Kaveli
JF-Expert Member
- Dec 4, 2012
- 5,412
- 8,815
Sikumbuki ilikuwa mwaka gani exactly. Ila my memory draws a line kwamba ni kama miaka mitano hivi imepita. Siku hiyo ilikuwa ni mkesha wa mwaka mpya. Back in ze dei !
Tupo mitaa ya kati uswazi, kwenye banda la video la msela mmoja hivi mmakonde. Ni mida mibovu usiku mnene! Mmakonde kaaga kwao kusini kuja 'kuchukua maisha' jijini darisalama, ana'run bizinesi' mpaka night kali. Ni msela fulani in his early 30's hivi by that time, anaonekana kabsa keshakuwa 'profesheno' ktk harakati za kutafuta maisha through elimu mtaani dot kom. Kafuzu elimu ya mtaa. Makomredi wa uswazini nadhani mnanielewa hapo. Mbali na kideo, ndani ya banda huduma zingine kadhaa zinapatikana, kama vile maji ya kandoro, n.k. Banda halina madirisha, ila kuna feni kadhaa ambazo zinapepea kwa kujikongoja kama bendera ya Tanza, na zimejaa vumbi mpaka rangi zake halisi hazijulikani. Wenye afya za mkopo lazima utoke mle na mafua yaliotukuka, ila kwa wenye afya ngangari ilikuwa ni barida barafu.
Kabla ya usiku huo, jioni yake tulitoka kumzika mtu pale jirani mtaa wa 3. Braza kaka fulani hivi 'alikata kamba' siku hiyo ya kufunga mwaka. Alikuwa ni 'home-boy' mzawa wa eneo hilo. Hustler huyo alikuwa ni dereva texi. Kapiga sana mishe za texi ila mambo yakawa bado bila bila, si Yanga wala Simba. Channel hazisomi! Ikabidi abadili mbinu za kivita, akaapply kazi ya udereva serikalini kwenye Halmashauri fulani. Mungu si Mwanalizombe, jamaa akapata shavu la udereva serikalini. Maisha yakachange alhamdulillah. Mambo sasa yakakaa mkao, akaanza 'kucheza bila kuvunja goti' !
Kifo cha 'hustler' huyo ni baada ya kufumaniwa na mke wa mtu, kwenye geto la mshikaji wake. Walikuwa 'smart' kidogo kwa kukwepa guest/lodge, wakawa 'wanadinyana' kwenye geto la mshikaji wake ambae yeye hakuwa ameoa. Za mwizi ni arobaini. Siku ya msala ikafika. Wapo chumbani wanapeana uroda na kubembea paradiso. Wakafumaniwa live!! Mwenye mke alikuja na wahuni mob. Kisago kitakatifu. Za chini ya kapeti zikatonya kwamba jamaa hataisahau hiyo siku huko kaburini, maana wahuni walimfanyia 'undava' uliotukuka. Walimvunja 'duka' bila hiana, warume-ndago walikula 'jicho' ! Aliuguzwa siku mbili. Akadanja siku hiyo ya kufunga mwaka. Hakika aliufunga mwaka kwa style ya kusikitisha. RI.P.
Kwenye msiba, kama kawaida ya uswahilini, mengi yalisemwa huku tukiwa 'busy' kuufinya ubwabwa. Wahuni wa mtaa walitupia kanzu kuuubwa na ndizi mifukoni zinaning'inia. Yes... ukifa ni sikukuu. Kufa kufaana. Huku uswazini kwetu hakunaga mambo ya kuvaa mawani makubwa meusi wala mambo ya 'ekotitee' utadhani bongo-movie wamevamia msiba wa 'ushuani'. Hatunaga mbwembwe sie huku. Baada ya kushiba wali nazi, wazee walikuwa busy kucheza bao ili kusindikiza matanga hayo kwa masaa kadhaa.
Jioni Matanga yakaisha, wananchi wakatawanyika. Lakini akina mama wengi walisikika wakisononeka sana. Kwa kujirudia rudia, walisikika wakitoa kauli hizi: ''jamani wanaume hawa, sijuwi wana pepo gani huko chini kwenye zipu zao. Kafa kifo cha aibu sana jamaniii''. Mama mwingine mtu mzima akasikika anasema hivi: ''wanaume wengi wakishaanza kupata vipesa huanza mambo ya ajabu sana. Mungu alimjaalia akapata kazi, mwishoe akaanza uasherati...''. Marehemu aliacha mjane na mtoto mmoja.
Basi tukawa tunaendelea kuukaribisha mwaka usiku huo pale kwenye banda la video. Nyomi ya hataree mle ndani, kijasho chembamba na karaha ya kujambiana jambiana in silent-mode! Luninga tunazo majumbani mwetu, ila tunakuja kuminyana kwenye mabanda haya ya vichochoroni, tena kwa entrance fee! hahahaaa uswazi raha sana walahi. Mkanda wa mpira footballl (mechi ya marudiano) ulikuwa unafika ukingoni. Ukaibuka mgongano wa hoja, je ni mkanda gani ufuatie mida hiyo? Wadau wakasikika: ''baba tuwekee 'pilau' tule kwa nadharia''. Wadau wengine wakanena: ''aaargh wana acheni uduwanzi. pilau ya nini wakati tunauanza mwaka? nuksi hizo bhana! Wa Milazo (jina la mwenye banda) eeh, tuwekee aksheni yeyote ya kizungu bhana tuuanze mwaka fuleshi...''. Muvi ya action ya kizungu mixa black america ikawekwa. Tukaendelea kula burudani. Macho kodooo kwenye luninga utadhani tunatizama ziara ya kushtukiza ya kiongozi wa awamu ya tano! Vifua wazi, tunakaribisha mwaka mpya! Lol
Muvi likaendelea kwa kunogeshwa na 'ubashiri' wa Rufufu. Muvi likafika kwenye love scene fulani hivi ambapo mwanaume na mwanamke (blacks) wanaonekana kutofautiana. Pamoja na 'ubashiri' wa Rufufu, muvi ile ilikuwa na english caption zinapita chini ya screen. Basi yule mwanamke akamwambia huyo mwanamme kauli ambayo kwakweli mpaka leo huwa haitoki kwenye kumbukumbu zangu. Mwanamke alitamka hivi: ''THE ONLY SIMILARITY BETWEEN MEN & RATS IS THAT BOTH THEY ALWAYS SEARCH FOR NEW HOLES''.
Kauli hiyo huwa siisahau kabsa, kwa sababu EITHER wanaume tunasingiziwa tu kuhusu hilo OR ni kauli yenye some elements of truth ndani yake. Hasa nilipokumbuka na kile kifo ya yule hustler siku hiyo ya kuuaga mwaka.
Karibuni uswazi.
- Kaveli -