Nyilawila autema ubingwa wa dunia (WBF) ili apambane na Cheka

Che Guevara

JF-Expert Member
May 22, 2009
1,236
346
Nyilawila aukana ubingwa WBF

Monday, 09 January 2012 21:01
Imani Makongoro, Mwananchi.

BINGWA wa dunia wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa duniani (WBF), Karama Nyilawila ametangaza rasmi kuutema ubingwa wake ili aweze kupambana pambano lisilokuwa la ubingwa dhidi ya Francis “SMG” Cheka mwishoni mwa mwezi huu.

Nyilawila anatakiwa kutetea mkanda wake dhidi ya bondia Ermis Cagri mwezi Februari 11nchini Ujerumani, lakini bondia huyo amesema kamwe hawezi kwenda huko kabla ya kupigana dhidi ya Cheka.

Pamoja na msimamo wa vyama mbalimbali kutotoa kibali kwa Nyilawila kupambana na Cheka ili aende kuuutete mkanda wake wa dunia, bondia huyo amesema anaamini ‘mikwara’ hiyo itamalizika tu na ndoto ya kupambana na Cheka itafanikiwa.

Nyilawila alisema hawezi kukaa na mkanda na kuwa na sifa za kimataifa bila kuwa na kipato chochote mpaka sasa.

Nyilawila alisema kuwa tangu apata fedha alipomshinda bondia Kreshmik Qato wa Albania Desemba 3 mwaka juzi mjini Spartaplatz, Prague, Jamhuri ya Czech, hajawahi kupanda jukwaani kuutetea mkanda huo wala kupambana pambano lolote.

“Mimi ngumi ndiyo fani yangu ya kupatia kipato, sasa baada ya kukaa muda mrefu bila kupata pambano, nimefanikiwa naambiwa kuwa natakiwa kwenda Ujeruman, kamwe sitaenda kwani tayari nimepanga kupambana na Cheka na promota amepatikana, sitabadilisha maamuzi haya,” alisema Nyilawila.

Alifafanua kuwa pambano lake dhidi ya Cagri limehairishwa zaidi ya mara nne, na mara zote hizo akiwa anajiandaa kwa ajili yake na kupoteza fedha na muda.

“Lakini hakuna mtu aliyekuwa tayari kunifidia baada ya kuingia gharama za maandalizi, ila wamekuwa mstari wa mbele niende huko, siwezi kuharibu heshima yangu kwa promota na mipango ambayo tumekwisha ifanya,” alisema.

Alisema kuwa anajua kutakuwa na maneno mengi, ila yeye anasimamia msimamo wake wa kucheza pambano dhidi ya Cheka.

Mpinzani wake Cheka alisema kuwa anachofahamu pambano lao liko palepale ni lazima acheze kwa kuwa mtoto amelilia moto mwenyewe.

Source: Mwananchi, Januari 10, 2012.

Swali:...Wadau hii imekaaje? Kutema ubingwa ili apambane na Cheka?
 
Back
Top Bottom