Nyoka ni alama ya Tiba na Uponyaji ndo maana taasisi nyingi za Tiba hutumia nembo ya Nyoka

Nyoka ni alama ya Tiba na Uponyaji ndo maana taasisi nyingi za Tiba hutumia nemboya Nyoka. Hata Shirika la Afya Duniani WHO linaumia nembo ya nyoka, waganga wa jadi wanafuga nyoka wa kutosha, hata kwenye nembo ya hospitali ya Muhimbili kuna chata ya nyoka, Noti ya shilingi mia tano pia ilikua na picha ya nyoka ikimaanisha uchumi imara unahitaji watu wenye afya.

Nyoka ni kiumbe pekee mwenye uwezo wa kijivua gamba, tafsiri yake ni kwamba kujivua gamba ni kuleta uhai mpya (Mgonjwa Kupona). Lile gamba la nyoka ukikutana nalo barabarani linatoa nuksi, lishike tu uondoe nuksi za ile rambirambi uliyokula. Hata vidonge vimeundwa kwa mfano wa mayai ya nyoka kuvipa uponyaji. Kumbuka madaktari wanatibu, uponyaji anatoa Mungu.

Mussa alitengeneza nyoka wa shaba akamweka juu ya mti na kila aliyegongwa na nyoka alipona kwa kumwangalia nyoka yule. Uamuzi wa Mungu kuweka uponyaji kwenye nyoka wa shaba hadi mwana wa israeli kupona ndio umefanya taasisi nyingi za tiba duniani kutumia alama iyo ya nyoka.

Mara nyingi ipo getini ili mgonjwa anapoingia getini tu amwangalie nyoka apokee uponyaji. Wazee wa zamani wanakuambia nyoka anajua dawa zoe za mitishamba, nyoka akipata jeraha hujitibu au hutibiwa na wenzake hadi apone walitumia mitishamba, ndo mana wazee wa zamani wakikutana na hali iyo waliwafuatilia nyoka na kuangalia wanachuma dawa kwenye miti gani? na kutumia miti hiyo kama Tiba.

Marekani walianza kutumia alama ya nyoka baada ya kuja Afrika na kujifunza siri hii kutoka kwa wazee wetu, wakati jeshi lao lilioamua kutumia nembo ya nyoka kama alama ya kikosi cha Tiba cha jeshi ambalo awali lilitumia alama ya msalaba. Hii inarahisisha kazi ya madaktari kwa sababu wanatibu mtu mwenye uponyaji teyari. Ndugu zangu hii dunia ni kubwa mno unachotakiwa ni kujifunza kwa bidii sana ili usiishie kutukana tu ati nyoka ni ushirikina.

Nyoka ni kielelezo cha udadisi na umakini, utamaduni wa kuhoji badala ya kukubali kila kitu kirahisi. Kitendo cha nyoka kumwambia Eva ale tunda kina tafsiri mbili. Wapo wanaoona kitendo hicho kama uongo na wengine kama udadisi. Tafsiri ya makala hii ni tujifunze utamaduni wa kuhoji, tusikubali kila kitu kama mazuzu na wakati tuna akili za kutosha.

Robert Gren anasema, mwandishi wa kitabu cha THE 48 LAWS OF POWER anasema,"Hatuna budi kumshukuru nyoka, nyoka alikua mwalimu mkuu wa kwanza duniani, mtetezi wa kwanza wa udadisi na utafiti, adui wa kwanza wa ujinga, mnong'onezaji wa kwanza kwenye sikio la mwanadamu wa kwanza ili ajikomboe." Hii inaitwa Mental Liberation.

Usipotuliza akili ukaenda kiroho sana utasema Gren alimkufuru Mungu na wakati bibilia inasema, "Nyoka alikua mwelevu kuliko wanyama wote wa mwituni aliowafanya Bwana." Soma Mwanzo 3:1.

Kumbuka hata yesu mwenyewe amewahi kukiri kuwa nyoka ni mwelevu sana na akawatuma wanafunzi wake wawe na busara kama nyoka. Hili ni funzo kubwa sana kwamba kila kitu kina ubaya na uzuri na ukijua hilo huwezi kumuua mke wako kwa sababu amekudanganya mana hata wewe ni muongo tena kumzidi mkeo.

Kwanza uongo unasaidia sana maana kuna ndoa bila kudanganya zingesha kusambaratika siku nyingi. Bila kudanganya kuna watu walishafukuzwa kazi siku nyingi. Kuna watu bila kudanganya wasingepata wachumba na wengine wasingeoa bila uongo. Kuna watu uongo umewaokoa na kifo, tatizo la uongo ukigundulika ndo utakoma.

