Nyoka mkubwa kaingia ndani kwangu halafu kajificha

cement

JF-Expert Member
May 5, 2012
581
218
Wadau mwenye kujua namna navyoweza kumtoa maana sielewi kaingia lini na kajificha wapi maana nimemwaga mafuta ya taa nyumba nzima pia nikachoma mpira na nimemuona leo asubuhi hata kazini nimeshindwa kwenda kabisa, watu wote tupo nje mpaka sasa hivi! Mwenye kujua ni namna gani naweza kumpata na kumtoa maana sijui kama yupo mwenyewe au kuna wenzake humo plz jamani mawazo yanahitajika ni Kimara hukuna tukishindwa kumpata tutashindwa kulala ndani wadau leo!

UPDATES
Katika hatua za kumtafuta nyoka hayawi hayawi mwisho wake kapatikana aisee ni mkubwa sana alikuwa kajificha nyuma ya friji upande unaotoka joto, imenishangaza sana lakini pamoja na kumpata bado tunaendelea kupanga mambo hapa ilikuweka mambo vizuri isije ikatokea akapatikana wakati mwingine!

Nawashukuru sana kwa msaada wenu mafuta ya taa yamesaidia sana na kuchoma mapira ndani thanks sana kwa msaada wenu
 
Pole sana mkuu, ninavyojua ile dawa ya mbu aka rungu inaweza mtoa akisikia harufu na huwa inawakatakata kabisa kama ukimpulizia kwa karibu...try that
 
Uwiiiiii
Pole naogopa nyoka....
Kuweni waangalifu na solution ni kumsaka huku mkiwa makini
 
Mafuta ya taa mwaga ndani humox2 alipoingia, halafu jitahidi kuweka vitu katika utaratibu mzuri ikiwemo kutoa makorokoro ambayo sio ya muhimu ili nyumba iwe nyeupe na wazi kiasi utaweza kuona kitu chochote kwa urahisi..
 
Dawa ni hiyo hiyo ya kuchoma mpira pia try hiyo rungu kuipuliza halafu wacha mlango wazi ili aweze kutoka!!
 
Nilichokuwa najua ni mafuta ya taa yanasaidia sana, ukishamwaga tu mafuta ya taa nyoka anakosa nguvu hata kutembea anakuwa hawezi kabisa, anabaki alipokuwa. Wiki mbili zilizopita kwangu kuna nyoka aliingia katika chumba cha dada msaidizi, tulitumia hiyo trick ya kumwaga mafuta hakuweza kukimbia. Alikuwa amekaa katika kona, tulipomwona tu tukammaliza hapohapo. Labda jaribu na hiyo dawa ya mbu huenda ikasaidia. Pole sana.
 
Pia uwe na mti mrefu kidogo baada ya kumwaga mafuta ili uwe unapitishapitisha ktk kona za chumba.
 
Dawa yake kubwa ni Mafuta ya Taa, ila uyamwagapo jitahidi kuwa makini maana akiwa katika harakati za kukwepa mafuta yupo radhi hata kujificha ndani ya suruali yako.
 
Wadau mwenye kujua namna navyoweza kumtoa maana sielewi kaingia lini na kajificha wapi maana nimemwaga mafuta ya taa nyumba nzima pia nikachoma mpira na nimemuona leo asubuhi hata kazini nimeshindwa kwenda kbs watu wote tupo nje mpk ss hv!mwenye kujua ni namna gani naweza kumpata na kumtoa maana cjui kama yupo mwenyewe au kuna wenzake humo plz jamani mawazo yanahitajika ni kimara huku,na tukishindwa kumpata tutashindwa kulala ndani wadau leo!

Tafuta liquid inaitwa formalin lakini iwe haijachakachuliwa, ila ni sumu kali sana. Nashauri upate maelekezo ya namna ya kufungua chupa yenye formalin na kuweka ndani ya nyumba. ila ikiwekwa kwenye chombo na kuingizwa ndani ya chumba lazima nyoka atoke ila itabidi muache milango wazi wa kutokea. Tahadhari ni kuwa usivute hewa yake maana ni sumu na ndiyo inatumika kuhifadhia maiti.
 
Ngoja nimlete MCHINA wangu, huyo nyoka atatoka tu. Labda kama hajipendi.
 
Mafuta ya taa, Oil chafu, Diesel, choma mipira vyote hivyo ni sumu kwa nyoka atatoka tu.
 
Kanunue x-pell puliza nyumba yote kama huna akili nzuri utamuona halafu punguzeni uoga kidogo, nyoka ang'ati mpaka umpige au umkanyage. Kitu kingine hujasema wa rangi gani, rangi nyingine ni kama toi tu la nyoka wawezamshika.
 
Pole mzee sasa ni hivi... Kwanza unatema mate ili yeye asikutemee, halafu unachukua kanga, kitenge au taulo unaviringisha kama kata ili asiweze kukimbia abaki pale pale alipo! Ndipo umtafate! Ukishindwa N-pm nije nimkome Nyani.
 
Mkubwa, dawa uliyokwisha tumia ndio yenyewe lakini wasiwasi wangu ni kwamba yawezekana ukawa umemwaga mafuta na kashindwa kutembea maana nyoka akigusa mafuta huwa anaishiwa nguvu, sasa basi endelea kuchoma maguludumu, then usiwe muoga pita ndani ukiwa na fimbo kubwa unaweza kumkuta mahala katulia au unaweza kukuta alishaondoka muda mrefu. Poleni sana najua amani ndani imepotea na wewe ndio wa kuirejesha. JIKAZE KIUME
 
Huyo nyoka anafananaje.... kama ulimuona..... ili nikwambie tabia zake...
 
Kwa hili tatizo linaninyima raha kabisa maana kama asipotoka tutaingiaje ndani! Hapa ss hv ndo tunachoma mapira ndani na mlango uko wazi ila pia tunajaribu kutoa vitu ndani kupata nafasi kama pengine tunaweza kumuona! Inachanganya sana hata kazini nimeshindwa kwenda!
 
Najaribu kufata ushauri kwa kila anaye nipatia nimeagiza oil chafu sasa hivi niweke kwenye kingo za nyuma yangu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom