Nyimbo kama wowowo zinashusha hadhi ya muziki wa bongofleva

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,636
7,005
Nakumbuka mwanzo wa muziki wa bongofleva watu wazima walichukizwa na mtindo huo na kuziona nyimbo hizo kama za kihuni.

Ni baada tu ya jitihada kubwa za baadhi ya wasanii maarufu kama akina Sugu, Prof J, lady JD na wengine waliofanya muziki huu uanze kubalika hata kwa watu wazima kutokana na kuimba mambo yasiyo na ukakasi hasa wimbo huo unapopigwa eneo la umma ama nyumbani wakiwepo watoto na watu wazima.

Sasa jitihada hizo naona zinabomolewa kwa kasi na hawa Clouds ambao siwaelewi kabisa. Leo natamani Clouds kwa sababu ya kuendeleza upumbavu huu hata iungue moto na kutoweka kabisa.Nyimbo zinadhalilisha utu wa mtu kwao ndio zinapewa kipaumbele.

Nyimbo kama mwanaume machine, zinamdhalilisha hadi mmiliki wa Clouds mwenyewe Kusaga ambaye iliwahi kusemwa na mwanadada mmoja maarufu mitandaoni kuwa "umbile lake linaweza kujadilika likamdhalilisha.

Nadhani umefika wakati wa kuwang'oa hawa wafanyakazi wa Clouds wasio na akili hata kuhisi tu baadhi ya nyimbo zinawadhalilisha hadi wazazi wao.

Kusaga amka na kama una ndugu zako wapo hapo Clouds hawajielewi kwani wanaendeleza udhalilishaji dhidi yako mwenyewe na watu wengi kwa ujumla.
 
Mambo ya ngono ngono ndiyo inatawala sahivi

Ova
Siku hizi watu wanaangalia Pesa kuliko maadili.
Lile tangazo la Tigo la mtoto anamuuliza baba, umempataje mama? Au lile tangazo la godoro Unafikiri lina maadili?
Sasa hivi ngono ndiyo imetawala. Iwe muziki, matangazo, filamu ni ngono n.k
Kuharibika kwa maadili ya Tanzania yameanza pale tulipoanza kupokea utamaduni mbovu wa kutoka nje ya nchi.
Unafikiri ukizuia Muziki wa ndani, na muziki wa nje ukaendelea kuwepo unafikiri itasaidia? Km mtaani kwako kuna madanguro, vibaka wanakaba mpaka mchana na watu wanawaangalia unafikiri nani wa kulaumiwa?
Mtoa uzi watu wametanguliza pesa mbele kwahiyo suala la maadili limewekwa kwando. Kilichobaki sasa kila mtu hakikishe anamlea mtoto wake ktk maadili mazuri. Hawa ndiyo watakaoubadilisha ulimwengu kutoka ktk kizazi kisicho na maadili kuwa ktk kizazi chenye maadili.
 
Kastory by Jeby
Swahiba by Jeby
Mwanangu huna nidhamu by Dudu baya
Mwambie ukweli by Jide
Dingi by Man dojo & Domokaya
Usinichukie by Afande Sele
Nitafanya by Daz Nundaz
Pesa by Madee
Nipe ripoti by Tundaman
Mkuki moyoni by Afande
Maji ya shingo by Daz Nundaz
Umeondoka by Dudu baya
Umeondoka by Afande Sele
Malaria by Afande Sele
Machozi ya furaha by Jide
Barua album by Daz Nundaz

Ni baadhi ya nyimbo za kizazi kipya ambazo huwa zikipigwa ni nadra sana ubongo wangu kunasa vitu vingine kwa wakati huo........zipo nyingi
 
Hizi zote zilikuwa nzuri kipind kile. Leo hii zimekuwa zilipendwa. Watu wanataka nyimbo za burudani zaidi kuliko kuelemisha na kuonya.
Mwanaume mashine au haina ushemeji ndizo zinatamba kwa sasa.
Macho kweny pesa
 
Kuburudisha si lazima uimbe mambo ya kudhalilisha utu wa mtu!Iwapo mzazi wako ndiyo anacho hicho kitu kinachoimbwa"wowowo" unadhani itajisikiaje wimbo huo ukipigwa?
Ama wewe mwenyewe ukawa na maumbile madogo halafu mkeo akawa anaupenda sana wimbo huo utalipokeaje?Yaani wewe si mwanaume humo ndani?Au tuseme kwa sababu ya kuongezeka kwa mashoga ndio maana hata watoto wa kiume wengi wanashobokea nyimbo hizo?Hamjaona watoto wa kike wana madildo kwa kuwa hawaridhiki na maumbile ya wanaume?Kwa hiyo mmeona mtunge na nyimbo za kutukuza uchafu huo?
 
Ushawai kumuuliza baba yako, alimpataje mama yako?
Tuanzie hapo kwanza
 
Unachuki na clouds fm.

"Watanzania wanapenda maendeleo lakini wanawachukia watu wenye maendeleo" By Justine Nyari
Sina chuki bali ninachukizwa na uchafu unaopewa nafasi kubwa zaidi na pengine cha ajabu ni pale ambapo huenda nao wanaamini hata boss wao si "mwanaume" kwani habari za machine yake zilishasemwa na mwanadada maarufu mtandaoni,kwa hiyo wanavyotukuza vitu kama hivyo ni kama wanamnanga pia boss wao.
Huwezi ukaimba wowowo wakati mnajua kabisa hayo ni maumbile ya asili ya wanawake wa kiafrika na hawawezi kuyaepuka hata wakishakuwa wazazi.Tuacheni mambo haya ya aibu kuyashobokea kwenye vyombo vikubwa kama clouds ambavyo vikitumika vibaya huweza kueneza ushenzi nchi nzima
 
Hizi zote zilikuwa nzuri kipind kile. Leo hii zimekuwa zilipendwa. Watu wanataka nyimbo za burudani zaidi kuliko kuelemisha na kuonya.
Mwanaume mashine au haina ushemeji ndizo zinatamba kwa sasa.
Macho kweny pesa
Muziki unaoishi ni muziki wenye pesa zaidi kuliko muziki unaoangalia pesa.

Kama tutaangalia, MJ alikuwa ndio mwenye pesa zaidi kwenye tasnia hiyo, nyimbo zako zikoje?

Ebu cheki nyimbo ya King Kikii, kitambaa cheupe....
Rangi ya chungwa....
Kajituliza kwake kasuku...

All in all, hao wanaofanya hiyo muziki ya shangwe na pesa hawana hizo pesa....ni kama bongo movie's. Chibu wakati anasema akaunti yake inasoma 1bn, alitumia miaka zaidi ya miwli kujenga nyumba ya thamani ya 260mil
 
Mpaka watu kuanza kuandika nyimbo zisizokuwa na maadili chanzo ni ss watanzania.
Unafikiri lile tangazo la tigo, lipo sahihi? Je, kwa maadili ya kitanzania ni halali?
Shuleni, kweny matamasha, wanafunzi wanaimba nyimbo za mapenzi na walimu wapo busy kumsikiliza. Nyumbani mzee anaangalia bongo fleva na watoto.
Nyimbo ya wowoo ya Zaiid ni matokeo yetu ya malezi ya jamii nzima. Leo mtoto wa jirani anakutukana, ukimpiga mzazi anakuja juu.
Tusilaumu vijana kwa hizi nyimbo, ila tuangalia tulipokosea ni wapi ili tutokomeze huu ujinga. Huwezi kuzuia nyimbo ya wowoo isichewe wakati nyimbo za nusu uchi kutoka nje zinapigwa.
Haina ushemeji tunakulaga by man Fongo ilikuwa hot na man Fongo ndiyo alitokea hapo. Je, hii nyimbo ya man Fongo ipo sahihi?
 
Muziki unaoishi ni muziki wenye pesa zaidi kuliko muziki unaoangalia pesa.

Kama tutaangalia, MJ alikuwa ndio mwenye pesa zaidi kwenye tasnia hiyo, nyimbo zako zikoje?

Ebu cheki nyimbo ya King Kikii, kitambaa cheupe....
Rangi ya chungwa....
Kajituliza kwake kasuku...

