Nyimbo: CHADEMA na Polisi walishirikiana mauaji ya Daudi Mwangosi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyimbo: CHADEMA na Polisi walishirikiana mauaji ya Daudi Mwangosi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Oct 28, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  TUKIO la kuuawa kwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel ten mkoani Iringa, Daud Mwangosi, limeendelea kuibua mambo mapya, baada ya aliyekuwa mgombea wa ubunge wa jimbo la Njombe Magharibi kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kudai chama chake kilishiriki mauaji hayo kwa asilimia 50 na asilimia nyingine 50 ilifanikishwa na Serikali kupitia Jeshi la Polisi.

  Nyimbo alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wandishi wa Habari Jijini Mbeya katika mkutano wake aliouandaa kwa nia ya kutangaza nia yake ya kujiuzulu uanachama wa Chadema na kubakia mwanasiasa huru asiye na chama.
  Alisema kuwa Chadema hawakuwa na sababu ya kwenda kuzindua tawi la chama hicho katika kijiji cha Nyololo wilayani Mufindi kwa sababu tawi hilo alikuwa tayari alishalizindua yeye mwenyewe miezi mitatu kabla ya kutokea kwa mauaji ya marehemu Mwangosi."Asilimia hamsini, mauaji ya rafiki yangu Marehemu Mwangosi yalisababishwa na Chadema kwa kutotii amri ya Jeshi la Polisi na kupanga kwenda kuzindua tawi la chama ambalo mimi nikuwa tayari nimekwishalizindua miezi mitatu iliyopita kabla ya tukio lile," alisema Nyimbo.

  Nyimbo alisema kuwa tabia ya viongozi wa kitaifa wa Chadema kutoka makao makuu ya Chama Jijini Dar es Salaam na kwenda mikoani kufanya mikutano ambayo huwa haijafanyiwa maandalizi yoyote na wenyeji wao, hali ambayo inawafanya walazimike kufanya maandalizi wao wenyewe, ndiyo inayosababisha migongano isiyokuwa ya lazima na Jeshi la Polisi na hatimaye kuwa chanzo cha vurugu kwenye mikutano ya chama hicho.
  Alisema kuwa kwa kawaida mikutano ya siasa inapaswa kuandaliwa na wenyeji kwa kuwa ndio ambao wanaofahamiana vizuri na uongozi wa Jeshi la Polisi katika eneo husika kwa kuwa wao wakikaa na kuzungumza huelewana, lakini suala hilo linapoingiliwa na wageni husababisha viongozi wa sehemu husika kuwa na wasiwasi wa usalama na hivyo kutokea migongano inayosababisha kutokea kwa vurugu.

  Akizungumzia ushiriki wa Jeshi la Polisi katika mauaji ya Mwangosi, Nyimbo alisema kuwa haikuwa sahihi kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa (RPC), Michael Kamuhanda kuingilia kati suala hilo kwa kuwa sheria ya mikusanyiko inaeleza wazi kuwa mwenye jukumu hilo ni Mkuu wa Polisi wa eneo linalofanyika tukio ambaye alipaswa kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD).
  Alisema kuwa ikitokea OCD akazidiwa nguvu au kushindwa kutoa maamuzi kwa suala husika ndipo hulazimika kuomba msaada kwa bosi wake ambaye ni RPC ambaye naye anastahili kutoa maelekezo na sio kwenda moja kwa moja kwenye eneo la tukio kama alivyofanya Kamuhanda.Kwa mujibu wa Nyimbo, hata tume iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi kuchunguza chanzo cha mauaji hayo ilikuwa ni batiri kwa sababu Dk. Nchimbi ni sehemu ya watuhumiwa kwa upande wa Serikali.Alisema kilichotakiwa kufanyika baada ya kutokea kwa tukio hilo ilikuwa ni uwakamata viongozi wote wa Chadema na viongozi wa Polisi waliokuwa eneo la tukio na kuwaweka ndani kwa muda kupisha uchunguzi wa tukio hilo na pia kuwapa fundisho wasijaribu kuchezea roho za watanzania na amani ya taifa.

