Nyongeza ya Mishahara: Ni hisani ya Rais, haki ya Watumishi au ni takwa la kisheria kwa Watumishi?

Dragon Kulala

Member
Jan 24, 2020
51
125
Ndugu Watanzania wenzangu hasa watumishi, naombeni mnitoe ushamba kwa swali nililouliza.

Kimsingi kumekuwa na sintofahamu ya miaka takribani mitano sasa kwa watumishi wa umma kutoongezewa mishahara kwa kisingizio kwamba wakubwa wanajenga/wananyoosha nchi na kutatua kero za Watanzania hasa wanyonge.

Hivi sisi watumishi siyo Watanzania wanyonge eeh! Na huo unyonge wa baadhi ya Watanzania mnaupima vipi nyie wakubwa?

Kwa kipindi hiki chote gharama za maisha zinapanda ila mkubwa amegoma kupandisha mishahara, unatupeleka wapi mheshimiwa?

Nipende kiwaeleza bayana ninyi wakubwa, mmefanya watumishi wengi tunaandamana mioyoni, na hii madhara yake ni makubwa!

Maisha tunayoishi sisi, ninyi mkiambiwa mysishi hata siku tano, wallaih mnakufa!

Tuna shida mno. Ifike mahala mambo yaliyopo kwa mujibu wa sheria,taratibu, kanuni na pengine Katiba, yatekelezwe jinsi yalivo! Kwanini awamu zingine zote mishahara ilikuwa inaongezwa, awamu hii yenyewe ni nini hasa kinachoipa kiburi?

Iko juu ya sheria? Ninyi mnatembea na maburungutu ya pesa, mnagawa, mnatoa misaada vizuri, kwani sisi hatutaki tutoe hata elfu kumi kuwasaidia watu au kuchangia maendeleo ya nchi yetu?

Mbona pesa hizo muwe nazo ninyi tu?

MNAZIPATA WAPI, MNAZIPATAJE, MTAZIREJESHAJE KAMA MNAKOPA?

LAZIMA MJUE, WATANZANIA SIYO WAJINGA KWA KIASI MNACHOFIKIRI!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
13,424
2,000
Katiba ya nchi inavunjwa na mkuu wa nchi mchana kweupe mbele ya media, kama alisema yule jamaa 'hata akishinda kesi' hawezi kuwa mtumishi wa umma ina maana hata maamuzi ya mahakama kwake hayana maana.

Kimsingi nchi haiongozwi kwa misingi ya utawala wa sheria bali kwa hisia na mawazo ya mtawala anaetawala kimabavu jinsi anavyotaka na asiependa kupingwa wala kuelekezwa.
 

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
6,179
2,000
Hivi zile arrears za watumishi hasa walimu waliopandishwa madaraka na kuporwa kisha kupandishwa tena April mosi nayo yanangoja kauli yake kulipwa?

Na he, ni nani hasa anahusika na fedha za nauli ya likizo kwa walimu kati ya wizara ya elimu, tamisemi na wizara ya fedha? Nauliza haya kwasababu wife anadai likizo kwa miaka mitatu tangu 2015 hajalipwa!

Natamani niijue Wizara inayohusika nikakiwashe hukohuko!
 

mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,342
2,000
Kweli mwanadamu ni kiumbe wa ajabu sana. We unadai nyongeza wakati kuna watu lukuki wenye vyeti vyao na usomi wao hawajawahi hata kuitwa usaili wowote hata wa kuosha maiti?

Tuhurumiane jamani. Hebu tuombe Mola awakumbuke hao ambao wanasota na vyeti halali bila kazi wala mtaji wa kuanzisha biashara
 

Dragon Kulala

Member
Jan 24, 2020
51
125
We MANGATARA unachowaza hakina tija wala correlation yoyote na uhalisia. Kwani kipindi Mishahara inapandishwa na viongozi wa awamu zingine, hao unaowaongelea hawakuwapo nchini?

Jenga hoja kuntu, taratibu, sheria, kanuni na miongozi inataka mishahara ipandishwe baada ya hao unaowataja ww kuwa wameisha? Mbona kwako hujaacha kula ili wanaolala na njaa mitaani wapatiwe ufumbuzi wa jinsi gani watapata chakula?

Mbona hujajipunguzia matumizi yako ili omba omba wote wapate maisha bora kwanza?acha zako ww, usitutibue nyongo, alah!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Pawa chilonda

Senior Member
Aug 13, 2017
171
250
Sio sheria
Sio Katiba
Sio rules
Sio regulations

Inayozungumzia nyongeza upungufu wa kisheria huo inabidi ujifungie ndani usiku huu Lia Sana kwanini ulizaliwa MASIKINI na sasa umeajiriwa na serikali ya wanyonge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom