Dragon Kulala
Member
- Jan 24, 2020
- 53
- 80
Ndugu Watanzania wenzangu hasa watumishi, naombeni mnitoe ushamba kwa swali nililouliza.
Kimsingi kumekuwa na sintofahamu ya miaka takribani mitano sasa kwa watumishi wa umma kutoongezewa mishahara kwa kisingizio kwamba wakubwa wanajenga/wananyoosha nchi na kutatua kero za Watanzania hasa wanyonge.
Hivi sisi watumishi siyo Watanzania wanyonge eeh! Na huo unyonge wa baadhi ya Watanzania mnaupima vipi nyie wakubwa?
Kwa kipindi hiki chote gharama za maisha zinapanda ila mkubwa amegoma kupandisha mishahara, unatupeleka wapi mheshimiwa?
Nipende kiwaeleza bayana ninyi wakubwa, mmefanya watumishi wengi tunaandamana mioyoni, na hii madhara yake ni makubwa!
Maisha tunayoishi sisi, ninyi mkiambiwa mysishi hata siku tano, wallaih mnakufa!
Tuna shida mno. Ifike mahala mambo yaliyopo kwa mujibu wa sheria,taratibu, kanuni na pengine Katiba, yatekelezwe jinsi yalivo! Kwanini awamu zingine zote mishahara ilikuwa inaongezwa, awamu hii yenyewe ni nini hasa kinachoipa kiburi?
Iko juu ya sheria? Ninyi mnatembea na maburungutu ya pesa, mnagawa, mnatoa misaada vizuri, kwani sisi hatutaki tutoe hata elfu kumi kuwasaidia watu au kuchangia maendeleo ya nchi yetu?
Mbona pesa hizo muwe nazo ninyi tu?
MNAZIPATA WAPI, MNAZIPATAJE, MTAZIREJESHAJE KAMA MNAKOPA?
LAZIMA MJUE, WATANZANIA SIYO WAJINGA KWA KIASI MNACHOFIKIRI!
Sent using Jamii Forums mobile app