Nyimbo za Jaguar huenda kufungiwa kupigwa nchini

kinondoniilala

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
988
762
Wanabodi...!

Msimamo wa umoja wa wamiliki wa vyombo vya habari nchini Tanzania, kwa kauli moja wapo mbioni kutoa tamko juu ya kutopiga nyimbo za Jaguar katika vyombo vyao vya radio na television ikiwa pamoja na kutokuchapisha habari zake ikiwa hatoomba radhi ndani ya siku ya 3 kuanzia kesho tarehe 26 Juni 2019.

Nawasilisha
 
Kafanyaje kwanza
KENYA: Mbunge wa Jimbo la Starehe, Charles Njagua ‘Jaguar’, amesema hataki kuwaona wafanyabiashara kutoka China, Tanzania na Uganda kwenye jimbo lake akidai kuwa wamekuwa kikwazo kwa wafanyabiashara wazawa wa nchi hiyo kukuza biashara zao kutokana na mashindano ya kibiashara baina yao.
Katika kipande cha video kinachosambaa mitandaoni, Jaguar ambaye pia ni mwanamuziki, amesema wanawapa saa 24 wafanyabiashara hao ambao ni raia wa nje (sio Wakenya) kuondoka nchini humo la sivyo watawapiga mawe na kwamba hawaogopi mtu wala kitu chochote.
“Watanzania, Waganda na Wachina wanaofanya biashara Kenya, hatuwataki, hatutaki wafanyabiashara wetu wa-compete na wafanyabiashara wa nje, tunawapa masaa 24 waondoke. Tunaomba waziri na idara ya uhamiaji alishughulikie hili, wasipoondoka tutawapiga na hatuogopi mtu,” amesema Jaguar.
 
DuuuH!! Ni Hatarii Saana Ila Simshangai Jamaa si nasikia kashawahi Kuzidunda Bungenii
 
Msanii aneyejiita Jaguar ambae anatokea Kenya amesikika akisema atafukuza watanzania ,wachina etc kutoka nchi yao..nilivyosikia tu mkuu
We unaona ni Jambo Dogo lakufumbia macho?? Nasisi tukisema tufukuze wakenya nchini Tanzania itakuwajee? Ameboronga Sana jamaa
 
Mbona hajui kuimba?haina haja ya kumfungia huwa yupo flat na melody moja nyimbo zote.
 
Back
Top Bottom