Nyoka ni ishara ya kujipa muda wa kufikiri kabla ya kutenda (Kuwa Makini) kwa asili nyoka ni mtulivu hafanyi jambo bila sababu. Ni hatari kwa viumbe wengine ana sumu kali, hafanyi jambo bila kufanya mchanganuo wa hasara na faida. Nyoka anapenda kukaa sehemu yenye utulivu, anaweza kuingia ndani ya nyumba na kusepa bila mtu yeyote kujua. Wengi tumelala na nyoka sana tu, wakati wa kiangazi wanakunywa maji ndani kabisa, sema kwa sababu ya mahesabu huwezi kuwaona. Nyoka wanacheza sana na watoto wako na hawafanyi kitu chochote kwa sababu wanajua watoto hawana roho mbaya.

Kupitia nyoka tunajifunza kutofanya mambo bila kuangalia madhara na faida kama mjinga anayepima kina cha maji kwa miguu miwili. Tusiwe kama yule mama mkwe aliyetumia hisia kujaji, kisa cha mama mkwe, "Bwana mmoja alikwenda kutembea ukweni kwake ilipofika usiku aliamka kwenda kujisaidia lakini kwa bahati mbaya taa zote zilikua zimezimwa, wakati anapapasa ili kuwasha taa aliparamia vyombo vya chakula jikoni. Kipindi anajaribu kuviweka vizuri mara taa ikawasha na mama mkwe akamuona yule bwana ameshika vyombo na kumwambia. Baba kama hukushiba ungesema.

Mama mkwe alitumia hisia kujaji hakujipa muda wa kufikiri. Shida ya hisia inakupa majibu ya haraka ambayo yanaweza kukuletea shida. Unadhani yule bwana aliendelea kukaa ukweni? Ndo yaleyale unakwenda kutembea sehemu unasikia sisi humu ndani hatujwahi kuibiwa kitu kabisa. Kichwa kisipofanya kazi vizuri ya kufikiri utakuwa mtu wa kuchafua hali ya hewa kila siku. Nyoka anatukumbusha kujipa muda wa kufikiri zaidi.

Kwaiyo unapokutana na nyoka mara kwa mara basi rejea hizi tafsiri hapa lakini unapokutana na nyoka ndotoni hizi hapa tafsiri kutoka kwa mtaalamu wa mambo ya asili.

1. Ukiota umegongwa na nyoka ina maana kwamba unatakiwa kuwa makini kwenye mambo yako vinginevyo utaumia. Umezoea kupiga hela acha, una tabia ya kula ada acha, una tabia ya kula michango ya harusi acha, unahonga hadi hela ya rambirambi acha mara moja, una tabia ya kuchepuka acha usikamatwe na mchepukaji mwezako akakunyonga.

Siku hizi wanaume wanaua sana na hiyo ndo maana ya ndoto ya nyoka. Wazungu wanasema if you have a dream of a snake chasing you, this might mean that you need to look at the relationship in your life and see if you have sweapt any issues underneath malizia kwa kugoogle huo msemo ........

2. Ukiota unamuona nyoka maana yake ni kwamba utadanganywa na mkeo au mumeo. jaribu kumkumbusha uaminifu katika ndoa, najua atawaka kwa sababu umemtachi lakini usikonde kwa sababu kinga ni bora kuliko Tiba ya mapenzi.

3. Ukiota unapigana na nyoka ni ishara ya kuwashinda adui zako, lakini ukiota unakimbizwa na nyoka jua adui zako wanakumaliza. Jipange, kazi kwako kupambana na hali yako. Kazi ya nyoka ni kukupa taarifa tu.

4. Ukiota unafuga nyoka au unamiliki nyoka au nyoka anakumeza hiyo ni ishara ya kupata madaraka makubwa ya uongozi. Kama ulipanga kutia nia we tia tu usiache.

5. Ukiota umemuona nyoka anauliwa barabarani hiyo ni ishara ya kutokea vita au magomvi. unaweza kuzichapa kazini, nyumbani au popote pale hivyo jitahidi kuwa makini.

6. Ukiota shamba lako limejaa nyoka ni ishara ya kwamba utapata mazao mengi msimu huo tunza shamba lako vizuri na unapomuota nyoka amekufa ni ishara umeepushwa na uadui na shari yake. pengine ulikuwa unapiwa hadi kutolewa meno.

7. Ukiota joka kubwa linajizongazonga mwilini mwako ni dalili ya jini aliyeingia mwilini anatafuta sehemu ya kujificha ndani yako. Piga sana maombi.

8. Ukiota una nyoka shingoni mwako ukamkatakata maana yake unakwenda kutoa talaka kwa mkeo.
Mh! ngumu sana
 
Back
Top Bottom