Nyimbo ya samaki ya wazanzibar mmh! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyimbo ya samaki ya wazanzibar mmh!

Discussion in 'Entertainment' started by Mtu wa Pwani, Sep 19, 2009.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2009
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Jamani kuna nyimbo mpya ya wale offside trick ya kule zenji ambayo nimeiona kwenye tv jana imeniacha hoi

  Iile nyimbo mbona imekaaa kimatusi sana

  Anasema wanamvyomla jicho na wanamvyombirua birua

  Kuna sehemu samaki huchanganywa changanywa kwa mchuzi nyanya na biringani

  Kkwa kweli ile nyimbo haijakaa vyema kimaadili au wadau mnasemaje?
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  mara nyingi wasanii watoa kitu kulingana na mahitaji ya soko, kama wewe unaona huo wimbo haufai bac ujue ni jamii nzima haifai, kwa sababu jamii imelishwa inachokitaka, maana cha ajabu huo wimbo umeuona kwenye TV tena pengine ya Taifa na watu wanaupenda tu
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  yale yale nilioyazungumza kwenye ile thread ya abusive colture
  mtua annaamua kuwa abuse watu bila kujali sababu zilizowafanya hao watu wawe hivyo.
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Nyimbo hizo ni ovyo hazifai zinaendeleza culture ya kuwalaumu victim na sio kuangalia tatizo,hao samaki wengi wao ni victim tu.
   
 5. King Zenji

  King Zenji Senior Member

  #5
  Sep 19, 2009
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33

  ....Mmmh thatha kwani THAMAKI hawa wanaowasema wao si ndo TUNAOKULA kila siku jamani au???,acheni kuhamisha GOAL POST hizo,jamaa wana maana halisi ya SAMAKI na sio SAMAKII waleeee!!!
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  we ndo wale wale i guess,
   
 7. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Wakuu naomba mtuwekee hiyo nyimbo tuisikie,

  Akhsanteni
   
 8. King Zenji

  King Zenji Senior Member

  #8
  Sep 19, 2009
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  ,, Ha ha haaaaaa!!,sa kumbe wana maana gani MKUU??
   
 9. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2009
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Najaribu kuvuta picha naona ile samaki ina maana mbaya sana na hasa wanapokazia kuliwa jicho maana kisha kichwa wanampa paka hapo tafsida yake ni pana walonayo waiweke ili watu waisikie na waweze kuichangia
   
 10. a

  ambu Member

  #10
  Oct 2, 2009
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  hahahaaaaaa waswahili kila neno latafsiriwa mpendavyo samaki ni samaki na ndo wale ina maana gani?
   
 11. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #11
  Oct 2, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  wimbo safi sana huu..yaani samaki analiwa jicho ye katulia tu....teh tukimla sie watu hawasemi ila yeye akitula sisi habari magazetini ,kwenye ma TV and maofisini....
   
 12. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Wewe ndio umekaa kimatusi matusi au labda ulikuwa unataka jamaa waimbe nyimbo ya matusi,hawa jamaa wameonyesha huruma juu ya hawa viumbe ambao walistahili kuja nchi kavu kuvuta hewa then warejee kwao,lakini mimi nawalaumu sana hawa wanaopenda kuwa vua vua hawasamaki,ndio wanaowasababishia matatizo yote hayo,pole sana samaki kwa kuvuliwa vuliwa!!!
   
 13. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona kuliwa jicho tuu ndio kumekushtua,we unamaanisha nini kuhusu hilo jicho?
   
 14. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2009
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  [ame="http://www.youtube.com/watch?v=gYuV1HEyKK8"]POLEEEEE SAMAKI POLEEEE......WANAVYOKUFANYA[/ame]
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  mbado kuusikia huu
   
 16. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #16
  Oct 21, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  SIku hizi kila neno utakaloongea linatafsiriwa kimatusi na akili zetu sasa zimekuwa tuned huko hebu fikiria neno KUMEGA, tafsiri yake ipo wazi kabisa kwenye kamusi na miaka yote limetumika vizuri tuu lkn leo umwambie binti HATA KAMA KASHIKA KWELI TUNDA MKONONI UMWAMBIE TUNDA LAKO LIMEMEGWA HILO WALLAHI MAHAKAMANI MTAFIKA, maana halisi ya neno imeshahamishiwa kubaya, Vile vile samaki kweli ana jicho/macho na unapomla samaki yale macho yake huwa km yanakuangalia kwa HUZUNI, vile vile kweli ukimaliza upande mmoja basi utamGEUZA upande wa pili, mimi sioni uhalisia wa MATUSI kwenye huo wimbo sababu ukichukua kamusi ukaangalia neno JICHO tafsiri yake ni tofauti na hii ya kwako ya leo, kwa maana hiyo mtu anayejua kiswahili vizuri wala hawezi kwazika lkn km ni hiki cha MTAANI au WAKATI HUU basi maana halisi ya KISWAHILI imepindishwa. Fikiria wimbo huu ungeimbwa miaka ya mwisho ya 1997-1999 hakuna mtu angeona kuna matusi hapo.
   
 17. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #17
  Oct 21, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndo kazi ya sanaa jamani
   
 18. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #18
  Oct 21, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  nyimbo hiyo labda ipigwe marufuku kwa video yake, ambayo naona haifai kuweka wakati wa day time televishen....
  lakini kwa lugha ilotumika ni bora kuliko nyimbi nyingi zinazosema nikenda geto nikampa msichana pesa nikammega.
  bora hii imetumia lugha ya kisanii, na ukitaka kujua tusi ujitafsirie mwenyewe tu
   
 19. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2009
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Sisi kule kwetu ziwa victoria tunakula macho na kichwa pia. Atleast I do.
  Kuna imani ukila kichwa na macho ya samaki yaani akili inakuwa sharp sharp tu. Ulishawahi ona mtoto wa kikerewe mdogo miaka chini ya mitano lakini anakula fulu (visamaki vile vidogo vidogoo) na kuchambua vimifupa kiustadi kabisa? lol tumwulize Mkandara.
  Hawa samaki wa pwani wanapewa pole, je sangara anayepigwa panki na mifupa kusagwa itakuwaje? Mimi naona itabidi waje na part II ya huu wimbo.

  Halafu we Chimunguru acha hizo, utamwambiaje mtoto tunda lako limemegwa hilo walahi? Lol, huo ugomvi.
   
 20. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #20
  Oct 21, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  ndio shida ya fasihi.....huwa inaachwa kila mtu atumie common sense yake kuelewa maana7ujumbe uliomo.Hata mpoto katika wimbo wake wa mjomba mpaka sasa kila mtu anatafsiri ajuavyo......inawezekana kweli haijakaa sawa kwako lakini ikawa na maana kwa waqliotunga na pengine walilenga kuonyesha huruma yao kwa samaki wanavyofanywa..................
   
Loading...