kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,298
- 12,600
Tusiomboleze kama watu tusio na imani na MwenyeziMungu. Eti utasikia nyimbo MTU anaimba sasa tutakimbilia wapi, tutaishije bila yeye, tangulia tu na sisi sote tutakufa na tutaonana baadaye, kwanini Mungu umemchukua, tutafanyaje sasa, hatatokea mwingine kama wewe, nk.
Nyimbo hizi hazitufanyi tuwe imara badala yake zinatudhoofisha na kumkufuru Mungu. Zinatudumaza badala ya kutuimarisha tayari kwa kusonga mbele.
Tuimbe nyimbo za kumtakia heri huko aendako marehemu lakini sio za kutuogopesha, kutukatisha tamaa kuwa basi tumekwisha tena na kukufuru.
Wasanii wetu tunawapenda lakini taifa na familia zimeondokewa na watu wao muhimu kwa maelfu na maelfu kwa karne na karne lakini bado maisha yanaendelea hadi leo. Tuimbe nyimbo za kuwasifu na kuwaombea roho zao ziwekwe pahala pema peponi ingawa haitawasaidia sana kama kwenye uhai wao hawakuwatendea watu na mungu mazuri.