Nyongeza kiduchu mishahara; nani hasa adui wa wafanyakazi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyongeza kiduchu mishahara; nani hasa adui wa wafanyakazi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by SILENT ACtOR, Jul 30, 2011.

 1. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Kumekuwa na mjadala juu ya nyongeza kiduchu wanazopewa wafanyakazi pamoja na ugumu wa maisha. Waziri Ghasia (Utumishi wa umma) amekaririwa na vyombo vya habari akisema maamuzi ya nyongeza iliyotolewa na serikali yamewashirikisha na kuridhiwa na viongozi wa TUKTA. Hata alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa asilimia ngapi imeongezwa alijibu waulizwe TUKTA wanafahamu kila kitu. Upande wa pili tumemsikia Mgaya (naibu katibu mkuu TUKTA) akisema, kwanza anapinga kiwango kidogo kilichoongezwa na pili wanasubiri waraka rasmi ili watoe tamko. Mchezo wa paka na panya!

  Kwangu mimi adui mkuu wa wafanyakazi ni TUKTA maake wanatumikia mabwana wawili(wafanyakazi na serikali). Hatujasahau siku ya sherehe za mei mosi jinsi mwenyekiti wa TUKTA alivyowapasha wafanyakazi kuwa ule ugomvi kati yao (TUKTA?) na Jakaya uliosababishwa na wafitini (wafanyakazi?) sasa umekwisha na mambo ni safi! Mpaka sasa najiuliza mambo safi ni yapi au ndio nyongeza hii? Siku hiyo (mei mosi) Kikwete alifurahia sana msemo huo hata akaurudia katika speech yake make alijua wafanyakazi habari yao kwishnei!

  Jambo lingine la ajabu ni TUKTA kujidai haijui kinachoendelea kuhusu mishahara, kumbe wameshakubaliana na serikali. Kwa mtaji huu tukubali tu kwamba bado hatujapata watu makini wa kutuongoza kudai haki zetu. Hawa waliopo yaelekea wameshawekwa mfukoni, kazi yao ni kupoza makali yetu pale tunapotaka kudai haki zetu kwa kutupa ahadi hewa wakishirikiana na serikali. Tumaini letu ni nini baada ya yote haya? Tutafakari pamoja.
   
 2. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,829
  Trophy Points: 280
  TUCTA wahuni, hakuna cha waraka. salary slip za wafanyakazi zinatosha yeye kutoa tamko. That could be a legal document to base your argument
   
 3. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,062
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Haya ndiyo matatizo ya njaa. Wakati mwingine hukubali kuwa viongozi wa CCM hupenda njaa na ujinga viendelee Tanzania ili waweze kufanya watakayo. Hakuna la ajabu hapo: kiongozi wa TUKTA ameahidiwa fedha zaidi kwa mukabala wa kuacha madai ya wengi. Ulidhania kama hakuahidiwa chochote, na yeye na wanawe wana njaa kama wengine, angekubali mapatano hayo?
  Haiingii akilini!
   
 4. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  This is a world wide conspiracy againts the workforce,wala sio tatizo la Tanzania tu.Nia ni ku-demorolize the workforce.Ni tatizo la kimfumo, na kwa vile watu wengi wana very little idea of what is going on, kutatua tatizo hili is next to impossible.
   
 5. m

  mwalimu_salum Member

  #5
  Jul 31, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Imefika mda wafanyakazi tufanye kazi kulingana na kile tunachokipata,vinginevyo tutakua tunasweat,tunaumia na hakuna anaetujali.
   
Loading...