  Mwangosi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wandishi wa Habari mkoani Iringa (IPC) aliuawa kwa kulipuliwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu wakati akiwa kazini katika kijiji cha Nyororo wilayani Mufindi ambako Chadema walikuwa wakizindua tawi la chama hicho kijiji hapo.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  Kahama CHADEMA kwa MAPENZI yake? Kwasababu Hakuvutwa CHADEMA... aliamua sababu kura hazikutosha yeye kUGOMBEA U-BUNGE kama Mwana-CCM.

  Na kiuhalali hawezi kupata U-BUNGE ndani ya CCM, Aliyechukua JIMBO ni KIJANA na MACHACHARI; Au ni hizo RETIREMENT PACKAGE's wanazopewa Wana CCM - AMEZIKUMBUKA???

  Sababu ukikaa kimya CCM Wanaweza kukuzika UKIWA BADO UNAWAKA na MAPESA MFUKONI...

  Sasa analeta Story ya Mauaji kwanini alisubiri muda wote huo??? au alikuwa anataka kupata MNUNUZi ambaye ni CCM?
   
 3. C

  Concrete JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Huyu dingi anatafuta mtaji wa kisiasa tu ili agombee ubunge 2015 kama mgombea binafsi.

  Tawi ni la CHADEMA sasa shida ni nini kwa wao kulizindua hata mara 100.
   
 4. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Je suis fatigué
   
 5. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hoja haina mashiko iyo kumbe cdm walishiriki kwa kuzindua tawi Mara ya pili Mimi nilidhani walimvisha mangos bomu...
   
 6. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,183
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  hizo ndio dalili za ugonwa wa ukiki,(ugonjwa wa kufilisika kisiasa) ulimpata akiwa ccm na ameshindwa kupata tiba yake cdm,maana hawaujui na hauko ccm
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Anaposema 'wenyeji' ndio walitakiwa waandae mkutano ana maana gani? Mwangosi alikuwa mgeni? Police walikuwa hamjui marehemu Mwangosi? Amesoma report ya tume ya haki za binadamu? Na huo utii kwa police anaosema ni kwa chama kimoja au?

  Politics aside, kwanini police wa Tanzania wanatumia silaha za moto kukabiliana raia ambao hawana silaha na wala hawaonekana kuwa tishio kwa police? Mwangosi (regretably) si victim wa kwanza wa mtindo wa policing hapa Tanzania. Ni lini police wetu watabadilika na kuwa kweli walinda raia na sio wauawaji wa raia? Na kama kuna 'watetezi' kama huyu mzee tuna matumaini gani?
   
 8. Ufipa-Kinondoni

  Ufipa-Kinondoni JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2012
  Joined: Jan 3, 2012
  Messages: 4,488
  Likes Received: 2,147
  Trophy Points: 280
  Nampongeza ameondoka wakati mzuri. CDM si sehemu ya kupanga dili zenu Nenda ccm.
   
 9. h

  hacena JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  huyu mzee kweli ni mpuuzi sasa kurudia kuzindua tawi kunatosha kuhalalisha mauaji? sasa mtu asipotii amri halali adhabu yake ni kifo, asante Mungu hakushinda ubunge angeungana na Shibuda ingekuwa kazi kweli kweli
   
 10. P

  PROF PHILOSOPHY Senior Member

  #10
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bado ana hangover za magamba. akili yake imechoka imechakaa. ni aibu mtu mzima kama huyu kutoa hoja nyepesi kama hizo. kweli hafai kuwa mbunge huyu. yaani kuzindua tawi tayari hilo tu cdm washiriki asilimia hamsini? ebo! mimi nilidhani ankuja na hoja nzito. akafie mbali huyu makapi ya magamba. alikuwa wapi siku zote. nonsense! kubwa jinga.
   
 11. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Njaa mbaya sana,hii mijitu yenye njaa zao muiangalie sana viongozi wa CHADEMA
   
 12. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Another Shibuda...,!mbona hakuyasema haya wakati ule wa msiba?
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  Kuna UZINDUAJI wa TAWI bila kupata WANACHAMA; Na PIA UZINDUZI wa Kupata WANACHAMA

  Sasa Kama NYIMBO alifungua TAWI tupu na Matumizi yapo lakini PESA hakuna; Kwanini Wasiende wanaojua kuvutia Wanachama chama HAKIHITAJI OFISI ni WANACHAMA HAI...
   
 14. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  Kufungua TAWI sio JENGO na BENDERA; Tawi ni WANACHAMA...
  Sasa kama huyu NYIMBO alienda kupiga picha na BENDERA OFISI tupu... nani ataiendesha hiyo OFISI

  BILA kuwa na WANACHAMA wa KUJITUMA na KUKICHANGIA CHAMA? NDIO MAANA ni LAZIMA waende hata MARA 20 kukizindua HILO TAWI na Wananchi na Wanachama wakielewe'

  Sasa kama NYIMBO ndio alifungua basi - hakuna tena sababu ya kwenda HUKO????

  HIYO NDIO SIASA GANI hiyo????
   
 15. N

  Nawaluzwi Member

  #15
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 14, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo mzee aache tabia za kuwa ,anapotezea waandishi wa habari muda wao,kwa kuongea utumbo,hatutaki kudanganywa kama watoto kwa vitu vilivyo wasi,kama avuta bangi basi aiache make inapeleka pabaya.
   
 16. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  jamani wazee kama hawa wapumzike..siasa za 2012 hawaziwezi...wastaafu wakae nyumbani walee wajukuu zao...
   
 17. anjnr

  anjnr JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 483
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Arudi kwa mafisadi wenzie, anatuzuga tu.ukweli mambo yake mengi yameyumba, moja nalolifahamu vema ni kwamba hivi karibuni kijijini kwake Wangutwa watu wa idara ya maji waligundua ame-bypass meter ya maji hivyo amekuwa akitumia maji kwa ajili ya kunyweshea mifugo yake bure.Alitozwa faini na kukatiwa maji, sijajua kama ameunganishiwa tena au la. Kwa kiongozi kama yeye anapaswa kuwa mfano na si kujifanya kukemea mafisadi huku na yeye yumo.huenda aliyafanya hayo akiwa ndani ya chama tawala enzi hizo.
   
 18. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Good riddance..
   
 19. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Fall out ya mauaji ya Daudi Mwangosi utazitesa pande zzote zilizo husika kadri mambo yanavyozidi kujitokeza hadharani.

  Imeanza kubainika kuwa huu mpango wa M4C sasa ni roller litakalo waathiri waliombele katikati na hata karibu na matukio yake , bila kujali maisha ya mtanzania.

  Kulingana na gazeti la Mtanzania leo 29/10/2012,page 14, Mzee Nyimbo aunguruma:

  "Nasema bila ya kubabaika na nina uhakika na ninachokisema ni kwamba kwa asilimia 50, mauaji ya mwanangu ambaye pia alikuwa ni rafiki yangu Mwangosi, yalisababishwa na CHADEMA kwa kutotii amri ya Jeshi la Polisi na kupanga kwenda kuzindua tawi la chama ambalo mimi (Nyimbo) nilikuwa tayari nimekwisha lizindua miezi mitatu iliyopita kabla ya tukio lile,"


  "Nyimbo alisema tabia ya viongozi wa kitaifa wa Chadema kutoka makao makuu jijini Dar es salaam kwenda mikoani na kufanya mikutano isiyokuwa na maandalizi ya wenyeji wao, inachangia katika kuzuka kwa migongano isiyokuwa ya lazima kati yao na Jeshi la Polisi na hatimaye vurugu kwenye mikutano ya chama hicho"

  My Take

  The pandora box is now open.
  Inalekea fujo zinazotokea wakati wa mikutano ya M4C is by design, na matokeo ya fujo hizo yanaratibiwa invyoelekea.

  Sasa hapo sijui sera ziko wapi za kuigwa.
   
 20. j

  joely JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,030
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  mbona amechelewa sana kusema, au alikuwa anapanga na waajiri wake wa zaman
   
Loading...