwa White House na kwenye Bunge eti "kutokana na yeye kuheshimu masuala ya haki za binadamu na demokrasia" hoja hiyo haina ukweli wowote - hivi American Administration (Govt) ingewezaje kutathimini uongozi wa Hichilema ndani ya mwenzi mmoja tangu ashinde kiti cha Uraisi nchini Zambia kwamba yu balabala - hoja nyingine za Waswahili zina shangaza sana - ukisoma baadhi ya maoni hapa unaona wazi wazi kwamba yana lengo la kuusema vibaya uongozi uliopo Madarakani Tanzania, ni hilo tu.

Ushauri wangu Hichilema hasijisahau sana kwa kudhani Wazungu wana nia njema ya kuiendekeza Zambia kiuchumi,viwanda na infrastructure - taifa pekee Duniani lenye lengo zuri la ku-help Africans to help themselves ni Uchina tu, wengine ni wasanii.
 
Wewe siyo mtu mzuri hata kidogo. Unajua unawaumiza sana mioyo ujumbe wa Tanzania ukizingatia walifanya kampeni kubwa sana ili rais Samia aalikwe sehemu kama hizo?
Mbona mnashangaza sana - nani kawambieni Rais Samia alikwenda Merikani kutembeza bakuli la kuomba misaada!!!

Mbona mnataka kuchukulia mkutano huo kama ulikuwa una lengo la kukutanisha Donor Countries na third World?
 
kuna watu ukiwaona wanakupenda sana rudi kwenye drawing board ukacheki umebugi wapi,
Asante.
 
Mbona mnashangaza sana - nani kawambieni Rais Samia alikwenda Merikani kutembeza bakuli la kuomba misaada!!!

Mbona mnataka kuchukulia mkutano huo kama ulikuwa una lengo la kukutanisha Donor Countries na third World?
Kwi Kwi Kwi
 
Ushauri wangu Hichilema hasijisahau sana kwa kudhani Wazungu wana nia njema ya kuiendekeza Zambia kiuchumi,viwanda na infrastructure - taifa pekee Duniani lenye lengo zuri la ku-help Africans to help themselves ni Uchina tu, wengine ni wasanii.
Umeanza vizuri ila ukaharibu mwishoni ukaharibu kwa kusema wachina wana nia nzuri na waafrika. Wachina ni wezi na matapeli wenye sura ya upole tofauti na mabeberu. Wazambia wako hoi kwa madeni ya mchina. Isitoshe mchina anaendelea kujimilikisha nchi ya Zambia. Hadi kwenye miji midogo mchina anajenga malls ambazo kiukweli zinawavuruga sana wazawa kwa maana ya unfair competition. Hichilema awe mjanja kucheza karata yake vizuri ili aiondoe Zambia kwenye mikono ya wachina. Kwenye kampeni zake HH alisema atadili na madeni kwanza.
 
Here we go again - emulating western dirty propaganda about China and her leaders.

Mambo mengine bwana-yaani waswahili wanaona mikopo ya mabeberu ni balabala lakini mikopo ya Wachina ni hatari - kisa? Vyombo vya habari vya magharibi vimekaririsha Waafrika kuami ni hivyo mabeberu are still stuck in by gone cold war mentality where western Nations were preaching evil of communism/socialism and blessing of CAPITALISM - ndicho kinacho endelea mpaka sasa mabeberu wana tisha tisha waafrika kuhusu ujio wa Wachina barani Afrika.
 
Wewe pia una propaganda. Tembelea Zambia ujionee Mchina aliyoyafanya ndo uje na utetezi wako. Halafu tumia lugha moja unapoandika comment.
 
View attachment 1952325

Wakati viongozi wengine kutoka nchi za kidikteta barani Africa wakirejea makwao mikono mitupu , kutokana na kupuuzwa na Jumuiya za kimataifa kwa sababu ya unyama unaotendwa nchini mwao na uminyaji wa Demokrasia na haki za binadamu , Rais wa Zambia Mh Haikainde Hichilema kwake mambo ni tofauti kabisa .

Hichilema yeye baada ya kutoka WHITE HOUSE , akaitwa bunge la USA kwenye kamati ya mambo ya nje ya seneti , kama haitoshi ameitwa World Bank , akavutwa pia kuonana na maofisa wa juu wa EU , na kwa kumalizia ametinga IMF .

Mungu ibariki Zambia
Hizi hakili buana sijui vp tu , nyota inang'aa au wanamhitaji ili kum-convert aendane na matakwa yao

Turuhusu mda ufanye yake
 
Back
Top Bottom