Nilitiwa mkwara wa kuimbiwa kikojozi weeeh mbona sikunywa maji siku nzima ili nisijikojo lee..! Yaani niligoma kabisaa..!Hahahahaaa hapana aiseeh mwema ukweli mpenz wa Mungu. Kuimbiwa huu wimbo barabarani hata watu wa nyumbani hawakuwahi niimbia japo nilijikojolea sana. Mama akagundua nikienda kulala kwa mjomba au babu au mamkubwa sijikojolei akajua home nafanya makusudi. Nikipoingia darasa la 2 akanipeleka nikakae kwa mjomba angu alikuwa anakaa oysterbay. Nakumbuka nilikaa miezi 6 January hadi June na sikukojoa kitandani hata siku moja likizo nikarudi nyumbani na tangu hapo sikujikojolea tena.
Nilikuwa nikienda kwa watu naona aibu kuamka godoro limelowa hivo nilikuwa sinywi maji kwa wingi. Nashukuru ndo ilikuwa poa yangu.
Ila home kwetu kitaani watoto walikuwa wanafungashiwa magodoro kila leo hasa jumamosi basi unawachungulia getini wanatia huruma. Mkakutane kwenye michezo jioni akileta za kuleta mnaanza hilooo ndo maana kikojozi hilooo. Basi unamuona mtu ana nyweeaaa hadi huruma. Kwakweli hiyo kindumbwendumbwe ilikuwa inafedhehesha sana watoto.
Halafu umenikumbusha huu sio wimbo bali ilikuwa mnapashana mkiwa mmegombana....
Utasikia twende twende twende miguu kama chelewa twende twende macho kama mayai huyooo nywele kama mkutano wa inzi muone kwanza tumbo kama pakacha la embe twende twende mrefu kama ngongoti twende twende masikio kama popo, mashavu kama chura muone mweupee kama karatasi, hilooo mweusi kama mkaaa hahahahaha hapo hadi unaishiwa maneno hehehehehehe eti hapo ndo ulikuwa unatukana looh
Kunguru wa zanzibar wamewafukuza wote..! Hawa wadudu ni waharibifu sana..! Wildlife society of Tanzania walikuwa wanaweka mitego kwenye magorofa kule posta ili kuwapunguza, European union walipogoma kufund hiyo project nao wakazidi kuongezeka..!Hahahaha hiyo tuliimbaa... Sijui huwa kuna muunganiko gani hapoo...afuu hivyo viyange yange sivioni tena!!!
Vipi zile ndege(plane) zilizokuwa zinaachia moshi mweupe angani zikipita unaimba ndege ya urusi hyooooo
Mie niliambulia vyote. Ila nilikuwa sijali.. Nikipata wasaa wa kucheza na wenzangu nilikuwa nasahau yote..!Yaaani leo basi tuu hadi mzuka wa kunanihii umepanda jinsi nilivyo furahi kukumbuka zamani.
Kiukweli nashukuru Mungu utoto wangu haukuwa mbaya nilipata malezi yote mema na ulinzi wa wazazi na ndugu. Ndomaana hapa nina furaha sana hadi kiwi imepanda hehehehehee.
Kuna watu utoto wao ulikuwa mateso chuki na tabu kedekede na imewatokea hivyo sio kwa kupenda ni mazingira waliyoyakuta. ....
Inshallah panapo majaaliwa kama Islamabad basi tutaonana.
Kumbe walikuwa wanapendeza Sana angani!!Kunguru wa zanzibar wamewafukuza wote..! Hawa wadudu ni waharibifu sana..! Wildlife society of Tanzania walikuwa wanaweka mitego kwenye magorofa kule posta ili kuwapunguza, European union walipogoma kufund hiyo project nao wakazidi kuongezeka..!
Huo mchezo bora niwe wa mwisho kuweka maana una maumivu makaliKinyuli nyulika mwanangwa wa Jumbe, kavaa nguo mbili, ya tatu kajifunika.Aliye juu aondoke.
Hapo mmefinyana nyumba ya viganja
yeah naukumbuka sana huo mchezo Iringa tulikuwa tunaita Uki, unachora mstatili wenye njia na viduara vinne kila kona kwa ajili ya kusimama unatakiwa ukimbie mpira unaporushwa usimame kwenye duara kabla mzingaji wa pili hajadaka mpira nafkiri.Its complicated sijui nianzie wapi. Mnaozinga mko wawili, mnaowawinda wanakuwa wanazunguka kwenye umbo mstatili.
KimbukaMimi mpaka leo najiuliza uhusiano wa nyimbo moja na tukio lililotokea huko US:
Mvua ikinyesha tulikuwa tunacheza kwenye mvua na kuimba, "Mvua njoo, katarina usije.....mvua njoo, katarina usije". Tuko wadogo, nadhani tulipokea/rithi hiyo nyimbo toka kwa wakubwa zetu; na ni miaka mingi nyuma, miaka mitatu minne nyuma tukashuhudia "Hurricane Katrina" na maafa aliyosababisha US; mvua inanyesha, moto unawaka!
Katarina/Katrina ni nini?
kuna katoto nilikua nacheza Nako kwa kukarusha juu Na kukadaka. Nakarusha tena Na kukadaka. Nilipo acha kakaniambia "acha us*nge nirushe tena" nikabaki hoi
Huu sio ule wa mgeni siku ya kwanza mpe mchele na panzi mtiliie kifuuni mkaribishe mgeni?Huu wimbo sisi tulikuwa tunaimba hivi
Moja ........(nimesahau)
Mbili, taa ya kandili
Tatu, mwali kaliwa na chatu
Nne, tumpate tumchune
Tano ,kapika wali manjano
Sita, waarabu waenda vita
Saba, ndiyo siku ya mahaba
Nane, ingia ndani tuagane
Tisa,tisatisa ya tisini
Kumi,kwa mateke na magumi.
Ukifika hiyo kumi unampiga aliye karibu yako ngumi au teke.
Mie ntaimba!Hahahahaaa Hahahaaa hivi tunao changia huu uzi tukisema tukutane leaders club halafu tuanze kuimba hizo nyimbo heheheeee er ntacheka nahisi hadi nijikojolee heheheheheee
Itakuwa bonge la burudani, ila saa hizi hutoruhusiwa kuchungulia chupi tukiwa tunaruka kamba.