Nyoka wanaopaa kufanyiwa uchunguzi Marekani

BA-MUSHKA

Member
Nov 22, 2010
66
2
Nyoka wanaoweza kupaa angani wanafanyiwa utafiti kujua wanapaa kwa nguvu ipi.
Source: CNN 24/Nov/2010
 
Ba-Mushka,

Mbona kupaa kwa kwaanzia juu na kutua chini? Mi nilitegemea kuona wakipaa kuanzia chini na kwenda juu.
 
JituParaTupu, kumbe umewaona, wanauwezo mkubwa wa kuruka sehemu moja hadi nyingine, usiombe ukutane nao.
 
Mkuu:

Hawa hawapai (Take off) ila wanaruka na kutuka chini. Gravitation inafanya kazi.

Nafikiri watakuwa wanatumia umbo la mgongo wa nyoka kukusanya nguvu kama Spring na kuziweka pamoja na baadaye wanaziachia na hiyo inawarusha mbali na baadaye wanaanza kutua. Ndiyo maana kabla ya kuruka, wanajikusanya kwa nyuma. Ni sawa na binadamu au Paka akitaka kuruka, anajikusanya kwa kuwa kama anachuchumaaa na hapo anaachia SPRING na kuruka.

Mwisho wanasema hawa nyoka si hatari kwa binadamu.

Last edited by a moderator:
Wasisahau kuunganisha pia wale wenzetu wanaopaa kwa ungo hapa kwetu, hua wanapata wapi petroli??????????
 
Ba-Mushka,

Mbona kupaa kwa kwaanzia juu na kutua chini? Mi nilitegemea kuona wakipaa kuanzia chini na kwenda juu.

huyo nyoka anapaa au anaruka kutoka mti mmoja kwenda mwingine? ka mjuzi pori ndo kana paa but nyoka mhhhh! labda sijui maana ya kupaa
 
Nyoka wanaoweza kupaa angani wanafanyiwa utafiti kujua wanapaa kwa nguvu ipi.
Source: CNN 24/Nov/2010

Nyoka wa aina hii si wageni, walikuwapo tangu zamani. Hata nakumbuka bibi yetu alikuwa akitusimulia hadithi fulani za nyoka hao ambao walikuwa wakidhuru watu kwa kuwang'ata kichwani. Na watu wakagundua njia ya kuwatega kwa kujitwisha kichwani uji wa moto ambao akijitumbukiza tu basi ndiyo mwisho wake.
 
Wasisahau kuunganisha pia wale wenzetu wanaopaa kwa ungo hapa kwetu, hua wanapata wapi petroli??????????

ha ha ha ha! Umenichekesha sana. Kweli wafanyie kazi ili kama vipi ng'ambo tuwe tunaenda na ungo tuokoe gharama na muda.
 
Mkuu,

huyu nyoka anaitwa KOBOKO au Black Mamba. Huyu anatabia ya kusimamia almost Mkia na kuanza kwenda kwa speed kali sana. Akikuwa mara nyingi huwa anaenda mbali sana na watu. Tatizo ni pale anapokwenda na kujenga makazi yake karibu na njia za porini kutoka kijiji kimoja kuja kijiji kingine.

Hapa kwetu ilishawahi kutokea hivyo. Nyoka aliweka makazi kwenye njia pori kutoka kitongoji cha kijiji chetu kwenda Sikonge wilayani. Kulikuwa kuna barabara ila inabidi uzunguke na hivyo watu walikuwa wakipita hiyo njia. Huyu nyoka alikuwa na tabaia ya kukaa juu ya mti na mtu akipita chini, anachukulia kama umekuja kumchokoza kwenye makazi yake. Anakushukia na kukutwanga akiwa juu. Ila si kuwa anaruka, laa hasha, yeye anakuwa bado kashikilia tawi kwenye mkia na kichwa kinaning'inia chini.

Dawa yake kweli ilikuwa hiyo. Mama mmoja jasiri alichukua Chungu na ndani kuna vitu kama Pumba na takataka nyingine zinazotunza moto wa hiyo liquid. Anabandika chungu kichwani na kujipitisha chini ya mti. Nyoka akishuka kugonga, kwishieni.
Nyoka wa aina hii si wageni, walikuwapo tangu zamani. Hata nakumbuka bibi yetu alikuwa akitusimulia hadithi fulani za nyoka hao ambao walikuwa wakidhuru watu kwa kuwang'ata kichwani. Na watu wakagundua njia ya kuwatega kwa kujitwisha kichwani uji wa moto ambao akijitumbukiza tu basi ndiyo mwisho wake.
 
Mkuu,

huyu nyoka anaitwa KOBOKO au Black Mamba. Huyu anatabia ya kusimamia almost Mkia na kuanza kwenda kwa speed kali sana. Akikuwa mara nyingi huwa anaenda mbali sana na watu. Tatizo ni pale anapokwenda na kujenga makazi yake karibu na njia za porini kutoka kijiji kimoja kuja kijiji kingine.

Hapa kwetu ilishawahi kutokea hivyo. Nyoka aliweka makazi kwenye njia pori kutoka kitongoji cha kijiji chetu kwenda Sikonge wilayani. Kulikuwa kuna barabara ila inabidi uzunguke na hivyo watu walikuwa wakipita hiyo njia. Huyu nyoka alikuwa na tabaia ya kukaa juu ya mti na mtu akipita chini, anachukulia kama umekuja kumchokoza kwenye makazi yake. Anakushukia na kukutwanga akiwa juu. Ila si kuwa anaruka, laa hasha, yeye anakuwa bado kashikilia tawi kwenye mkia na kichwa kinaning'inia chini.

Dawa yake kweli ilikuwa hiyo. Mama mmoja jasiri alichukua Chungu na ndani kuna vitu kama Pumba na takataka nyingine zinazotunza moto wa hiyo liquid. Anabandika chungu kichwani na kujipitisha chini ya mti. Nyoka akishuka kugonga, kwishieni.

huyo nyoka ni noma ukigongwa nae huchukui mda unasepa
 
Hahahaha Sikonge bana....hiii hadithi imeenea sana Unyamwezini na Usukumani. Ni folklore flani hivi......Nakumbuka wakati niko mdogo mama yangu alikuwaga akinisimulia hii stori....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom