Nyota ya binadamu ni nini na ina maana gani kwenye maisha yake?

Tairus

JF-Expert Member
Mar 13, 2013
676
1,055
Nianze kwa kutanguliza salamu

Nina imani kubwa kuwa umesikia kihusu maswala yahusuyo nyota ya binadamu mara nyingi.Swali la msingi apa ni kuwa kuna uhalisia wowote katika hili.

Imani yangu ni kuwa hivi vitu havina uhalisia bali ni sisi binadamu tumejijengea mazoea tuu na mwisho wa siku tunapotea.

Iko ivi watu wanaendekeza ushirikina kwa miavuli ya kusafisha nyota.
Unambiwa nyota yako imechafuka unaamini ni sawa na mtu akikuwambia flani kakuloga bila uthibitisho.

Nyota ni nini..Tunaambiwa ni ule mvuto au nuru binadamu anazaliwa nayo.
Tunaambiwa nuru hii hufifia na kung'aa
Ikififia una hali mbaya na ikingaa una hali nzuri.

Tunaambiwa kuwa kila unapompa mganga nafasi ya kuipitia nyota yako na kuisafisha unampa pia uwezo wa kuichafua kwa maana ya kuamisha baraka zilizokuwa kwa ajili yako na kumuamishia mteja wake mwingine anapokuja.
Kwa hali hiyo kila siku utakuwa unarudi kwa kalumanzira na yeye anafanya kuwapanga tuu.

Pia tuambiwa tuoe wanawake ambao nyota zetu zinaendana lakin bado kila siku watu wanaachana.

Baada ya hayo turudi kwenye mada.
Mganga ni nan na nan kampa uwezo wa kucheza na nyota za watu...je ni kweli ushawai kusafisha nyota na ukafanikiwa.
Kama Mungu alitaka uwe mtu fulani toka mwanzo kwa nin akubal mtu mwingine aharibu.

Utakubaliana na mimi kuwa kinachofanyika ni kiini macho tuu nyota ya mtu ipo na hakuna wa kuisafisha wala kuichafua sababu alipangalo Mungu mwanadamu hawezi pangua.

Nakaribisha wataalamu wa haya maswala kwa uchambuzi zaidi yakinifu.

Tairus.
 
Nyota ni mipango ya Mungu, familia uliozaliwa, akili yako, na muonekano wako
 
Imani yangu ni kuwa hivi vitu havina uhalisia bali ni sisi binadamu tumejijengea mazoea tuu na mwisho wa siku tunapotea.

Utakubaliana na mimi kuwa kinachofanyika ni kiini macho tuu nyota ya mtu ipo na hakuna wa kuisafisha wala kuichafua sababu alipangalo Mungu mwanadamu hawezi pangua.

Maelezo yako yanajikanganya yenyewe yakibainisha nyota ni vitu vya kufikirika lakini tena kama vitu halisi kuwa mganga anaweza kucheza nayo.
 
Binadamu huwa haamini hadi yamkute.Ila kama bado unapumua NEVER SAY NEVER
 
Hilo ni jambo la Ki-biblia kabisa . kama wewe ni mkristo,tafuta mafundisho ya mchungaji mmoja wa KKKT anaitwa Mchungaji Wiliamu Kopwe ni Phd.soma vitabu vyake .Utafunguka na kuelewa sana juu ya hii maada.Sema wachawi na washirikina waliiijua hii siri mapema ndiyo maana wame-tuovertake. Na ni kweli pia nyota yako inaweza chafuliwa na wachawi,ila pia haiwezi kusafishwa kwa kikamilifu na waganga ila damu ya YESU
 
Back
Top Bottom