All in all, hao wanaofanya hiyo muziki ya shangwe na pesa hawana hizo pesa....ni kama bongo movie's. Chibu wakati anasema akaunti yake inasoma 1bn, alitumia miaka zaidi ya miwli kujenga nyumba ya thamani ya 260mil
Unamaanisha king kiki ana pesa kuliko diamond? Kitu ambacho haukijui katika industry, nyimbo ambayo inatrend haraka ndio inaingiza pesa kuliko nyimbo ambazo zinaishi, buble gum music ina pesa sana kamuuloze fidq kwa nini "sura mbili" haikutamba mbele ya "fresh". Ndio kizazi kinavyotaka na sanaa ni industy ya kama bakhresa anavyokuuzia energy drink. Hata huko ughaibuni ukisikiliza ngoma za kina krs-one, mass, big, pac zilikuwa zina mlengo mzuri lakini kizazi cha sasa kimewakubali sana waKina drake, wyne na minaj. Hitaji lako watu wanalifanyia biashara. Kama mtaani kwako wanapenda sana ufuska option itakuwa ni kujenga guest tu, ndivyo ilivyo.
 
Wrong perception........mob psychology, that's all I can say!
 
Ushawai kumuuliza baba yako, alimpataje mama yako?
Tuanzie hapo kwanza
Huenda tuligeuzie swali hili kwako dada,unaweza kumuuliza mama yako kwa nini alimkubali baba yako?Sikuelewa mantiki ya wewe kutaka kuanza kwa kuniuliza swali hilo.Ila dada yangu nakushauri tu kama Mungu kakujalia hicho kinachoimbwa wowowo,kuna watu wazima mama zetu,shangazi zetu na hata Dada zetu wengi wasiopenda kujadiliwa maumbo yao kwenye nyimbo.Mtu anaenda sokoni vijana wahuni wanamwimbia wowowo huku akiwa na mwanae ni aibu na inaweza kuchafua amani
 
Nimekuuliza swali hilo kimakusudi kbsa ili kupima uelewa wako kuhusu suala la maadili na nimegundua unahitaji elimu kuhusu haya mambo.
Suala la maadili linaanzia nyumbani kwenye nyumba ya baba yako na mama yako kisha linasambaa kwa watu baki (watu ambao hawako ktk familia yenu.)
Makosa yameanzia nyumbani na sasa yamesambaa kwa watu baki.
Baba na mama wanaangalia bongofleva wakiwa na watoto wao, video zinachezwa watu wakiwa nusu uchi nao wanafurahia tu. baba anatukana matusi mama na watoto lkn yy mzazi anachukulia kawaida. Mama nayy kwa watoto hivyo hivyo.
Huko nje, watoto wa baba huyu wakifanya makosa, na jirani akamuadhibu mtoto baba na mama wanakuja juu.
Mtoto anafanywa mali ya wazazi na siyo jamii, ndipo hapo matokeo unayaanza kuyaona. Inapigwa nyimbo haina ushemeji tunakulaga by man fongo unachekelea tena unaongeza na sauti kbsa ili uisikie vizuri, ukisikia nyimbo ya mikasi bya Ngwair unaruka juu kwa furaha, sasa hivi kuna lile tangazo la Tigo la mtoto, pia kuna tangazo moja la godoro jamaa anamwambia mshikaji watoto wangu wamepatikana kweny hili godoro lkn haya yote hakuna mtu anayekemea wote wapo kimya, nafikiri hata ww unafurahia sana ukiona lile tangazo la tigo lkn leo umesikia nyimbo ya wowoo umehamaki. You are too late my brother. Hiyo ya wowoo ni matokeo ya hainaga ushemeji tunakulaga n.k
Kwahiyo usishangae kuuona watu wanatoa tangazo wakiwa nusu uchi.ili kuyadhibiti hii maadili yaanzie nyumbani na mtoto au watoto wawe wa jamii nzima.
Km nyimbo ya man fongo hainaga ushemeji tunakulaga ili tamba, kwahiyo jitafakari. Sasa hivi tupo kweny -1, tukifika 0 usishangae
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom