Nyoka na fimbo kwenye Noti ya Tsh 500 ina Maana gani? BoT yatoa ufafanuzi

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Sep 2, 2011
4,875
1,214
TZ35.JPG

Wana Jf,naomba mnijuze Ile picha ya nyoka aliejiviringisha kwenye fimbo pembezon wa Noti ya Tsh 500 ina wakilisha nini?

Habari wana jf! Naombeni kufahamishwa kuhusu picha ya nyoka aliyejizungusha kwenye fimbo, nilishaiona kwenye Taasisi kubwa za Afya kama Muhimbili kisha nimeiona tena kwenye noti ya Tshs. 500 upande wa nyuma kushoto. Ina umuhimu gani mkubwa mpaka kutumika kwenye mahospitali na kwenye noti? Kama kuna mwingine aliyebahatika kuiona kwenye kitu kingine naomba atujuze!

Kila nishikapo noti ya shilingi mia tano huwa nakutana na picha ya nyoka aliyejiviringisha kwenye fimbo. Kwa anayejua naomba anipe ufafanuzi japo kidogo, hivi mchoro ule unawakilisha nini?
IMG_20180825_115033.png

======

UFAFANUZI

========

MAELEZO KUHUSU BAADHI YA ALAMA KATIKA NOTI NA SARAFU
Kumekuwa na mijadala kuhusu alama zilizopo katika noti na sarafu za Tanzania, hususan alama ya nyoka inayoonekana kwenye noti ya shilingi 500.

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:

Utengenezaji wa noti na sarafu za nchi yoyote ile huanza baada ya kukamilika kwa mchakato wa usanifu na michoro ya fedha husika.

Usanifu huo unahusu, michoro na alama mbalimbali ambazo zinaelekeana na nchi husika.

Katika kutekeleza jukumu la kuamua nini kitumike au kisitumike katika kutengeneza fedha, nafasi ya wananchi huzingatiwa. Hapa nchini, Benki Kuu ya Tanzania ina jukumu kubwa katika maamuzi hayo.

Alama za kawaida katika noti na sarafu nyingi hapa duniani ni kama picha za watu mashuhuri, picha zinazoonesha shughuli za kiuchumi, mali asili kama milima na maziwa, majengo marefu na wanyama.
Alama na michoro inayokuwa katika noti na sarafu ina maana halisi ili kuepusha tafsiri potofu ambazo zinaweza kutokea.

Ni wajibu wa Benki Kuu ya Tanzania kuhakikisha kwamba picha, michoro na alama zozote zinazoleta ukakasi zinaepukwa.

Kiwango cha elimu na namna ya utunzaji wa pesa kinachangia namna fedha ilivyo pamoja na alama zake.

Inatakiwa namna fedha ilivyo na alama zake ziwe zinaelekeana na kuwa rahisi kuzitambua.

Hivyo, alama ya nyoka aliyejiviringisha katika fimbo ambayo inaonekana na katika noti ya shilingi 500, inamaanisha utoaji wa huduma za afya. Hii ni alama ya huduma ya tiba inayotumika karibu duniani kote, zikiwemo taasisi za afya za hapa nchini na za kimataifa. Benki Kuu ya Tanzania iliweka alama hiyo katika noti ya shilingi 500 kuonesha umuhimu ambao serikali inaweka katika huduma za afya.

Upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi, wakiwemo watoto, ni suala ambalo linapewa kipaumbele na Serikali. Hili linajidhihirisha wazi katika mgawanyo wa bajeti ya serikali ambapo sekta ya afya inapata rasimali ya kutosha.

Imetolewa na:
Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki
24 Agosti 2018
 

kikahe

JF-Expert Member
May 23, 2009
1,350
279
Hiyo alama iko hata pale MUhimbili, wanadai ni alama ya utabibu
 

Monasha

JF-Expert Member
Apr 2, 2011
559
419
Maana yake fimbo ya mkononi ndiyo iuayo nyoka, na pesa ndio fimbo ya leo, inatatua matatizo mbalimbali


Dah! mwanangu hii inareflect hali halisi ya sasa ndugu yangu......Kweli watu mnafikiria saana. Anayebisha hayupo tanzania kimawazo kaka.
 

mikatabafeki

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
12,777
4,623
nyoka ni imani ya kwamba hutunza kitu................lakini kwa bongo naona inadidimiza
 

Pota

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
2,012
711
<br />
<br />
Ndo maana Maajali hayaishi kale kanyoka kanakunywa damu za watu.

kama ndio hivyo basi ajali hazitokei tena, inabidi abiria wawe wanakaguliwa,
wote wenye noti za miatano wanyang'anywe kwani kanyoka njiani katasababisha
ajali ili kanywe damu... unajua tena safari ni ndefu then hakajala kitu....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom