Naomba kuuliza wataalamu wa jamii check. Maisha yangu yote naamini kuwa nyongo ya mamba ni sumu, lakini kuna bosi wangu mmoja tumebishana vikali akidai kuwa si sumu bali ni nyongo tu kama ya binadamu. Ukweli ni upi?

- Tunachokijua
- Kwa miaka kadhaa nyongo ya mamba imekuwa ikitajwa kuwa chanzo cha vifo vya watu, ambapo watu wengi wakaamini kuwa nyongo ya mamba ni sumukwa binadamu. Januari 2015 nchini Msumbiji watu 75 walitangazwa kufariki ambapo redio zilitangaza vifo hivyo kusababisha na nyongo ya mamba.
Hata hivyo, JamiiForums baada ya kupitia maandiko kadhaa ya wataalamu akiwemo Profesa Norman Nyazema ambaye ni mbobezi wa fani ya famasia, amekanusha imani maarufu hii baada ya kufanya utafiti wa kina wa jambo hilo.
Prof Nyazema, ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Limpopo nchini Afrika Kusini, amethibitisha kuwa nyongo ya mamba haina sumu kabisa, hata hivyo huwa inakausha na kuuzwa China kama dawa ya kuongeza nguvu za kiume.
Katika wasilisho la utafiti wake alisema iko miti ambayo ina sumu kali na hutumiwa na waganga wa kienyeji katika kuua watu katika matukio ya kunywa pombe kwa Pamoja ambayo ndio matukio yanayoripotiwa mara kwa mara.
Hata watu waliokufa nchini Msumbiji baada ya kunywa pombe yenye sumu, pombe waliyotumia ilithibitisha kuwa sumu iliyokuwa kwenye pombe ile haikuwa nyongo ya mamba.