Maisha pesa
JF-Expert Member
- Nov 6, 2015
- 681
- 630
Nyie wanawake nani kawaroga?
Siku ya mechi ya nusu fainali Euro France vs Germany nilikuwa nimekaa baa moja maridadi pembeni ya jiji nikibarizi na glasi yangu ya wine huku macho yangu yakiwa makini kwenye tv kubwa ya inch kama 70 hivi.
Wakati mechi ikielekea ukingoni huku France wakiwa mbele 1-0 ghafla Antoine Griezmann akapachika bao la pili na kuwa 2-0. Kijana mmoja aliyekuwa mbele yangu aliruka kwa furaha huku akishangalia kuwa ameshinda milion 5 baada ya kubet. Sielewi ni wapi kilipotoka kikundi cha wanawake watatu waliovalia nguo fupi na laini zenye kuonyesha maungo yao wakaanza kumpepea kijana wa watu aliyeshinda milioni 5 huku wakimbusu na kumkumbatia na kumuinua kitini wacheze naye mziki.
Hakika niliyaona mapenzi ya ghafla kwa kijana huyo wakimmiminia kinywaji kwenye glasi picha kibao za mashauzi zikapigwa yaani ilikuwa ni vituko lakini baadae kijana alishtuka akaamua kuwakimbia make anaonekana hakuwa mkware.
Jamani nauliza tena wanawake nani kawaroga? Yaani hadi kwenye hela za betting? Pengine kijana alishajiwekea nia akishinda anunue kiwanja au afungue biashara ya saloon.